Zuia Sayayi
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 841
- 133
Boti tatu zenye silaha zinazoaminika kuwa za Jeshi la Iran zimejaribu leo kuikamata meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la Ghuba bila mafanikio
Shirika la Utangazaji la CNN limeripoti likiwanukuu maafisa wawili wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya Uingereza ilikuwa ikiingia katika mlango bahari wa Hormuz wakati boti tatu zilipoikaribia na kuiamuru kusimama katika mipaka ya Bahari ya Iran
Hata hivyo, meli ya kivita ya Uingereza iliyokuwa ikiisindikiza meli hiyo ya mafuta ilitishia kuzishambulia boti za Iran na kuziamuru kuondoka
Hata hivyo, Jeshi la Iran lilikana kuwa limeizuia meli ya mafuta ya Uingereza likisema hakukuwa na makabiliano katika muda wa masaa 24 na meli yoyote ya kigeni, ikiwa ni pamoja na meli za Uingereza
Kisa hicho kinajiri siku chache tangu Uingereza ilipoikamata meli ya mafuta ya Iran katika eneo la Gibraltar kwa madai ya kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria
Tukio hilo lilizusha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya Iran na Uingereza na Iran ilitishia kuwa itakamata meli ya mafuta ya Uingereza kama hatua ya kulipa kisasi.