Breaking news: Uchaguzi wa serikali ya mtaa wa migombani waingia kwikwi mara baada ya afisa

LJ BLOG

Senior Member
Jul 24, 2011
194
151
[h=3] UCHAGUZI WA SERIKALI YA MTAA WA MIGOMBANI WAINGIA KWIKWI MARA BAADA YA AFISA MTENDAJI WA KATA YA SEGEREA KUJA KUTANGAZA KUSITISHA UCHAGUZI[/h]
IMG_8472.JPG


Wakazi wa Mtaa wa Migombani, Uliopo Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka gari la Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza kusitisha uchaguzi wa serikali ya mitaa kimya kimya.
IMG_8519.JPG

Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa kawekwa mtukati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila sababu ya msingi. waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo cha kupigia kura cha Migombani.
IMG_8466.JPG

Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea
IMG_8604.JPG

Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi wa Migomabni akielezea sababu za kusimamisha uchaguzi huo kwa muda kutokana na kusubilia barua ya kumtaka kuendelea na uchaguzi kutoka kwa afisa mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka kujaribu kusitisha Uchaguzi huo kwa kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
IMG_8563.JPG

Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.
IMG_8581.JPG

Hii ndio barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea inavyosomeka ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi wa migombani kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa uchaguzi unaendelea
IMG_8522.JPG

Afisa mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila sababu za msingi
IMG_8543.JPG

Wakazi wa Mtaa wa migombani, Kata ya Segerea wakimzuia Afisa mtendaji huyo kuondoka mpaka atangaze tena kuwa uchaguzi unaendelea.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog


Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.


Hali ya Kushtusha imetokea katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani Mara baada ya Afisa Mtendaji huyo kuja na kutangaza kimyakimya Kuwa UChaguzi huo umesitishwa, Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kusikia ndipo walipoanza sasa kutafuta mchawi na kumtia nguvuni afisa mtendaji huyo wa mtaa kwa kutaka kujua sababu za msingi zinazopelekea yeye kuja kutangaza kusitisha uchaguzi huo.

Afisa mtendaji huyo baada ya kuulizwa sababu za msingi alijitetea kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya ilala. Mara baada ya Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna dalili za kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo walipomuweka mtu kati na kumtaka Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa maandishi kuwa uchaguzi unaendelea ndipo wakazi hao walipomuweka mtu kati na kuhakikisha anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.

Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kwenda nae katika ofisi ya kata kwaajili ya kugonga muhuri kuthibitisha Uchaguzi huo kuendelea ndipo uchaguzi ukaendelea na muda huu zoezi la kuhesabu kura linaendelea

SOURCE: LUKAZA BLOG
 
Kata ya vingunguti pia uchaguzi umeghairishwa mpaka wiki ijayo kisa uchache wa karatasi za kupigia kura
 
ccm wameona wanashindwa wanaanza kutumia ubabe wangempiga huyu mpumbavu
 
Kata ya vingunguti pia uchaguzi umeghairishwa mpaka wiki ijayo kisa uchache wa karatasi za kupigia kura
huu uzembe kwa serikali ya ccm hawapo makini kwani wakati watu wanajiandikisha hawakupewa idadi
 
Back
Top Bottom