Brands zinazoonekana kwenye Korean dramas

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
522
1,000
Ushawahi kuangalia series ya kikorea alafu ndani yake ukaona brands mbalimbali kama Subway, Samsung, KIA au hata Lipstick?

Usichanganye, sio kwamba ni bahati mbaya La hasha! ile ni makusudi na ni njia mojawapo ambayo Korean dramas inatengeneza pesa kwa sababu kulingana na NewYork Times wanasema Brand Placements zinagharimu takribani USD 900,000 kwenye series moja ya kikorea.

Brand placements inatokea pale ambapo bidhaa fulani inaonekana kwenye series au movie kama ni kitu cha kawaida kumbe ni tangazo.

Kwenye series kwa mfano, unakuta watu wanafanya kikao KFC au Subway au wanaonesha dhairi shairi kuwa wanatumia kinywaji fulani. Sasa kinachofanyika pale ni kwamba zile brands zinazoonekana pale zinalipa watayarishaji wa filamu ili brands zao zionekane.

Kwa Tanzania kwa mfano kipindi Cha Dadaz cha EATV ukiangali pale kwenye set kwa nyuma wanaonesha Pads kwa ajili ya wadada. Ile ni brand Placement.

CILIN CLARK Country Director wa Subway nchini Korea Kusini anasema tangu waanze kuonesha bidhaa zao kwenye series kama Goblin na Misaeng basi mauzo yalipanda sana. Japo hakutoa maelezo kamili yalipanda kwa asilimia ngapi lakini alisema tu yalipanda.

Mfano kwenye series ya Descendants of the sun Subway Korea ilitumia takriban USD Million 2 kuonesha bidhaa zake tu, hiyo ni mara tatu ya kiwango cha kawaida kwa ukweli ni kwamba watengeneza series wanafaidika sana na mtindo huu wa matangazo.


Ifuatayo ni orodha ya series ambazo zimeshawahi kutumia brand placement :

1) GOBLIN
Kwenye Goblin hapa kampuni ya SUBWAY ilijitangaza sana ambapo Sunny character kwenye series aliigiza kama mmmliki wa mgahawa huo ulioanzishwa huko Connecticut nchini Marekani.

Ukiachana na Goblin pia series kwenye series ya Crash Landing On You mgahawa wa Subway pia ulionekana.

2) VINCENZO

Yes, hii series ndio naiangalia sasa hivi na of course sijaimaliza bado lakini kuna brands pia zimeonekana humu kama ZIHAIGUOI ambayo ni brand kutokea China.

Baada ya brand hii kuonekana sana kwenye series hii, mtandaoni kukawaka moto maana watu hawakupenda, kwa sababu series ni ya kikorea alafu brand ni ya kichina.

Of course hakuna kitu kilichobadilika maana Kituo Cha TVN kilisubiri mpaka Mkataba wake na kampuni hiyo uishe ndio iweze kuachana na brand hiyo.

3. DESCENDANTS OF THE SUN

Hii ni series nyingine ambapo humu ndani kampuni ya Hyundai Motors ilionesha bidhaa zake yaani magari.

Kuna scene moja ambapo Jin Goo na Kim Ji Won wapo kwenye gari la Hyundai. Hii ilikuwa ni njia ya kukuza na kutangaza magari ya hyundai. Pia series ya IRIS kuna magari mengi KIA yametumika mule.

Tamthiliya nyingine zilizotumia mtindo huu wa kutangaza bidhaa ni pamoja na KING ETERNAL MONARCH, MEMORIES OF ALHAMBRA, ITS OKAY NOT TO BE OKAY pamoja na MISAENG.

Vipi kwa Tanzania unadhani huu ni mfumo mzuri wa matangazo?

Uzi Tayari!

goblinsubway1.jpg
tumblr_pahdtqJD9z1x0e2spo1_1280.jpg
63a32a6345efe2885cf30411f244f796.jpg
WaterGod14-00702.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom