JPM anatawala kwa vitisho, alishamtisha huyo gavana mpya kuwa angeweza kumfukuza kazi kama mtangulizi wake kama asingefuatai amri zake!! Huyu bwana haelewi kuwa BOT ina independence yake kufuatana na sheria iliyoiunda ili kutimiza wajibu wake; haitakiwi kuingiliwa na wanasiasa katika utendaji wake. kuingingilia utendaji wa BOT na wanasiasa ni kutaka kujijengea mazingira kama ya EPA ya kutaka kuja kuchota fedha pindi uchaguzi utakapowadia. Nina kila sababu ya kuamini kuwa karibu na uchaguzi kutakuja kuwa na wizi mkubwa sana hapo BOT na ndio maana hivi sasa kuna mabadiliko mengi yanafanywa ili kufanikisha zoezi hilo muda ukifika.