Bro Hamis nisamehe

kipachaibwe

Member
Dec 11, 2020
36
71
Habarini wadau wa jukwaa pendwa,

Kama kichwa Cha habari hapo kinavyosema.

Katika shughuli zangu nilikutana na dada mmoja ambaye kiumri kanizidi sana japo hajachuja yupo kwenye ubora.

Na yeye ana saloon yake ya kike kwahiyo hana njaa za ajabu. Changamoto kubwa ni kwamba kazi yangu na yake zinaingiliana yani tupo kwenye kamati ya sherehe, sasa mara nyingi tunapopata sherehe basi Kila mwanakamati anapewa kazi inayomfaa.

Kama una genge la viungo na mbogamboga basi tenda zote za hivyo unapewa wewe, kwahiyo mara kadhaa tunawasiliana hata Kama hatuna shughuli ila tunapeana michongo pia nje ya kamati.

Sasa Mimi sikuwahi kumuona akiwa na mume wake hata siku moja na sikuwa nikimjua ila kwasababu ni mtu mzima niliamini ana mume. Mwaka Jana December alianza kunitongoza na kuniahidi vitu vingi sana nilichat nae WhatsApp akanitumia picha zake nyingi zinazofaa na zisizofaa.

Kwakweli niliingia mtegoni nikamtamani sana tukapanga sikukuu ya mwaka mpya tuonane maeneo ya mjini (Tanga)
Kabla ya muda nikampigia simu kumwambia kuwa natangulia na simu haikupokelewa nikatuma ujumbe sms Kisha nikaondoka.

Baada ya muda nikajibiwa sms yangu, jibu lilisomeka (sawa mpenzi nakuja). Dah nilifurahi Sana nikajua nishatoka kimaisha kwasababu aliniambia kuwa mumewe kafariki hana mume

Nilipofika mjini barabara ya 16 nikampigia hakupokea akatuma sms kuniambia chukua chumba lakini isiwe katikati ya mjini nenda hata Mikanjuni huko akanitumia 20,000 dah meno yote njee nkajua leo ni leo Kila saa naangalia picha zake alizo nitumia.

(Mke wa mtu sumu)
Baada ya kufika Mikanjuni nikapata guest nzuri tu nkalipia nkaingia nkaoga vizuri nikatoka kwenda kula nikampa ramani yote mpenzi wangu. Lakini kwanini hapokei cm anataka tuchat tu?

Kwasababu sikuwa na begi wala mzigo wowote nilitulia sehemu ya nje kuna bar, nikaagiza ugali mkubwa dona wakati nakula sms ikaingia "upo ndani baby?' nikajibu ndio. Nilijibu kwasababu sikumuona hapo bali niliona wanaume wanne wawili nawajua kwasababu tunatoka Kijiji kimoja tukasalimiana pale wakaniuliza vipi unamchongo gani?

Nkacheka kidogo nkawaambia Kuna ndugu yangu nimekuja kumsalimia, sasa hayupo kwahiyo napata msosi hapa nirudi
Bro mmoja ambae walikua wanamwita Kaka Hamis kwenye mazungumzo yao akasema wazee twendeni yupo ndani
Basi jamaa wakaniaga wakaingia wote.

Nikanyanyuka nikasepa, Nnmerudi home na wamenikosa lakini wapo kimya hawajaniambia chochote
Wasiwasi wangu je wanapanga nini? Je bro Hamis ambae inavyoonekana amekuja likizo atahisi mimi ndo muharibifu
Story nilozopata mtaani ni kwamba Kuna dogo alimtumia mke wa Hamis sms lakini simu alishika Hamis kwahiyo Hamis akamjibu huyo dogo wakachati lakini alivyomkosa alimpiga Sana mke wake na akaapa lazima ampate huyo kijana.

Wadau nifanyaje jamaa yupo serious
 
Kuna mpemba mmoja jirani hapa kamshushia jamaa boooooonge moja la busha la puππbu moja, hii ni baada ya kugundua kuwa jamaa alikuwa akimtoππbea mkewe (Mrs. Mpemba) na katika kumkadiria akaona kwa kipigo hatomuweza.

Jiandae kisaikolojia
Hii imetokea wapi huko mkuu?huyo jamaa alijaribu kutafuta tiba yake?
 
😂😂😂😂😂😂😂

Wangekudaka sikukuu yote wangekula na wewe!
Kama ni mlokole nenda ukatoe sadaka ya shukrani kanisani
 
Sasa kama umeshajua ni kazi ya mtu mkuu unatafuta nini zaidi???

Achana nae kula kilicho jasho lako, ama sivyo ukitaka kula basi jitahidi kutembea n mafuta yatakusaidia mkuu
 
Jiandae kupakwa "Rays" hamna namna ingine, ikibidi hama mtaa kabisa mapema.
 
Mbona umeshajiweka wazi kabisa... Sasa wewe msubiri bro hamisi hapo ulipo
 
mwanakulifind mwanakuliget, anza kutembea na box la mafuta ya nazi kabisa kama KY hutapata.
 
usiogope na wewe kuwa serious omba pambano la ngumi na huyo Hamis, mshindi analala na pisi siku hiyo
 
Back
Top Bottom