Botswana waichana live USA

Botswana waichana live USA

Botswana wananifurahisha sana.

Nimetoka kusema kwenye thread nyingine, nchi za Afrika zinatakiwa kufukuza hawa mabalozi wa Marekani na kuvunja uhusiano wa kibalozi na Marekani mpaka rais wa Marekani aombe radhi.

Aone kwamba Marekani hata kama ina nguvu vipi, nayo pia inategemea ushirikiano na nchi za ki Afrika katika vita dhidi ya ugaidi, biashara etc.

Afrika kwa sasa inaweza kirahisi sana kuamua kufanya biashara na Ulaya na China, ikaipotezea Marekani.

Tatizo kila nchi ni kibaraka wa marekani.
 
Vidonge kwa msaada wa watu wa marekani na kila kitu kwa msaada wa watu wa marekani.
 
Na huyu mwingine mnasema hayohayo!
Nenda YouTube kaangalie ile video ya wazungu walivyo mtukana trump na kumkanyulia makalio kwenye tower zake!
Alafu wamemtupa nje kwenye mkutano wa mataifa Europe na amealikwa Obama instead
Trump ni jendawazimu pasee
 
Hapa suala si mtu kukuita mbwa na wewe kupambana naye.

Suala ni, mtu akikuita mbwa halafu mwanawe anakuja kuchumbia kwako, utakubali huo uchumba?

Kuna ujumbe wa bunge la Marekani unakuja Botswana kutafuta deals. Kuna wafanyabiashara wa Marekani wako Bitswana wanafanya deals.

Trump mwenyewe kasema rafiki zake wanakuja Afrika kutafuta utajiri.

Sasa kama huko ni shithole countries, kwa nini hawaishi kuja?

Africa hata nchi inayoonekana haina kitu, ina jangwa tu kama Niger, ina uranium inayotakiwa dunia nzima kwenye nuclear weapons.

Sasa mtu mwenye akili ataziitaje hizi nchi shithole wvwn from a merely practical standpoint?
Hapo penye red ndio jibu lilipo, ni mwendawazimu, hajielewi!
Kama anatuma mwanawe kuja kuchumbia kwako maana yake yeye ndie mbwa namba moja, kazaa mbwa anayekwenda kuchumbia kwa mbwa. Ukiukataa uchumba wakati yeye anajiona ni binadamu afu ww mbwa utakuwa umeafiki kuwa ww ni mbwa kweli!
Kupambana na trump utapata presha bila sababu! Uwezo wake wa kupambanua mambo ni mfupi sana! Ni rahisi sana kwake kufikia hitimisho lenye mlengo mfinyu sana!
 
Husibishane na mpumbavu utaonekana mwenda wazimu.....Mimi siwezi kubishana na Trump
 
Hapo penye red ndio jibu lilipo, ni mwendawazimu, hajielewi!
Kama anatuma mwanawe kuja kuchumbia kwako maana yake yeye ndie mbwa namba moja, kazaa mbwa anayekwenda kuchumbia kwa mbwa. Ukiukataa uchumba wakati yeye anajiona ni binadamu afu ww mbwa utakuwa umeafiki kuwa ww ni mbwa kweli!
Kupambana na trump utapata presha bila sababu! Uwezo wake wa kupambanua mambo ni mfupi sana! Ni rahisi sana kwake kufikia hitimisho lenye mlengo mfinyu sana!
Kwa hivyo utaukubali au utaukataa uchumba?
 
This is good news. Kama ni u maskini wetu ni bora tufe nao kuliko kutukanwa na mpuuzi mmoja ambaye hajawahi kuwa hata katibu wa kijiji huko kwao
 
Hao ni Botswana, straight foward na bila longolongo wala kuuma maneno. Kazi ipo kwa Mswanglish wa Bongoland
 
U
Botswana wananifurahisha sana.

Nimetoka kusema kwenye thread nyingine, nchi za Afrika zinatakiwa kufukuza hawa mabalozi wa Marekani na kuvunja uhusiano wa kibalozi na Marekani mpaka rais wa Marekani aombe radhi.

Aone kwamba Marekani hata kama ina nguvu vipi, nayo pia inategemea ushirikiano na nchi za ki Afrika katika vita dhidi ya ugaidi, biashara etc.

Afrika kwa sasa inaweza kirahisi sana kuamua kufanya biashara na Ulaya na China, ikaipotezea Marekani.
ulaya na china wanaitegemea marekani pia
 
U

ulaya na china wanaitegemea marekani pia
Na Marekani inazitegemea Ulaya, China na Afrika.

China wameanza kukataa kununua madenibya Marekani, Wall St. wameanza ku panic.

Ulimwengu huu ni wa kutegemeana katika biashara za kimataifa, chumi zimefungamana, hakuna anayeweza kusimama peke yake.

Russia imevamia Crimea iliyopo Ukraine. Lithunia ambayo kwa kawaida ilikuwa inauza maziwa yake Russia, imeshindwa kuuza maziwa Russia kutikana na vita hii. Ikageuza kibao nabkuuza maziwa yake Marekani, ambako maziwa yalikuwepo kibao, supply ikazidi sana demand, bei ya maziwa ikashuka. Faida za wafugaji wengine wa Marekani zikashuka 90%.

Hapo unaweza kuona chumi za ulimwengu zilivyoingiliana.

Hakuna anayeweza kusimama pekee.

Moja ya sababu mtu aliyepewa dhamana ya urais anatakiwa kuongea jwa heshima kwa nchi za aina yoyote muda karibu wote.

Siku hizi watu wanatumia kila kitu kiu humi. Hata hizo shithole countries kama ni kweli kuna siku unaweza kuhutaji mavi hayo hayo yaende kutengeneza umeme wa gesi ya asili, sasa ukishawatukana unaweza kukosa maliasili ya kutengeneza umeme.
 
trump yupo sahihi, mmezoe maneno yakulembwa

trump anasea ukweli kama unahasira ni wewe na mkeo mkalie chumbani kwenu

msubiri utawala democratic watawaficha, fyuuuuuuuuu
Kwa akili yako inafikiri katukanwa nani pale? Ni mama na babaako kule kijijini mkuu
 
Ana tofaut ipi na rais wa Tanganyika
Tofauti ni kubwa sana huyu wa Tanganyika hajalelewa kwenye mazingira ya pesa (utajiri), huyu wa kwetu ni lazima awe mkali kwa sababu upole na umwinyi ndio uliotufikisha kwenye mkwamo mbaya wa kimaisha.

Huyu wa kwetu ni lazima atupeleke mbio ili tuwafikie Wakenya na Wanyarwanda kiuchumi, hakuna namna ya nchi kuwa ya kipato cha kati ifikapo 2025 kwa kuendekeza hulka za kizembe.
 
Afrika tunatatizo moyo nalo ni kujihisi wanyonge hatufai na kuwaona wazungu wako juu, kwani kila jambo likitamkwa tunaona tumebaguliwa, kwani sisi hatuwezi kutamka jambo lolote kwao. Tubadilike
 
Botswana siyo nchi ya kisportsport.

Hapo Tanzania ingekuwa ni picha za UDSM zimesambazwa ungeona matamko kutoka kila kona.

Ila hili la "shithole countries tuko kimyaaa kama vile tumekatwa mikia "

Ningekuwa mkuu wa hapo Tanzania, Lazima Ubalozi wa USA ungefungwa kwa Kweli. Na Balozi wetu wa Tanzania angerudi ndani ya 24 hours.
 
Back
Top Bottom