Breakfast yako kuu kwa sasa ni ipi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,997
46,092
Wengine kila asubuhi chai Mkate wengine hupendelea Viazi mviringo kila asubuhi na wengine kiporo cha wali.
Mimi Kwa mazingira ninayokuwepo asubuh siwezi kukwepa Mihogo Kama mnavojua cassava Kwa sasa ndo ipo on chart bila kuchoka Maharage na Juice ya passion. Kwanini kwanza navikubali vitu hivo

Juice ya Passion ina vitamini C nyingi, ambayo ni antioxidant inAsaidia kulinda mwili .Vitamini C inaongeza kinga ya mwili, mwili unanyonya madini ya chuma zaidi kutoka kwa vyakula vinavyotokana na mimea, so juice yangu hio inaboresha uwezo wa mwili wa kupambana na maambukizi mwilini.

Ukija kwenye cassava hapo una kalori nyingi na wanga nyingi na vitamini na madini pia. Na wenyewe una vitamini C, thiamine, riboflauini n. k ingawa Kati ya muhogo na kiazi kitamu ambacho kipo juu Kwa nutrients ni kiazi kitamu.

Maharage hapo ndo penyewe sasa uhakika kwenye Protini ambayo ni kirutubisho muhimu kutengeneza mwili pamoja na folate. Maharage ni mazuri mnoooo Kwa afya ya moyo.yanapunguza hatari ya saratani,kisukari na mwisho kabisa hayana cholesterol.. Me daima nitakula Maharage hakuna cha vidonda vya tumbo wala kiungulia. Me nayatandika Mpaka mwisho.

Tubadilishane uzoefu we unakula nini asubuhi mara nyingi nyingi.

DSC_0195.JPG
DSC_0087.JPG
 
Wengine kila asubuhi chai Mkate wengine hupendelea Viazi mviringo kila asubuhi na wengine kiporo cha wali.
Mimi Kwa mazingira ninayokuwepo asubuh siwezi kukwepa Mihogo Kama mnavojua cassava Kwa sasa ndo ipo on chart bila kuchoka Maharage na Juice ya passion. Kwanini kwanza navikubali vitu hivo

Juice ya Passion ina vitamini C nyingi, ambayo ni antioxidant inAsaidia kulinda mwili .Vitamini C inaongeza kinga ya mwili, mwili unanyonya madini ya chuma zaidi kutoka kwa vyakula vinavyotokana na mimea, so juice yangu hio inaboresha uwezo wa mwili wa kupambana na maambukizi mwilini.

Ukija kwenye cassava hapo una kalori nyingi na wanga nyingi na vitamini na madini pia. Na wenyewe una vitamini C, thiamine, riboflauini n. k.... ingawa Kati ya muhogo na kiazi kitamu ambacho kipo juu Kwa nutrients ni kiazi kitamu...

Maharage hapo ndo penyewe sasa uhakika kwenye Protini ambayo ni kirutubisho muhimu kutengeneza mwili. ..pamoja na folate. Maharage ni mazuri mnoooo Kwa afya ya moyo.yanapunguza hatari ya saratani,kisukari na mwisho kabisa hayana cholesterol.. Me daima nitakula Maharage hakuna cha vidonda vya tumbo wala kiungulia. Me nayatandika Mpaka mwisho.
Tubadilishane uzoefu we unakula nini asubuhi mara nyingi nyingi..
Mimi hupendelea kiporo cha ugali ninakichoma kwenye jiko la mkaa nakula na dagaa wa kukaanga kwa mawese nashushia na maji bardiii.
 
Chapati mbili, au vitumbua vitatu, au maandazi matutu na kikombe kimoja saizi ya kati inatosha. Nikibadilisha nakunywa supu bakuli moja na idadi ya hivyo vitafunwa hapo juu inatosha. Au vipande viwili vya mihogo/viazi vitamu kwa chai tosha
 
Back
Top Bottom