Botswana Nchi ya WATU 2M inalialia - zenye WATU 60M zifike wapi?

Botswana Nchi ya WATU 2M inalialia - zenye WATU 60M zifike wapi?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
2,091
Reaction score
1,918
Aliongeza kuwa Wizara ya Fedha imeidhinisha bajeti ya dharura ya dola milioni 18.7 ili kuushughulikia mzozo huo. Rais Duma Boko alisema jeshi litasimamia usambazaji wa dawa za dharura, huku shehena za kwanza zikiondoka mara moja katika mji mkuu wa Gaborone na kuyapa kipaumbele maeneo ya vijijini ambayo hayajahudumiwa.

Tangu kuanza kwa mwezi huu, Wizara ya Afya ilikuwa imeziagiza hospitali kuahirisha shughuli zisizo za lazima kwa sababu ya uhaba wa dawa. Botswana ni miongoni mwa mataifa kadhaa ya Afrika yaliyoathiriwa na hatua ya hivi karibuni ya serikali ya Marekani kupunguza misaada ya maendeleo katika sekta ya afya. Mgogoro huo pia unahusishwa na kupungua kwa bajeti ya taifa kulikosababishwa na kudorora kwa soko la almasi duniani. Botswana, yenye wakazi milioni 2.5 kusini mwa Afrika, ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa almasi duniani.

Wishing to know:-
Huduma za afya kwetu ni imara au kuna changamoto kama hizi za wenzetu???
 
Hapa zikiwa mbovu ,zikiwa nzuri hatutajua 🤣
Siasa imetamalaki hadi kwenye afya za watu
 
Mbona unaongea irrelevant. Bora hata Botswana wanapeleka madawa huku sawa hakuna kabisa.
 
Back
Top Bottom