Bro Hamis nisamehe

Mambo yameshaharibika usiwe fala, jamaa kashajua kama ni wewe na lazima ahisi kuwa umeshampiga mzigo mke wake sana hivyo hama haraka.
 
Tafuta kale ka mbegu ka kuharisha wakikukamata tu we kameze, Piga uharo wa kufa mtu mpaka wapoteane
 
Tafuta kale ka mbegu ka kuharisha wakikukamata tu we kameze, Piga uharo wa kufa mtu mpaka wapoteane
Asante mkuu hivi ipoje hio kwasababu Kuna dogo naskia alikamatwa na dereva wa magari makubwa walikua wamfanye mbaya dogo akanya Sana wakamuacha
 
Habarini wadau wa jukwaa pendwa,

Kama kichwa Cha habari hapo kinavyosema.

Katika shughuli zangu nilikutana na dada mmoja ambaye kiumri kanizidi sana japo hajachuja yupo kwenye ubora.

Na yeye ana saloon yake ya kike kwahiyo hana njaa za ajabu. Changamoto kubwa ni kwamba kazi yangu na yake zinaingiliana yani tupo kwenye kamati ya sherehe, sasa mara nyingi tunapopata sherehe basi Kila mwanakamati anapewa kazi inayomfaa.

Kama una genge la viungo na mbogamboga basi tenda zote za hivyo unapewa wewe, kwahiyo mara kadhaa tunawasiliana hata Kama hatuna shughuli ila tunapeana michongo pia nje ya kamati.

Sasa Mimi sikuwahi kumuona akiwa na mume wake hata siku moja na sikuwa nikimjua ila kwasababu ni mtu mzima niliamini ana mume. Mwaka Jana December alianza kunitongoza na kuniahidi vitu vingi sana nilichat nae WhatsApp akanitumia picha zake nyingi zinazofaa na zisizofaa.

Kwakweli niliingia mtegoni nikamtamani sana tukapanga sikukuu ya mwaka mpya tuonane maeneo ya mjini (Tanga)
Kabla ya muda nikampigia simu kumwambia kuwa natangulia na simu haikupokelewa nikatuma ujumbe sms Kisha nikaondoka.

Baada ya muda nikajibiwa sms yangu, jibu lilisomeka (sawa mpenzi nakuja). Dah nilifurahi Sana nikajua nishatoka kimaisha kwasababu aliniambia kuwa mumewe kafariki hana mume

Nilipofika mjini barabara ya 16 nikampigia hakupokea akatuma sms kuniambia chukua chumba lakini isiwe katikati ya mjini nenda hata Mikanjuni huko akanitumia 20,000 dah meno yote njee nkajua leo ni leo Kila saa naangalia picha zake alizo nitumia.

(Mke wa mtu sumu)
Baada ya kufika Mikanjuni nikapata guest nzuri tu nkalipia nkaingia nkaoga vizuri nikatoka kwenda kula nikampa ramani yote mpenzi wangu. Lakini kwanini hapokei cm anataka tuchat tu?

Kwasababu sikuwa na begi wala mzigo wowote nilitulia sehemu ya nje kuna bar, nikaagiza ugali mkubwa dona wakati nakula sms ikaingia "upo ndani baby?' nikajibu ndio. Nilijibu kwasababu sikumuona hapo bali niliona wanaume wanne wawili nawajua kwasababu tunatoka Kijiji kimoja tukasalimiana pale wakaniuliza vipi unamchongo gani?

Nkacheka kidogo nkawaambia Kuna ndugu yangu nimekuja kumsalimia, sasa hayupo kwahiyo napata msosi hapa nirudi
Bro mmoja ambae walikua wanamwita Kaka Hamis kwenye mazungumzo yao akasema wazee twendeni yupo ndani
Basi jamaa wakaniaga wakaingia wote.

Nikanyanyuka nikasepa, Nnmerudi home na wamenikosa lakini wapo kimya hawajaniambia chochote
Wasiwasi wangu je wanapanga nini? Je bro Hamis ambae inavyoonekana amekuja likizo atahisi mimi ndo muharibifu
Story nilozopata mtaani ni kwamba Kuna dogo alimtumia mke wa Hamis sms lakini simu alishika Hamis kwahiyo Hamis akamjibu huyo dogo wakachati lakini alivyomkosa alimpiga Sana mke wake na akaapa lazima ampate huyo kijana.

Wadau nifanyaje jamaa yupo serious
Sasa dogo mbona umeachia codes zote?? Kama bro Hamis ni member humu ni rahisi kukujua
 
Back
Top Bottom