BoT: Watu watumie huduma za mitandao, benki zikae na waliokopeshwa, riba zifikiliwe kutokana na Corona

Huwa nikiona neno "KUSHUSHA RIBA NA HATI FUNGANI" Hapo najua hali ni tete. Au wachumi uchwara mnasemaje hapo?

Hapo lazima tuelewane tu hakuna sababu ya kuniambia mna akiba ya fedha za kutosha wakati mimi mwananchi sina kitu na nmekaa kimya.

Na nyie kaeni kimya tu uhalisia utaonekana tu kadri siku zinavyokwenda. Sio kuleta machapisho ya kisenge hapa wakati sjapata hata chakula cha mchana hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwa Benk kuu ya Tanzania (BOT) imeshusha riba kwa asilimia saba(7%).
kwenye mabenki ya biashara nini reflection kwa watumiaji ambao ni wakopaji.
 
Level seat, tena siti ya mbele hapa nasubiri kupata elimu.

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
1. Riba zinapaswa kushuka sana!! BoT wamepunguza Reserve Ratio; hivyo benki zimeongezewa mtaji kiaina.

2. Pia zimepunguziwa riba, ikiwa kama zitakopa kwa riba ya 5%, sitarajii ziwatoze wateja zaidi ya 10%; hasa kama Valuer wapo makini.

3/ Biashara ya kukopesha ni kama biashara nyingine: hutegemea DEMAND AND SUPPLY.
Swali: Je demand ya mitaji ipo miongoni mwa wawekezaji? Yaani, kuna nwejezaji yupo tayari kwenda kuomba 200m kipindi hiki?

4/ Note: Ukiona bidhaa yoyote imeshuka bei jua haina walaji.
 
Kamati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Benki Kuu ya Tanzania imepitisha hatua mbalimbali za kisera zinazolenga kukabiliana na athari za mlipuko wa #COVID19 katika Uchumi ili kudumisha uthabiti wa Sera ya fedha.

1. Kampuni zinazotoa huduma ya fedha kwa njia ya mtandao kuongeza kiwango cha miamala kwa siku kwa mteja kutoka Tsh. Milioni 3 hadi Tsh. Milioni 5 na kiwango cha akiba kwa siku cha mteja kutoka Tsh. Milioni 5 hadi Tsh. Milioni 10.

2. Kuongeza unafuu kwenye dhamana na hati fungani za Serikali zinanazotumika na benki kama dhamana wakati wa kukopa Benki Kuu. Kiwango cha dhamana kimepunguzwa kutoka 10% hadi 5% kwa dhamana za muda mfupi na pia kutoka 40% hadi 20% kwa hati fungani.

3. Benki Kuu itatoa unafuu kwa benki na taasisi za fedha zitakazotoa unafuu katika kurejeshwaji wa mikopo kwa namna zinavyoona inafaa na kujadiliana na Wakopaji kwa kuzingatia uwazi bila upendeleo.

4. Imeshusha kiwango cha chini cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania, kutoka asilimia 7 hadi asilimia 6. Pia, imeshusha kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki kukopa kutoka 7% hadi 5%.

Aidha, Benki Kuu inaufahamisha Umma kuwa nchi yetu ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kuwezesha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi na Wananchi wanahimizwa kufanya miamala kwa kutumia Shilingi badala ya fedha za kigeni.

bot-1.jpeg
bot-2.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miluzi bado mingi sana
Huyu anasema hiki yule anasema kile!

Swali watu wanataka kufahamu corono ipo na kama ipo iko kwa kiwango gani, haya mambo ya kunyamaza.

Inafanya Wananchi wachukulie poa na wanaishi kama kawaida

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilitakiwa wapunguze makato ya kwenye m-pesa,airtelmoney nk. kwa zaidi ya 85% ili kiwashawishi watu watumie hizi huduma
 
Kwa wafanyakazi huu ni wakati muafaka waruhusiwe kuikopea ile 1/3 ya mshahara maana huko mbele ni giza.

Lakini pia, serikali inapaswa kuanzisha survival and recovery allowance hasa kwa walimu mbali na mshahara.

Hili itasaidia sana hasa pindi shule zinapofunguliwa baada ya janga kupungua walimu watakuwa wako stable kurudi kazini ili kuwapatia wanafunzi Elimu na kukuza uchumi
Asante
 
Kumbe BOT ndio mnasababisha tufirisiwe na mabenki...kwanini mlikuwa mnawatoza riba kubwa na wao wanaileta kwetu? Aaah kumbe
 
Kamati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Benki Kuu ya Tanzania iliyokutana tarehe 8 Mei 2020 imepitisha hatua mbalimbali za kisera zinazolenga kukabiliana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa ya virusi vya Corona (COVID-19) katika uchumi. Lengo la hatua hizi ni kudumisha uthabiti wa sekta ya fedha na upatikanaji wa huduma za fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Hatua za kisera zilizopitishwa ni:

1. Benki Kuu kushusha kiwango cha chini cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania, kutoka asilimia 7 hadi asilimia 6, kuanzia tarehe 8 Juni 2020. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ukwasi katika sekta ya benki.

2. Benki Kuu kushusha kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki kukopa Benki Kuu kutoka asilimia 7 hadi asilimia 5, kuanzia tarehe 12 Mei 2020. Hatua hii itawezesha kuongeza wigo wa benki kukopa kutoka Benki Kuu kwa riba nafuu, na hivyo kupunguza riba ya mikopo kwa wateja.

3. Benki Kuu kuongeza unafuu kwenye dhamana na hati fungani za serikali zinazotumika na benki kama dhamana wakati wa kukopa kutoka Benki Kuu. Unafuu huo unapatikana kwa kupunguza kiwango cha dhamana kutoka asilimia 10 hadi asilimia 5 kwa dhamana za muda mfupi, na kutoka asilirnia 40 hadi 20 kwa hati fungani, kuanzia tarehe 12 Mei 2020. Hatua hii itaongeza uwezo wa benki kukopa kutoka Benki Kuu kwa unafuu zaidi kultko ilivyokuwa awali.

4. Mabenki na taasisi za fedha kutathmini kwa kina athari zinazotokana na mlipuko wa COVID-19 kwenye urejeshaji wa mikopo, kujadiliana na wakopaji namna ya kurejesha mikopo, na kutoa unafuu wa urejeshaji wa mikopo itakavyoonekana inafaa. Benki Kuu itatoa unafuu kwa mabenki na taasisi za fedha zitakazotoa unafuu katika urejeshwaji wa mikopo hiyo kwa kuzingatia uwazi na bila upendeleo

5. Makampuni yanayotoa huduma za fedha kwa njia ya mtandao kuongeza kiwango cha miamala kwa siku kwa mteja kutoka Shilingi 3,000,000 hadi shilingi 5,000,000, ma kiwango cha akiba kwa siku kwa mteja kutoka shilingi 5,000,000 hadi shilingi 10,000,000. hatua hii inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha za kidigitali katika kufanya miamala mbalimbali, na hivyo kupunguza ulazima wa wateja kwenda katika Mabenki. Aldlia, Mabenki yamehimizwa kuongeza matumizi ya mifumo ya kufanya miamala kwa njia ya kidigitali, ikiwemo matumizi ya mashine za kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki.

6. Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kufanya tathimini ya athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa ya virusi vya Corona katika sekta mbalimbali za uchumi na kuchukua hatua stahiki ili kupunguza madhara ya athari hizo.

Aidha, Benki Kuu inapenda kuufahamisha urnma kwamba nchi yetu ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kuwezesha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi. Vilevile, wananchi wanahimizwa kuendelea kufanya miamala mbalimbali nchini kwa kutumia Shilingi badala ya fedha za kigeni.

Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kuwashauri wananchi kuchukua hatua na taadhari ili kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa homa ya virusi vya Corona nchini.

Prof. Florens D."A. M. Luoga
Gavana, BENKI KUU YA TANZANIA
12 Mei 2020
 
Makato ya shuke chini!!!!, inakera sana kugawana hela na mtandao Mimi kwa Sasa hela nazungusha manual kwa maeneo ya karibu sivumili ujinga

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Kabisa, walipaswa kutoa MAELEKEZO/MAAGIZO siyo kushauri. Upuuzi mtupu.

Yale yale ya kushauri wenye nyumba na vyumba vya kupangisha wasidai kodi wakati serikali hiyo hiyo inadai kodi kwa nguvu toka kwa wapangaji hao hao; na kana kwamba kuna ahueni ya kodi popote walipoitoa wao.
 
Wakuu naomba mnieleweshe:
Kutokana na kishuka huku kwa riba kutoka 7% mpaka 5% je taasisi za kifedha zibazotoa mikopo nazo zitashusha riba kwa mikopo wanayotoa au ndio watabakia walipo kwa ajili ya kulinda faida zao?

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
BoT ni kibogoyo haina meno.

According to the BOT act ,they are given a modicum of independence!! Inategemea pia confidence aliyonayo GAVANA wa BOT at any point in time na pia jinsi mkuu wa nchi anavyoheshimu sheria zilizotungiwa hiyo taasisi!!
 
Back
Top Bottom