Brother ananishawishi nitembee na Mkewe kabisa wa Ndoa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Ni muda kiasi nmekuwa na changamoto hii katika mahusiano na brother wangu. Ni watu wa karibu sana tunaopendana mimi ni mdogo wake wa pili. Bro toka ameoa tena kwa kuchelewa kidogo ni miaka miwili na nusu sasa. Mimi nlioa zamani kiasi na nikafanikiwa kuwa na watoto watatu. Wawil wa kiume na mmoja wa kike.

Kaka yangu amehangaika sana kutafuta mtoto. Sana. Na bahati nzuri yeye kiuwezo yupo vizuri so pesa si tatizo kwake. Lakini ameekuwa akiwambiwa kuwa hana uwezo wa kumpatia mwanamke mimba.

Yapata mwezi sasa amekuwa akinifuata na kuniomba nitembee na mkewe nimpatie ujauzito then yeye alee na mkewe. Mara ya kwanza nlidhan amelewa. Haikuwa hivyo. Alikuwa sober kabisa. Akaja akanambia tena kuwa anaomba nimpatie mimba mkewe.

Last week alikuja na mkewe home tukaongea na baadaye akaomba tutoke wote watatu na mkewe tukae tuongee jambo.huko akanambia kuwa wamekubaliana na mkewe nifanye naye mapenzi siku za kupata mimba apate mimba.shemeji yangu alionesha kukubaliana na jambo hili kwa amani kabisa.

Nikawaambia wanipe muda nifikiri.nmefikiria sana nikawaambia kama wapo serious nawapa week moja kila siku wawe wanatuma meseji kila mtu kwangu akisisitiza jambo hilo. Kweli wamefanya hivyo. So limebaki kwangu. Mke wa bro ni mzuri sana tu. Ni mke ambaye hata mimi ngeweza mwoa. So tatizo si mvuto...she is attractive and so sexy. Nawaza hili jambo nifanyeje?

Mke wangu sijawambia. Wazazi hatujawaambia. Ni mimi, bro na shemeji yangu tu ndo tunafahamu

NB: Wadau, mimi ni Mwandishi tu mwenye mkasa ni mtu mwingine.
 
Ha ha haaa, afadhali hapo mwisho umesema siyo wewe, maana nilikua nasoma huku nafikiria ile comment yako iliyojaa fact kwenye mkasa wa Babu Seya kule.
 
Wakati wanaume wengine wakikataa kuoa wanawake waliozaa na kuwadharau hata kama anamuheshm kias gani,Huku wanaume wengine wanatafuta watoto kwa juhudi zote hadi huruma

Aisee MUNGU huyu

Mwambie tu bro avumilie ndo mitihani yenyewe hiyo unaweza pewa kila kitu ukanyimwa kitu kidogo tu,amshkr tu Mungu na aamini ni M/Mungu pekee ndo anaweza kufanya yasiyowezekana yakawezekana
 
Hilo siojambo geni katika ulimwengu huu Mimi nimemzalishia bro wangu watoto Wawili mapacha tena nimpangu Wa watu Wawili tu Mimi na Shem alipoona amekaa mdamrefu hajapata mimba akijicheck yeye alishawahi kujata MTOTO namwanaume mwengine walipotemana bro akamuoa anamiaka nae 6 alikua hajapata MTOTO alinibembeleza sana na akanisisitiza sana kua hakupenda kumbambikia brother MTOTO kutoka nnje yaukoo wetu nikaona nijipindue tumepata pacha nimefanana nao nibalaa nahisi brother ameustukia mchezo ila namna yakumuuliza mkewe au Mimi inakua shida maana sina mazoe saana nashem maana maranyingi anamwambia Shem mbona watoto wamefanana sana namdogo wangu Shem hua anamjibu nyinyisidamu moja mbona nyie mmefanana? Nahofia siku wakigombana sijui Shem ataropoka yaani nipo njia panda huu nimkasa wakweli ambao umetokea kwangu Mimi mwenyewe na sio muandishi nilietumwa kufikisha ujumbe.
 
Bora umeandika kwamba wewe ni mwandishi tu maana ningekuchana kwa kutuletea script za bongo movie.
 
Back
Top Bottom