BOT achaneni na noti ya 10,000/-

Ugumu wa kapatikana chenji inashiria nini?

Ova
 
Ugumu wa kapatikana chenji inashiria nini?

Ova
huwezi ukaingia mahala na hiyo dola mia yao, ukaagiza kitu cha dola 1 halafu usilete shida ya chenji

tatizo letu wabongo tuna inferiority complex

kila tatizo tulonalo tunaona ni kisa ujinga wetu

kumbe matatizo hata ulaya yapo, hata wao wanatafuta chenji kama sisi, ni jambo la kibiashara hilo
 
wakipunguza sifuri moja kwa kila noti itakuwa kama ifuatavyo:-
10,000=1000
5,000=500
2,000=200
Tatizo itabidi tutembee na magunia ya hela na noti kiukweli zitachakaa mno.Sababu hela yetu dhidi ya dola iko chini.Kwa muktadha huo noti ya elfu10 na elfu5 haiepukiki especially for big transaction.
Mi nashauri wangepunguza sifuri moja katika kila hela
 
hapa maana yake unalazimisha mfumuko wa bei lazima thamani ya shs itashuka
 
Zinaishia 100 kwa sababu zina thamani.Zetu hazina thamani.Hata euro ipo hadi 500 lakini kuwezi kuitumia kwenye manunuzi, hata kwenye ATM mwisho kutoka ni 50 euro.Ila ukiitaka noti ya 500 inabidi uende bank uombe wakupe bills za 500.
Halafu bank wakishakupa hizo noti za 500 unazipeleka wp kama hazitumiki kwenye manunuzi?
 
una pointi ya msingi na ni kitu kilichofanywa na zambia, walifanya 'currency rebasing' (haiitwi kupunguza sifuri, wanaita currency rebasing)

yani waondoe shilingi hii, kisha walete shilingi mpya ya kitanzania ambayo, kwenye kubasilishiwa ukipeleka benki sh 2000 ili upewe noti mpya basi unapewa pesa mpya ya noti ya ya 200 yenye thamani sawa na hiyo buku mbili

serikali inaweza kufanya hivyo, ila naona wanaona sio lazima maana ukipanda daladala ukalupa 500 kesho ukapewa hela mpya ukalipa 50 haumaanishi umeimprove llolote, maana ule mshahara wako wa 50,000 nao sasa utasoma 5000 hivyo ukali wa maisha uko palepale

faida pekee ni kwenye kuimport, tunakuwa na strong currency, wasomi wa uchumi wanajua zaidi
 
Hapana Mkuu mbona USD zinaishia 100.Cha msingi lazima uchumi wetu uwe Imara huwezi kufanya hicho anachotaka mleta Uzi kwa uchumi wetu huu.
UMEJIBU VEMA,uchumi wa nchi ndio kitu kikubwa hapa jirani zetu Zambia wamelifanya hili na Kwacha yao inathamani na haina 00000 za ajabu,pls my no 1 chukua shilling yetu na tuipandikize kwa Zambia kwacha,au Pula
 
Huku mtaani hakuna kitu kinasumbua kama chenji.
Watu hawauzi kisa kakosa chenji au auzunguke wee.
5000 na 10000 ni shida,
Mbadala wa efu kumi mprinti 2000 na noti mpya ya 3000 ziwe nyingi za kutosha bila kusahau 500 na 1000.
Chenji ni tatizoo.
Siku hizi noti zote ni shida kupata chenji kutokana na uhaba wa maghwala. Njia pekee ni kuwa na maghwala mengi kutokana na hayo kuwa kwenye biashara zaidi.
 
Halafu bank wakishakupa hizo noti za 500 unazipeleka wp kama hazitumiki kwenye manunuzi?
Hizi zinasaidia ubebaji hasa kwa mtu anayesafiri .Badala ya kubeba noti za 50 50 unachukua hizi.Na kwenye bureau de change unapata change nzuri ukiwa na hizi kuliko noti za 50 au 20.kwa hiyo zinachukuliwa na ma bank au bureau de change lakini kununulia vitu mitaani hawazichukui.Ni kwa usalama na ni sheria za nchi.
 
Hapana, thamani inabaki vilevile maana muundo wa hela na matumizi hautabadilika
 
Haya mawazo ni ya mchumi wa Madabwida huko! Yaani pesa ndogo ziondolewe?
 
Ukiona mwenye elfu kumi jua ana mshahara huyo...

Wafanyaniashara wa bidhaa za kuzid elfu kumi wamepukutimlkaa
 
Kama yuko Nanjirinji si itakuwa kibarua kufunga safari mpaka Kilwa Masoko kufuata chenji?
Kama uko serious na biashara inabidi uchukue chenji benki. Wahindi na watu wengine serious huwa wanafanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…