BRELA NA UOZO WAO

BRELA NA UOZO WAO

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
878
Reaction score
2,382
Brela imekuwa mwiba kwa sasa, hawatoi huduma kama hujawapa kakitu.
Kumekuwa na hawa mawakala wanaosajiri makampuni na majina ya biashara. sasa ukiwatumia wale wanakwambia weka na 50,000 ya kupush kule ndani.

Sasa ikitokea hujawatumia hawa mawakala ukienda Brela ORS mwenyee ukatuma maombi yatasubiri sana aisee. yaani wale walioko kule ndani hawa deal na maombi ya kwenye mfumo kama huja push na njia pekee ya kupush ni lazima uwape mawakala wakufatilie jambo lako.

Hii inakera sana hasa pale unapokuwa umelipia gharama zote zinazohitajika. Bora ingekuwa unalipia baada ya kupatiwa huduma unaweza kuahirisha.

Kibaya zaidi mfumo wa Brela haukuruhusu kufanya maombi mapya kama la zamani halijamalizwa. So hata ukitaka ulifute utafute watu wakusaidie bado utakwama.
 
Back
Top Bottom