mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,073
Brela,Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ni moja ya taasisi kongwe inayopaswa kuliingizia taifa fedha nyingi kupitia tozo na malipo mbalimbali yahusuyo usajiri wa biashara,makampuni,viwanda,haki za kibiashara na uhakiki husika.
Tuhuma za wizi wa tozo na malipo katika taasisi za serikali kupitia mabenki hasa yenye mifumo ya uhakiki wa kitehama limekuwa tatizo lenye mizizi na vyombo vya usalama vyapaswa kutupia jicho la tatu na la nne ili kuepusha fedha za umma kudumbukia katika mifuko ya wenye uchu wa kujitajirisha pasipo kujali maendeleo ya taifa.Mfano wizi wa tozo za mamlaka ya bandari { TPA}kupitia mabenki yenye heshima ni moja ya madoa ktk mifumo inayotumika.
Makampuni na biashara nyingi zimekuwa zikisajiriwa na taasisi yetu pendwa ya Brela kila iitwapo leo {siku za kazi} na malipo kufanyika kupitia akaunti kadhaa kama ambavyo imekuwa ikiainishwa kupitia ankara zinazotolewa kieletroniki kupitia mfumo wa tehama na baada ya wateja kuweka pesa katika akaunti husika taarifa za ujumbe mfupi uingia katika simu za viganjani kuthibitisha kupokewa kwa malipo husika na risiti yenye nembo ya BRELA hutolewa baada ya mteja kuwakirisha hati ya malipo benki hivyo mchakato wa usajiri kukamirishwa baada ya siku mbili mpaka tatu ila kwa wenye haraka sana na wenye kutoa sadaka ndani ya siku moja kila kitu kinaweza kukamirishwa{pongezi kwa maboresho kwa muda unaotumika kuwa mchache tofauti na huko nyuma}.
Inasemekana pamoja na mihamala mingi kufanywa na makampuni mengi kusajiriwa lakini fedha zilizopo kwenye akaunti za BRELA haziwiani na zinazopaswa kuwepo kwa maana zilizopo ni chache mnoo..Kasheshe!!!.Wasiwasi,Baada ya malipo kufanywa Benki na mteja kupewa nakala za uthibitisho ujumbe mfupi tajwa unaotumwa na mfumo tehama kuthibitisha malipo hauitaji taasisi ya BRELA bali BLARE/BRALE ambayo kimsingi sio BRELA.
USHAURI:
1. Ikithibitika ya kuwa kweli kuna utofauti wa kina,Uhakiki wa kina ufanywe na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
2. Hatua za kinidhamu ziwalenge watumishi wasio waaminifu pekee na mitandao ya ndani na nje.
3. BRELA ifinyangwe upya ili kukidhi haja za uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara/uwekezaji Tanzania likiwepo la mchakato wa usajiri na upataji leseni.
4. Leseni zote za biashara na uwekezaji zitolewe na Brela kwa mfumo kitita kwa kuiwezesha BRELA kuwa na ofisi katika Manispaa {Mapato ya usajiri na utoaji leseni katika manispaa yagawanywe kwa BRELA na manispaa husika}.
5. BRELA iwe na dawati mtambuka linalohusisha uratibu wa uwekezaji na biashara mahususi {Viwanda,Miradi mikubwa}.
6. Mifumo ya tehama iboreshwe ili kufanikisha upatikanaji wa taarifa kitita kwa malipo nafuu.
7. Kutengenezwe mfumo mtambuka unaohusisha usajiri wa biashara/kampuni na upataji wa usajiri ktk masuala ya kodi {TIN/VRN-TRA} na Utoaji leseni.