Boti za Iran zakwama kuikamata meli ya mafuta ya Uingereza. Iran yapinga vikali taarifa hizo

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
841
133
Boti tatu zenye silaha zinazoaminika kuwa za Jeshi la Iran zimejaribu leo kuikamata meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la Ghuba bila mafanikio

Shirika la Utangazaji la CNN limeripoti likiwanukuu maafisa wawili wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya Uingereza ilikuwa ikiingia katika mlango bahari wa Hormuz wakati boti tatu zilipoikaribia na kuiamuru kusimama katika mipaka ya Bahari ya Iran

Hata hivyo, meli ya kivita ya Uingereza iliyokuwa ikiisindikiza meli hiyo ya mafuta ilitishia kuzishambulia boti za Iran na kuziamuru kuondoka

Hata hivyo, Jeshi la Iran lilikana kuwa limeizuia meli ya mafuta ya Uingereza likisema hakukuwa na makabiliano katika muda wa masaa 24 na meli yoyote ya kigeni, ikiwa ni pamoja na meli za Uingereza

Kisa hicho kinajiri siku chache tangu Uingereza ilipoikamata meli ya mafuta ya Iran katika eneo la Gibraltar kwa madai ya kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria

Tukio hilo lilizusha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya Iran na Uingereza na Iran ilitishia kuwa itakamata meli ya mafuta ya Uingereza kama hatua ya kulipa kisasi.

1151225
 
Boti tano zenye silaha zinazoaminika kuwa za Jeshi la Iran zimejaribu leo kuikamata meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la Ghuba bila mafanikio, Shirika la Utangazaji la CNN limeripoti likiwanukuu maafisa wawili wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya Uingereza ilikuwa ikiingia katika mlango bahari wa Hormuz wakati boti tano zilipoikaribia na kuiamuru kusimama katika mipaka ya Bahari ya Iran, Hata hivyo, meli ya kivita ya Uingereza iliyokuwa ikiisindikiza meli hiyo ya mafuta ilitishia kuzishambulia boti za Iran na kuziamuru kuondoka, Kisa hicho kinajiri siku chache tangu Uingereza ilipoikamata meli ya mafuta ya Iran katika eneo la Gibraltar kwa madai ya kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria, Tukio hilo lilizusha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya Iran na Uingereza na Iran ilitishia kuwa itakamata meli ya mafuta ya Uingereza kama hatua ya kulipa kisasi.

View attachment 1151225

chanzo:Mwananchi:D
mbona boti zipo zaidi ya tano?
 
Aah hao sindio wasambazaji propaganda za mabeberu...walituaminisha mambo mengi sana ya uongo kumu husu Gaddafi ''Ili tu ma bwana zao wapate kumtoa madarakani. ..So unadhani wataongea ukweli upi kuhusu iran. ..wakati unajua fika kuwa ni iran ni adui wa mabwana zao
Leta za ukweli kutoka upande wa pili
 
Iran wamechemsha alafu wamedai kuwa Uingereza ni Wazushi na kuwa Boti za Iran zilikuwa kwenye Doria zake kama kawaida yao na wala hawakuisimamisha Meli ya UK... Sasa kama zilikuwa Doria why zilijaribu kuisimamisha hiyo meli na huku ikitoa tamko kuwa Marekani na Uingereza zitakuja kujutia kitendo cha kutekwa meli ya Iran... Nadhani wanamchezea Uingereza ambae hawajui kuwa ni Sleeping Giant... United Kingdom mambo ya utawala wa Dunia alishaachaga na sio kwamba hawezi tena Ile Damu ya Kifalme bado ipo watambue Iran anaona kuachwa achwa basi bichwa hilo..
 
Huyo iran analo analolitafuta na atalipata tu....ni swala la muda tu
Iran wamechemsha alafu wamedai kuwa Uingereza ni Wazushi na kuwa Boti za Iran zilikuwa kwenye Doria zake kama kawaida yao na wala hawakuisimamisha Meli ya UK... Sasa kama zilikuwa Doria why zilijaribu kuisimamisha hiyo meli na huku ikitoa tamko kuwa Marekani na Uingereza zitakuja kujutia kitendo cha kutekwa meli ya Iran... Nadhani wanamchezea Uingereza ambae hawajui kuwa ni Sleeping Giant... United Kingdom mambo ya utawala wa Dunia alishaachaga na sio kwamba hawezi tena Ile Damu ya Kifalme bado ipo watambue Iran anaona kuachwa achwa basi bichwa hilo..
 
tehteh.........
Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yameripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz - kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom