Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Dar es Salaam. Wakati Tanzania Bara ikikosa mikopo na misaada nafuu iliyotarajia kutoka kwa wahisani, Zanzibar imepokea zaidi ya mara nne ya ilichotarajia.
Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Fedha kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyotolewa mwezi huu, inaonyesha kuwa jumla ya misaada kutoka kwa wahisani ilikuwa Sh22.1bilioni wakati matarajio yalikuwa Sh5.4 bilioni.
Wakati ripoti ya BoT ikieleza hayo, ripoti ya utekelezaji wa bajeti iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kwa nusu mwaka, ilionyesha kati ya Julai hadi Novemba, 2016, Tanzania ilipokea misaada ya Sh287.5 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 28.4 ya lengo la ambalo ni Sh1.01 trilioni ndani ya kipindi hicho.
Waziri alisema washirika wa maendeleo waliahidi kuichangia bajeti ya Serikali Sh3.6 trilioni lakini katika kipindi hicho jumla ya misaada na mikopo nafuu iliyotolewa ilikuwa Sh603.9 bilioni ambazo ni sawa na asilimia 21.5 ya lengo la Sh2.8 trilioni katika kipindi hicho.
Waziri alisema Serikali ilishindwa kutimiza masharti magumu yaliyowekwa na wahisani au wakopeshaji.
Katika kipindi hicho mapato ya ndani ya Serikali ya Zanzibar yalifikia Sh250.2 sawa na asilimia 106.1 ya makadirio ya makusanyo. Ongezeko la makusanyo hayo limetokana na kuimarika kwa ukusanyaji wa kodi za uingizaji wa bidhaa (import taxes), Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na ukusanyaji wa ushuru wa bidhaa (excise duties).
Kwa mujibu wa ripiti ya BoT, katika nusu mwaka ya kwanza, urari wa biashara Zanzibar ilikuwa na ziada ya Dola 35.4 milioni za Marekani kutoka nakisi ya Dola 40.9 milioni kwa kipindi kama hicho mwaka uliopita wakati Tanzania Bara ilikuwa na nakisi ya Dola bilioni moja za Marekani ikiwa imepungua kwa asilimia 33.2 kutoka Dola 1.5 bilioni.
Wakati Zanzibar ikikusanya zaidi ya makadirio, Tanzania Bara ilibana matumizi na kuongeza fedha kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ripoti inasema katika nusu ya kwanza, mapato yaliyokusanywa na kuwekwa kwenye akaunti za Serikali zilizoko BoT yalikuwa Sh8.07 trilioni, sawa na ongezeko la asilimia 22.1 ya mwaka 2015/16 lakini ni asilimia 96.0 ya makadirio ya kipindi hicho.
Mkakati wa Serikali wa kubana matumizi umefanikiwa kuokoa asilimia 2.3 baada ya kuelekeza Sh6.45 trilioni kwenye matumizi ya kawaida ikilinganishwa na mwaka 2015/16.
Matumizi ya maendeleo yalikuwa Sh2.08 trilioni ambayo ni ongezeko la asilimia 14.7 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliotangulia.
Licha ya kuongeza uwekezaji, Serikali imepunguza deni la nje kwa asilimia 1.1 kutoka Dola 17.18 bilioni za Marekani, Juni 2016 mpaka Dola 16.99 bilioni lililokuwapo Desemba. Lakini, deni la ndani liliongezeka kwa asilimia 4.5 na kufika Sh10.47 trilioni kutoka Juni mpaka Desemba 2016.
Ongezeko la deni la ndani lilitokana na kuuza dhamana na hati fungani ili kugharamia bajeti ya Serikali.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana alisema licha ya umuhimu wa mchango wa wahisani, nchi za Kiafrika zinapaswa kujitegemea katika utekelezaji wa bajeti zao.
“Ufanisi wa Zanzibar katika kupokea misaada unaonyesha wahisani hawakuwa na masharti kama ilivyokuwa bara. Pamoja na kilichotokea, tumeona Serikali ikitekeleza miradi mingi bila kuwategemea wahisani,” alisema.
Aliitaja miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, hosteli ya wanafunzi UDSM, nyumba za askari Magereza Ukonga na Serikali kuhamia Dodoma na kusema, “Haya yote yasingewezekana kwa kuwategemea wahisani.”
Chanzo: Mwananchi