Babylon
JF-Expert Member
- Feb 5, 2009
- 1,332
- 82
Ndugu watanzania jana tu hapa nilitowa fikra za kulisaidia taifa na ulimwengu kwa ujumla, kwa kuitaka nchi yetu iweke sheria ya kuwatumia watu walio hukumiwa vifo badala ya kuwauwa wawe wanatumika katika Maabara kujaribia madawa yatakao vumbuliwa kwa kinga au tiba ya Binadamu, kwa mfano hawa wezetu wamevumbuwa chanjo hii na kama sisi tutavumbuwa aina ya madawa yatakao weza tibu binadamu wahukumiwa vifo wawe ndio wa kwanza kujaribia .
Chanjo ya HIV yapunguza maambukizi
Chanjo imejaribiwa kwa wanawake na wanaume wasioathirika nchini ThailandWatafiti wanasema kwa mara ya kwanza chanjo ya UKIMWI iliyofanyiwa majaribio imeweza kupunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.
Chanjo hiyo ambayo ni mchanganyiko wa chanjo mbili zilizofanyiwa majaribio hapo awali, iligaiwa kwa watu 16,000 nchini Thailand.
Watafiti hao wamesema imepunguza kwa takriban theluthi ya hatari ya kuambukiza ukimwi, virusi vinavyosababisha ukimwi.
Imesifiwa kuwa ni hatua muhimu hasa katika nyanja ya kisayansi, licha ya kuwa chanjo hiyo bado ina safari ndefu ya kutumika duniani kote.
Utafiti huu ulifanywa na jeshi la Marekani na serikali ya Thailand kwa zaidi ya miaka saba kwa watu waliojitolea.
Watu hao waliojitolea walikuwa wanawake na wanaume wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 30 katika maeneo yaliyoathirika sana na ugonjwa huo huko Thailand.
Chanjo imejaribiwa kwa wanawake na wanaume wasioathirika nchini Thailand