BoT na CMSA wautahadharisha umma kuhusu Taasisi ya Upatu ya D9 Club

Noted
Taarifa zilizopo ni kuwa *withdraw ya dollar kwenda Bitcoin kwa sasa imesimama*
Confirm about that issue please
Hello habari,withdraw haijasimama ila kinachofanyika ni utengenezaji was platform ya D9 ambayo itawezesha utoaji wa pesa kwa haraka zaidi,maana Mara ya kwanza ilikua ikitumika block chain ila ilionekana kuzidiwa maana member niwengi mno wanao request kutoa via bitcoin na hii ilikua ikichukua many days up to 9 days to receive your payment requested.so there in final step to complete the new platform
 
Ivi wale walio fungiwa na wizara ya fedha ni akina nani?? Sio hawa kweli??
Umetazama hio video aliekuwepo huyo advocate?
Itazame kwanza ndio utaweza elewa.

Pia sio wizara ya fedha Bali ni financial instutions ndio zilizokua zikipiga kelele,maana pesa nyingi zilikua zinapelkwa njee ya nchii
 
Hii kitu ina miaka na miaka na sijawahi kusikia kwamba mtu analalamika ameibiwa. Kwa hyo ni vema wange eleza ni watu gani waliowekeza huko walio lalamika kuibiwa . vinginevyo ni chuki tu za kutaka wachache ndio watajirike and the rest wabaki . Uzuri wake hii kitu inachezwa mtandaoni sijui kama wataweza. Miezi mitatu ela yako imerudi sasa hapo mtu anatapeliwaje. Mfano mm mwenyewe huu mwezi wa sita , nimerudisha ela yangu miezi mitatu ya mwanzo na sasa nimeshakula faida ya 2m miezi miwili na bado saba. Hapo wakisitisha huduma zao utasrmaje nimeibiwa
Kwa hiyo unaona raha wewe kupokea pesa za wenzako hao wa chini yako alafu ikisitishwa wenzako ndio wanaumia... wewe huoni unakula fedha ya dhuluma?
 
Wanajamvi kunawatu wanalia pesa zao wiki mbili zimekwisha bila malipo sababu hazijawekwa bayana jadi sasa na Uzi huu kila ninapoweka unafutwa tuwe makini na d9

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Deci , iliwapiga watu nikajua watanzania wamejifunza sasa inakuwaje, bado mnapigwa!?

Poleni sana.
 
Kama ambavyo nimeandika hapo, tetesi ni kwamba D9 clube imefungwa, na account zote online zimefutwa!Kama ilivyokuwa kwa DESI wale wa mwanzo wamepata faida kubwa na walioingia chini ya miezi 4 iliyopita sasa hivi ni maumivu!
Kinachotokea ni kwamba ndani kwa ndani wanajitahidi kufarijiana kwamba account zitafunguliwa tena baada ya miezi kadhaa na malipo yatakuwa makubwa zaidi! Na tahadhari imetolewa "wasisemeseme nje ya group lao" kwani wana haribu taswira. Najiuliza kama maumivu yana Taswira.
Watanzania hatukomi tu??
 
Back
Top Bottom