Buchosa, Mwanza: Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumtupa ndani ya ziwa Victoria

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia wanawake wawili katika matukio tofauti likiwemo la mwanamke mmoja kumuua mwanaye.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema katika tukio la kwanza, mwanamke mmoja mkazi wa Kisiwa cha Nyamango, Kijiji cha Soswa katika Tarafa ya Buchosa, Nyamisi Bahati (27) anashikiliwa na polisi akituhumiwa kuumua mtoto wake, Sakimu Hassan mwenye umri wa miezi 7 kwa kumtupa ndani ya ziwa Victoria.

Msangi alisema tukio hilo lililotokea juzi saa moja usiku wakati mtuhumiwa alipotoka nyumbani kwake kwenda kuwasalimia wazazi wake huku ikidaiwa kuwa aliondoka akiwa na mtoto wake.

"Akiwa nyumbani kwao ghafla alitoka nje akiwa na mtoto wake, ilionekana kama anaenda kumbembeleza baada ya muda alirejea akiwa hana mtoto ndipo bibi yake alipoanza alipo mtoto", alisema Msangi.

Alisema baada ya kumhoji zaidi, baadaye mtuhumiwa alikiri kumtupa ndani ya ziwa Victoria.

Baada ya bibi kupokea taarifa hiyo ilimshtua na kuanza kupiga kelele kuomba msaada kwa watu ili waweze kusaidia kumuokoa mtoto huyo.

Kamanda huyo aliendelea kueleza kuwa majirani walikusanyika katika tukio hilo walimsaidia kutoa taarifa kituo cha polisi ambao nao walifika eneo hilo na kuanza shughuli ya uokozi hadi walipofanikiwa kuupata mwili wa marehemu.

Msangi alisema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mtuhumiwa ana matatizo ya akili ingawa bado wapo kwenye upelelezi na mahojiano kujua ukweli wa jambo hilo.

Katika tukio la pili, polisi wanamshikilia mkazi wa mtaa wa Malulu, Kata ya Igogo wilayani Nyamagana, Ghati Chacha (36) kwa madai ya kukutwa na pombe haramu ya gongo lita 23.


Chanzo: Mwananchi
 

rubii

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
11,428
2,000
Afadhali karudi kwa Mungu mapemaa, maana kwa adha za hizi dunia watu tunatamani tungetupwa mtoni tu kama huyo mtoto
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Unyama ulioje?

Na huyu mtoto aliteseka namna gani kifo chake. Inasikitisha
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
170,313
2,000
Ila kama ndugu walikua wanafahamu ana matatizo ya akili wangekua nae makini aah mtoto mdogo kateseka ndani ya maji mengi tena ya baridi kabisa. Pumzika kwa amani mtoto.
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Hapa hakuna cha ugonjwa wa akili wala nini. Asilimia kubwa wanawake ni wakatili mno ijapo wametuzaa, visa vya kutupa watoto vipo sana

JF. Kenya mwanamke amfungia mwanae ndani ya gari na kumuacha akafa huku akijiburudisha na mpenzi gesti.
 

Yegomasika

JF-Expert Member
Mar 21, 2009
12,986
2,000
Hapa hakuna cha ugonjwa wa akili wala nini. Asilimia kubwa wanawake ni wakatili mno ijapo wametuzaa, visa vya kutupa watoto vipo sana

JF. Kenya mwanamke amfungia mwanae ndani ya gari na kumuacha akafa huku akijiburudisha na mpenzi gesti.
Usihukumu, na wewe utahukumiwa! Kuna uwezekano mkubwa huyo mama ana ugonjwa wa akili!
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,822
2,000
Maskini katoto, pumzika kwa amani.....
Ndugu kama wanajua mama ana tatizo walitakiwa wamuangalie kwa karibu
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,900
2,000
jamii ingetambua mwanamke anapojifungua na kukosa malezi bora na upendo wa hali ya juu hasa kutoka kwa watu karibu zaidi mume wake anaweza pata uchizi,, nadhani tungeokoa matukio ya watoto kutupwa na kuuwawa ....

tujifunze kwa kweli kama jamii hata mwanao akizalia home mwanaume kamkataa mtie moyo muonyeshe bado ni wathamani tu,.... mambo mengi sana hupita kwenye vichwa vyetu kipindi hicho..

nyie wanume watoa mbegu jitahidini mkojoe sehemu mnayojua kuwa mnapenda mtatusaidia sana ..

mwanamke jamani tusali sana na kupenda hivi viumbe tokea tumboni huwezi waza kutupa hata aweje....

hospital jitahidi kutoa cancelling pia , mjifunze kuwajua wamama wapo kwenye hali gani hasa kimauhisiano mtaokoa wengi sana hasa wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ...

lala kwa mani mtoto ,,, inahuzunisha sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom