Mashindano ya namna hii yanatakiwa kuwa transparent zaidi kwa siku zijazo siyo kunongóna nongóna jukwaani wakati wa kutaka kutaja mshindi na zawadi. Aidha kweli pamoja na juhudi za madame Rita naona kama kweli ama alikuwa highly motivated au kuna kitu alitumia kabla maana hakutulia kabisa wakati wa kutoa comments na pia wakati wa kupresent zawadi.
Maneno ya majaji (Rita, Master J & Jabir) kwa washiriki hayako zaidi kiprofessional bali kishabiki. Payne alikuwa mzuri lakini hakustahili kushiriki full stop na hivyo mnapata mgogoro kujifanya kumpa # 3 wakati ni ninyi mlimuruhusu kufika hapo.
Je mmesikia yule mtoa zawadi (wa Kampuni ya simu) kwa mshindi wa 2 & 3 kasema kuwa Kampuni yao imejiunga na BSS kupromote VIJANA WA KITANZANIA , je Payne ni kijana wa Kitz?
Hizi ndio contraditctions ambazo Ms. Rita unatakiwa uziondoe toka mwanzao yaani kaa na Kampuni yako mpitie tena your Mission & Target group katika BSS! Maana kwa namna moja au nyingine ninyi Majaji ndio mmeonekana Wabaguzi lakini pia ni nyinyi mlimruhusu kuparticipate kitu ambacho kwa kweli hakustahili.