BoT: Mnaoshikilia Dola mziweke sokoni kwenye mfumo rasmi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa tahadhari kwa wale wote wanaoishikilia dola ya Marekani kuwa wapo hatarini kupata hasara kutokana na uamuzi huo wa kuficha pesa hizo wakitegemea kupata faida katika soko la fedha.

Akizungumza katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Gavana wa Benki Kuu Emmanuel Tutuba, amesema Tanzania inatekeleza mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa dola hivyo kuendelea kushikilia pesa hizo kuna athari ya kupata hasara badala ya faida.

"Niwaombe wanaoshikilia dola mziweke sokoni katika mfumo ulio rasmi, tutawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kujihusisha na biashara haramu ya soko la fedha (black market)," amesema Tutuba
 
Nchi za kiafrika za ovyo sana. Badala yafungue fursa ya vijana wapige hela hata waruhusu paypal.

Yanawawaza vitisho tu kila kukicha. Kama wananchi wana USD wenyewe hawana basi wajitafakari na hawana faida yoyote.

Ndiyo shida ya kuwaweka wazee ambao hata kubadili password kwenye simu hawezi mpka abadilishiwe na mtu.

Nchi yenyewe haiuzi bidhaa yoyote ipo ipo tu sasa hizo USD zitatoka wapi?
 
Hii ndio suluhisho.
Au labda ni kweli hawana hizo Dola $.

Wakiongeza supply, ikaanza kuimarika, wenyewe waliohodhi wanazitoa.

Kama wanawaza kuwasaka waliohodhi, basi akiba yao ni ndogo sana, itakuwa kweli
Nashangaa wao ndio wanalia
Kwani hawawezi hata kukopa nje? Mbona kila leo Waziri anakopa tu au hizo sio hela ni maandishi tu?
Sielewi kabisa wanamlenga nani
Au bandari haina mzunguko
 
Kuelewa wachumi wa Tanzania ni kazi sana.

Labda wanazokopeshwa hazijaingia ktk mzunguko!
Au wanalipa nje tena ..
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa tahadhari kwa wale wote wanaoishikilia dola ya Marekani kuwa wapo hatarini kupata hasara kutokana na uamuzi huo wa kuficha pesa hizo wakitegemea kupata faida katika soko la fedha.

Akizungumza katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Gavana wa Benki Kuu Emmanuel Tutuba, amesema Tanzania inatekeleza mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa dola hivyo kuendelea kushikilia pesa hizo kuna athari ya kupata hasara badala ya faida.

"Niwaombe wanaoshikilia dola mziweke sokoni katika mfumo ulio rasmi, tutawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kujihusisha na biashara haramu ya soko la fedha (black market)," amesema Tutuba
Wanaoshikilia dola ndio wenye sauti nchini kwa sasa mpka BOT mpige magoti kwao
 
Ni upuuzi BoT kuendelea kuhifadhi na kuabudu Dola huku sarafu yake ikizidi kudidimia.
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa tahadhari kwa wale wote wanaoishikilia dola ya Marekani kuwa wapo hatarini kupata hasara kutokana na uamuzi huo wa kuficha pesa hizo wakitegemea kupata faida katika soko la fedha.

Akizungumza katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Gavana wa Benki Kuu Emmanuel Tutuba, amesema Tanzania inatekeleza mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa dola hivyo kuendelea kushikilia pesa hizo kuna athari ya kupata hasara badala ya faida.

"Niwaombe wanaoshikilia dola mziweke sokoni katika mfumo ulio rasmi, tutawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kujihusisha na biashara haramu ya soko la fedha (black market)," amesema Tutuba
Nchi kama USA sijawahi ona gavana wa benki ikipiga mkwara wawekezaji. Huwa anaitisha press anatoa speech iliyojaa facts za kiuchumi mpaka wawekezaji wanaona hapa hali si nzuri wanajikuta wamechukua hatua bila kupenda.

Sasa huyu mmatumbi anapiga wawekezaji mikwara? Au kawa BoT imekua kituo cha polisi?
 
Nchi za kiafrika za ovyo sana. Badala yafungue fursa ya vijana wapige hela hata waruhusu paypal.

Yanawawaza vitisho tu kila kukicha. Kama wananchi wana USD wenyewe hawana basi wajitafakari na hawana faida yoyote.

Ndiyo shida ya kuwaweka wazee ambao hata kubadili password hawezi mpka abadilishiwe na mtu.

Nchi yenyewe haiuzi bidhaa yoyote ipo ipo tu sasa hizo USD zitatoka wapi?
Huyu jamaa utakuta ni kada wa ccm.
 
Hivi bureau huwa zinahifadhi dola? Au umeamua kuandika ili mradi?
Mda mwingine zinatumika kutakatisha fedha, kabla ya magufuli ndio kitu walikuwa wanafanya mtu kapiga michongo yake siyo halali, anaenda kuzibadilisha into usd wanahifadhi, nao wanaofanya hizo biashara hawapeleki taarifa nani kabadilisha nini kwa kiasi gani kukwepa kodi n.k unaweza ukapata picha hapo
 
Huyu jamaa utakuta ni kada wa ccm.
Mna dhahabu, gesi, maziwa, Almasi, Tanzanite, makaa ya mawe n.k bado mnalia dola hakuna, watu waweke hela kwenye mzunguko.
Upewe nini?
Serikali ingekuwa inachimba dhahabu yenyewe, almasi, dhahabu, gesi na Tanzanite na kuuza hiyo USD ingepatikana rahisi sana.
Unauza kwa USD mali yako, sasa umebinafsisha vyote. Unategemea USD zitapatikana kweli?
Nchi za kiafrika zina mali sana ila ni masikini sana mpk huruma
 
Ni upuuzi BoT kuendelea kuhifadhi na kuabudu Dola huku sarafu yake ikizidi kudidimia.
USD ni mali.
Marekani kawakopesha nchi mahela mengi sana na unatakiwa urudishe kwa mfumo wa dola.
Unatakiwa urudishe mkopo kwa mfumo wa USD na hauna, unategemea nini kinatokea hapo?
 
Hivi bureau huwa zinahifadhi dola? Au umeamua kuandika ili mradi?
Vipi kuhusu black market?
Wanaoshikilia hizo noti, wanazishikilia kwa njia labda? Ili iweje?

Gavana anasema, kwa minajiri ya kupata faida, kivipi?

Fafanua kisha uliza tena swali hilo.
 
Kuelewa wachumi wa Tz ni kazi sana.

Labda wanazokopeshwa hazijaingia ktk mzunguko!
Au wanalipa nje tena ..
Au wao ndio wanazificha
Kuna viongozi huwa wanaficha majumbani ila sio kwetu kwa majirani wanakamatwa kila kukicha

Ila sisi sijui kila anaewafuatilia wananyamazishwa kwa gunia moja we never know
Hii ndio suluhisho.
Au labda ni kweli hawana hizo Dola $.

Wakiongeza supply, ikaanza kuimarika, wenyewe waliohodhi wanazitoa.

Kama wanawaza kuwasaka waliohodhi, basi akiba yao ni ndogo sana, itakuwa kweli
Wameamua kujibu
 
Attachments

  • Screenshot_20230822_185310_Instagram~2.png
    Screenshot_20230822_185310_Instagram~2.png
    246.7 KB · Views: 6
Back
Top Bottom