kemi2011
JF-Expert Member
- Dec 25, 2013
- 735
- 290
Nsbu kakwambua DKila baada ya muda fulani DECI inakuja kwa jina tofauti na bado kuna watu wanaingia mkenge
Nsbu kakwambua DKila baada ya muda fulani DECI inakuja kwa jina tofauti na bado kuna watu wanaingia mkenge
Inaonekana unaumia sana watu wanapopiga hela.....Nmefurahi sana maana nlidhan mmetusahau watanzania maana weng wanaibiwa kuna dada kashatoa million 4.kambiwa kila week ataingiziwa laki 4 lakin zitakatwa riba ila mpaka sasa hakaingiziwa hata sh. 500 ya silver hii ni hatari.....
Pia BOT muwe mnawah kutoa taarifa coz D9 ipo muda kdg toka ianze kutangazwa so n vyema mnapoona mambo haya haraka sana mnataarifu wananchi maana weng wanataamaaa na pesa za haraka haraka na hawajui hzo pesa znazalishwa vp had mtu akupe ww milllion 16 kwa kuwa umetoa million 4??? Okay jamn sambazan hiyo barua nanyi tuwaokoe ndugu zetu wanaoliwa
Ilikuwa DECI, sasa ni D9 sasa itakuja Dig MoneyNsbu kakwambua D
Muda Umefikia sasa wa kusikia walioibiwa kwa vile new members wanaenda kutoweka, malipo yalikua yanatoka kwa Wateja wapya ndo maana watu wanahangaika kushawishi wenzao, subiri wote wapate taarifa baada ya wiki tatu utawasiki walio tapeliwa mbaya zaidi kwa wale new members Sababu watakua hawawezi kurudisha pesa yaoHii kitu ina miaka na miaka na sijawahi kusikia kwamba mtu analalamika ameibiwa. Kwa hyo ni vema wange eleza ni watu gani waliowekeza huko walio lalamika kuibiwa . vinginevyo ni chuki tu za kutaka wachache ndio watajirike and the rest wabaki . Uzuri wake hii kitu inachezwa mtandaoni sijui kama wataweza. Miezi mitatu ela yako imerudi sasa hapo mtu anatapeliwaje. Mfano mm mwenyewe huu mwezi wa sita , nimerudisha ela yangu miezi mitatu ya mwanzo na sasa nimeshakula faida ya 2m miezi miwili na bado saba. Hapo wakisitisha huduma zao utasrmaje nimeibiwa
Bit coin ni mfumo wa malipo wa kielectronic ambao mtu anaweza kutumia kuafanya malipo, huwa ni vigumu kutrace malipo na pia hakuna sheria Kama za mabenki hiyo biashara haramu kwenye mitandao zimekua zikiupenda zaidi, hata kile kirusi cha juzikati (ransomware) kilihitaji malipo yafanyike Katika mfumo wa bitcoin, mfumo wenyewe hauna shida watumiaji kama d9 ndo wanashida Kama vile bastola inaweza kutumiwa kiusalama na kwa uhalifu inategemea na mtumiajiKuna bit coin pia mkuu....hebu nayo imulikwe
benki inaonaje wivu?Wana wivu sana BOT
Mamlaka imetoa tahadhari kwa umma kwamba, taasisi ijulikanayo kama D9 Club inayotangaza au kushawishi, pamoja na mambo mengine ununuzi wa hisa, inafanya hivyo bila vibali vya mamlaka husika. Kumekuwepo na Michango tofauti kupitia JamiiForums kuhusiana na Taasisi=>D9 Club, upatu unaosambaa kwa kasi Tanzania kama moto wa kifuu. Tuwe makini.
View attachment 523909
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) zinapenda kuutahadharisha umma kwamba, taasisi ijulikanayo kama D9 Club inayotangaza au kushawishi, pamoja na mambo mengine ununuzi wa hisa, inafanya hivyo bila vibali vya mamlaka husika.
Ni imani ya BoT na CMSA kuwa ushawishi unaofanywa na D9 Club kwa umma kushiriki katika mpango wao utasababisha watu kupoteza fedha zao, na pia ni kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania ambayo katika Fungu la 171A,171B na 171C, ni kosa la jinai kuendesha, kushawishi watu kushiriki, na kushiriki au kuchangia fedha katika upatu.
Ifahamike kwamba upatu haramu hubuniwa kwa namna ambayo fedha za kila mshiriki mpya hutumika kumlipa mshiriki aliyetangulia, na hakuna maelezo ya namna yoyote ya kuwekeza au kuzalisha fedha hizo.
Kwa taarifa hii, umma unasisitizwa kutoshawishika kwa namna yoyote ile kushiriki katika upatu uliobuniwa na D9 Club na mipango mingine ya aina hiyo. Aidha, wananchi watoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana na vyombo vya usalama (Polisi) kuhusiana na mikutano au mafunzo yanayoendeshwa na D9 Club na mipango mingine haramu kama inayofanana na huo.
Imetolewa na:
BENKI KUU YA TANZANIA & MAMLAKA YA MASOKO YA
MITAJI NA DHAMANA
14 Juni 2017
Kwa maelezo zaidi wasiliana na: kanyoni@bot.go.tz & info@cmsa.go.tz
Mmiliki halali anaitwa Danilo Santana na tarehe 7 July anaingia Dar. atakuwa pale Mlimani City na atapewa escort ya king'ora kutoka serikalini. Akishaondoka ndo mtajadili juu ya utapeli. Uganda kuna registered office ambayo ina operate kwa ajili ya Tanzania, Kenya na Uganda. ofisi nyingine iko Nigeria. Usipofanya wewe haizuii wengine kufanya. Hata hapa Dar ipo ofisi ndogo inayosimamiwa na ofisi ya Uganda na ndio inayoandaa mapokezi ya CEO wa D9. Wala hajifichi na biashara sio upatu. Ukiingia leo unapewa contract ya mwaka mmoja kwa hela yako. Kuingiza watu ni kutaka kuongeza kipato tu ila kama una shughuli zako nyingine unaendelea tu.Mimi huwa sifanyi biashara za Mitandaoni! kwa sababu mara nyingi ni vigumu kufahamu mumiliki halali ni nani, anapatikana wapi na pia kuna kiwango kidogo cha usalama!
Malipo yapo kama kawaida mkuu. Ni biashara ya mtandaoni na inatoka kimtandao. Kwa wenzetu nje unatoa bank through bitcoins ila huku kwa vile tumezoea ujamaa na kujitegemea huku migodi ikiuzwa ndo mnalishwa umbea eti ni upatu. Hii ni biashara. Kama hujui ni bora ukajifunza kulikokusema watu wanaibiwa wakati watu tunakula hela kihalali.Muda Umefikia sasa wa kusikia walioibiwa kwa vile new members wanaenda kutoweka, malipo yalikua yanatoka kwa Wateja wapya ndo maana watu wanahangaika kushawishi wenzao, subiri wote wapate taarifa baada ya wiki tatu utawasiki walio tapeliwa mbaya zaidi kwa wale new members Sababu watakua hawawezi kurudisha pesa yao
Unabahat mbayaAiseee kuna watu wameweka hela zao huko na mie ilikuwa kidogo niweke hela huko
Mkuu nasikia bado watu wanakula hela bado japo sio member mimiWadau tuambieni mmefikia wapi na upatu wa hawa jamaa bado mnavuta madolari?