BRELA inakimbiza wawekezaji

Mm nina kz yangu toka mwaka jana May hadi leo kila mara marekebisho hayyaishi
 
Naunga mkono hoja hata mm nimezungushwa sana na hao BRELA zaidi ya mwezi.
Ni ukanjanja sio professional zinazofanya kazi.
 
Umeandika kwa ufasaha sana nadhani wahusika watalifanyia kazi.
Kila ofisi ya Serikali hivi sasa ni UKIRITIMBA tu. Nadhani wanamhujumu Magufuli kiaina, itachukua muda sana Magufuli kugundua watendaji wanamhujumu and infact wanaoihujumu taifa, Magu yupo leo lakini kuna siku ataondoka eidha kikatiba au kwa mapenzi ya Mungu. Lakini damage ambayo watumishi wataacha itakula vizazi na vizazi
 
Unafikiri ni kwanini wanamhujumu. Kwa maoni yangu nadhan wanahujumiana.
 
Mkuu ni aibu sana,hapo CHADEMA watakuwa wanahusika kuhujumu UWEKEZAJI 🤣🤣🤣🤣 M-5 TENA 😃😃😁😁🤣🤣🙏🙏🙏
 
Mkuu ni aibu sana,hapo CHADEMA watakuwa wanahusika kuhujumu UWEKEZAJI 🤣🤣🤣🤣 M-5 TENA 😃😃😁😁🤣🤣🙏🙏🙏
Utakua unawaongelea wale kina Lord waliotupostia picha hapa wakati wa kupiga kuru wakatuonyesha kadi ya CCM na pembeni kura kwa Tundu
 
Kuna ujinga sana ....online karibia zote hata Latra wanakuzingua hivyo hivyo ili uende ..usajili magari wakiona yako mengi kidogo lazima uende ........ili muende sawa
 
kuna madogo ukitoa kitu kidogo siku 2 tu unapata usajiri wapo pale chini Brela.mimi mpaka sasa maombi 3 tofauti nimelipa .mpaka leo akuna kitu
 
BRELA imekuwa taasisi ya ovyo kabisa wakati huu! Ni bora enzi huko nyuma tunapanda lifti zao zilizokuwa na dereva pale ushirika!
Kwa uchungu nasema hivi nilianza ku- update taarifa za kampuni yangu toka mwaka jana tarehe 11/04/2020 ! Kila niki- submit document wanaleta issue mpya ! Unasubmit baada ya siku tatu wanarudisha na wana- rise issue mpya hadi mwaka ukaisha nikachelewa ku- submit documents za kuomba leseni mahali.

January hii wameniletea invoice baada ya kufanya assessment nikajua nimekamilisha nikalipa karibia milioni 1.5 wakaniambia ni- upload pay in slip ya malipo nikafanya hivyo!

Baada ya siku 3 naangalia ili niendelee na hatua nyingine nakuta wananiambia ni- upload company consolidation form nimewambia nilishafanya hivyo mpaka nimefanyiwa assessment na nimelipa hawataki kunielewa kabisa! Niameanza mchakato upya! BRELA ni taasisi ya HOVYOOOOOOOOOOOOOOO KABISA!
 
Aisee iyo rudisha ondoa ongeza inakera sana hawapo kwaajili ya kusaidia watu wenye nia ya kuanzisha biashara hawa jamaa hawajui maaana ya muda kabisa!

Unaweza cheza nao miezi zaidi ya miwili

Kwa mtu ambaye alisha wahi kusajili anajuwa kabisa apo umesema 100% ukweli
 
Hii nchi Kuna watumishi wanaihujumu. Brela ni namba moja.

Kama mheshimiwa raisi anasoma hii meseji nakuomba uwafunge mtendaji mkuu wa Brela na Watumishi wengine wa brela. Wasihamishwe kazi ila wafungwe gerezani.

Mimi nilisajiri kampuni kwa miezi mitatu na kulikuwa Hakuna sababu yoyote ya msingi. Imagine eti unarudishiwa ufanye marekebisho kwa kutokuweka mkato kwenye sentence. Najua watakuja humu kujitetea ila serikali siku moja itume watu wa usalama pale Brela makao makuu wavhunguze vilio vya watu.

Hivi watu wa usalama hawayaoni yanayoendelea Brela? Kwanini wasifungue kampuni feki walau 5 waone tunayoyasema Kama ni kweli au si kweli?

Huduma kwa wateja ni mbovu unaweza kupiga simu ukiwabishia Kitu wanakata simu. Customer service department ya Brela ni ya hovyo kabisa kusahi kutokea duniani.

Bila watu kuwa wanafungwa kwa kuisababishia serikali hasara Kama hizi sidhani Kama huu uzembe utakuja kuisha serikalini.

 
Mwaka Jana nilitaka kufungua kampuni Marekani kupitia Jimbo la Delaware Kama domestic company.

Ila kilichonishangaza ni jinsi mfumo wao ulivyokua direct, yaani kama una documents zote ambazo zinatakiwa ndani ya siku moja unakamilisha kila kitu under usd 400.

Ila ukija BRELA utasumbuliwa sana kuna saa najiuliza tunakwama wapi, tunasundwaje kuwa na mfumo ambao uko direct kama nchi za wenzetu.
 
Kwanini unapenda kuifananisha Marekani na Tanzania? Hao jamaa wapo very advanced kuliko nchi nyingi sana hapa duniani.

Marekani wanapiga kura ya Veto huko UNSC. Tanzania wanazo hizo nguvu za kisiasa?

Matatizo ya Afrika yanahitaji ufumbuzi wa kiafrika na sio kila kitu kuiga kutoka Ulaya na Marekani.
 
Ninaowateua Wameshindwa Kufikiria Nje Ya Box. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Ninaowateua Wameshindwa Kufikiria Nje Ya Box
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Huzijui kero za brela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…