Budget Comparison

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Leo nikiwa kikazi Dubai ninasoma gazeti la Asubuhi GULF NEWS, JIJI la DUBAI latangaza budget yake ya 2021 kuwa ni US$ 15.5 Billions, Dubai lina wakazi 3.31m, Uchumi wa Dubai unategemea Biashara, Service Industry na Utalii; JIJI la tatu UAE la Sharjah Limetangaza budget yake ya US$ 9.1Billions, LINA WAKAZI 1.4 M, Uchumi wa Sharjah ni Biashara Services na wana GAS kiasi kidogo.

Hali ambapo Tanzania Nchi iliyo kubwa sana zaidi ya UAE, Budget yetu ni US$15.14 Billions, Na tuna fursa ya kuweza kushawishi Biashar kwa ukubwa zaidi, Tuna vivutio zaidi ya Nchi za Kiarabu zote ukizichanganya, Wao wana wananchi wasio pita million 2, na wageni 8million wanao fanya kazi na biashara.

Ninaishauri Serekali Yangu na Raisi wangu, tuache ujuaji mwingi, hebu tuwasome hawa rafiki zetu na tujaribu kuwaiga:

Dubai welcomed a record 16.73 million tourists in 2019, an improvement over the previous two years driven by soaring Chinese, Russian and Omani visitor numbers. The number of international visitors grew by 5.1 percent last year but is still short of its 2020 target of 20 million tourists.Jan 23, 2020 ( Dubai announces record tourism arrivals in 2019. )

SWALI JEE TUNAWEZA ITUMIAJE FURSA YA KUWEZA KUUTUMIA URAFIKI MZURI TULIOKUWA NAO NA HAWA MARAFIKI WATUPENDAO WA UAE, NA KUWEZA KUJIFUNZA WALIVYOFANIKIWA KULIFANYA JANGWA LAO LEO LIKAWA KIMBILIO LA ULIMWENGU MZIMA, KUWA NI PAHALI MUHIMU SANA PENYE RAHA, AMANI, NA SHOPPING NZURI NA KWA KILA UWEZO.

“In five years' time Oil in UAE will run out, but it has diversified its assets and interests enough with 95% of its income derived from tourism, property and music shops, other countries in the region should learn from what Dubai has done and they should beware that conventional fuel will begin to decline in the next.

( Oil in UAE is Running Out: It’s time Emiratis Prepare for a Brave New World - )
 
Mi mwenyewe niko YEMEN, huku TANDALE. Mpanga budget wetu mkuu anatueleza kwamba serikali yetu ya mtaa haina budget, ila ina makusanyo na matumizi tu, na vyote vinavyokusanywa vinaenda kwenye posho ya vikao mbalimbali vya mtaa.
Serikali yetu ya mtaa haijui idadi yetu sisi wakazi wake. Haijui changamoto zetu.

Haijui vipaombele vyetu. Uchaguzi uliopita tuligawiwa kanga zenye rangi ya Yanga na kofia zake, wakati wakazi wengi wa huku shida yao kubwa ni ukosefu wa lishe.

Akipita huyu anakupa kanga, akipita Yule anakuletea fulana. Akija mwingine kofia, yaani zawadi zinajirudia hizohizo. Nina doti 21 za kanga. Nitatengenezea bikini, g string, na chupi nikauze, lakini quality yake iko chini sana, wadada wa mji huu wanaweza kunitumia hata majini
 
Hawa Marafiki zetu, wao hawathamini sana kodi, wanaamini kuhakikisha kila mkazi, anatumia nusu ama robo tatu ya mapato yake nchini, vanachukua VAT 5%, Hakuna kodi nyengineo ila kuna malipo kama Municipality tax kwa kila receipt ya mahoteli, mkataba wa kodi za nyumba nk..
 
Utalii pekee ungeweza kututoa lakini kwa projection ya Ilani ya CCM ya watalii milioni tano ifikapo 2025 kwa nchi yenye watu millions zaidi ya sitini,sisi bado Sana
Utakuzaje utalii kwa kumtumia Stephen Nyerere?
 
Acha upotolo wa ki CCM wewe chukua pato lote la Dubai, Kisha gawa kwa idadi ya watu wake milioni 3.5 utapata kila mkazi wa Dubai ana kiasi gani?
unaona mlivyo viazi.
kwahiyo dubai kila mtu ana uchumi sawa na mwingine.
 
wakatu dubai inaanza kuchukua hatua za mabadiriko 1901 ili kuwa jiji la starehe duniani kufikia 2050,sijui tanzania tulikuwa na mkoroni wa rangi ipi mwaka huo!!.

leo miaka 120 tunageukia matokeo tu,na kuanza kulaumu,huku tukiwa tumesahau kwamba zikijengwa barabara nzuri hatutaki,zikinunuliwa ndege na kujengewa viwanja hatutaki,kitu tunataka ni kuona hela zikiwa zinapeperuka kwenye miti.

sisi ndio watz.
 
Usijifananishe na vitu ambavyo havikuhusu utajivimbisha afu hamna ktu,yaani n sawa sawa wewe kujifananisha na mbappe,au Rashford n wadg kwako lkn ustake kufanana nao kwa sabb n wakubwa kiuchumi ila n wadg kiumri
 
Kwani tunavyosema kila Mtanzania pato lake kwa mwaka ni chini ya milioni mbili kwani huwa mnamaanisha watanzania wote ndio kipato chao hicho? Nyie misisyemu mbona wasahaulifu hivyo?
ndio maana tunasema mahesabu ya wazungu sio msahafu au katiba,wanafanya wanachotaka wao kiwe,sio lazima uwe ndio uhalisia.

wao maisha chini ya $1.9 kwa siku wewe no masikini,sasa nikuulize shuilingi elfu 5 tz unafanyia vingapi??
 
Na tuna fursa ya kuweza kushawishi Biashar kwa ukubwa zaidi,
Kwa mihemko ya serikali ya jiwe. Kwamba RC, TRA, NEMC, polisi, OSHA, n.k wote wanageuka kuwa maadui wa mwekezaji.

Kila mwekezaji akiamka anakutana na kituko cha faini, haiwezekani tukawavutia kuja.
 
wakatu dubai inaanza kuchukua hatua za mabadiriko 1901 ili kuwa jiji la starehe duniani kufikia 2050,sijui tanzania tulikuwa na mkoroni wa rangi ipi mwaka huo!!.

leo miaka 120 tunageukia matokeo tu,na kuanza kulaumu,huku tukiwa tumesahau kwamba zikijengwa barabara nzuri hatutaki,zikinunuliwa ndege na kujengewa viwanja hatutaki,kitu tunataka ni kuona hela zikiwa zinapeperuka kwenye miti.

sisi ndio watz.
Ndugu issue sio Lini walianza, Mimi siku ya kwanza kutua Dubai ilikuwa september 1977, nikiwa kijana wa miaka 14, nikielekea India na mzazi wangu, kwa Gulf Airways. tulikaa wiki moja kwa ndugu wa kizanzibari, mji haukuwa na harakati hivyo, Dar ilikuwa zaidi ya Dubai. kitu wanachotuzidi ni utendaji na namna wanavyopigania kuwa bora No.1. kwa kila kitu. Best service, Best Facility, Fast implementation, na zaidi ya hayo Investments zinapewa vipao mbele vingi, total encouragement and support.

Hawa wana usemi toza hodi ndogo, kuimarisha uchumi, uwekezaji na utumiaji. Sisi tungekuwa tunatoza ushuru mdogo si tungekuwa RE-EXPORTERS wakubwa kwenye nchi zote za jirani.
 
Back
Top Bottom