BOT pigeni marufuku kufukizia Udi noti

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,131
3,912
Leo jamaa kanilipa hela yangu aliokaa nayo muda mrefu lakini vibunda vya pesa vinanuka Udi kama duka la baniani.

Harufu siipendi lakini pesa naipenda.Sijui alinuia nini?

Benkuu(BOT) wapige marufuku harufu za ajabu kama hizi.
 
Duuh...

Basi watapiga marufuku hata Perfume,so inamaana hata kuzishika,au kuwa nazo.
 
Halafu hiyo sheria wataisimamiaje? Kwamba tunuse noti kila tunapopewa halafu tukaripoti BOT?

Vitu vingine tuwe tunakaa kimya. Mara ngapi umepewa noti zimefukiziwa ubani hadi iwe issue ya BOT kupiga marufuku?
 
Kuna jamaa angu ni dereva alikua anafanya kazi kampuni fulani ya wahindi kurasini alikua anadai wakipewa mshahara, wakati huo bado walikuwa wanapewa cash mkononi sio bank,zile noti zilikua na harufu ya udi.
 
Unakuta hiyo pesa inakupa maamuzi ya ajabu.Unashangaa umeenda karume kununua misuruali mibwanga.Mara umepoteza.

Bora hizo zinukazo UDI,nyingine harufu yake ni kana zimetolewa mali..... Toni.
Naishukuru serikali kuitengeneza pesa kubwa kwa Rangi nyekundu imesaidia sana.
 
Back
Top Bottom