Boss nisamehe mimi mtoto wa kike

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Maisha haya asikwambie mtu ,baadaa ya kumaliza chuo na kujiajiri na baadae mtaji kukata, akatokea boss mmoja katika jiji moja kubwa hapa Tanzania ameniajiri kwenye kampuni yake.

Nina miezi 6 tu kazini ila sasa boss ananilazimisha nikafuate mzigo Hong Kong tofauti na kazi niliyoajiriwa.

Ananiambia bila kwenda Hong Kong ataniachisha kazi na anaweza kunifanyia kitu mbaya nikiwambia mamlaka.

Ananitaka niende Hong Kong mara moja tu na nikirudi atanipa kazi special kwenye kampuni na pia atanipa kitita cha kutosha.

Naombeni ushauri, nipo kwenye mawazo mazito. Je, nikikamatwa si ndo maisha yangu yatakuwa hivyo tena? Au niache kazi
 
Kama nimekuelewa vzr shogaangu, Boss anakutuma uendee unga huyo. Option pekee salama kwako ni kuacha. Usithubutu kucheza patapotea kwenye maisha: ukikamatiwa HongKong ni risasi; ukikamatiwa Bongo ni kifungo kisicho na kikomo.
 
Pole, upo kwenye kundi la organized crime ambalo kulikwepa kwake unatakiwa uwe makini sana. Toroka acha hiyo kazi kajifuche kijijini badili na simu, na acha mazoea mazoea. Huyo anakupeleka kwenye kifo.
Asant
 
Mzigo gani? Kwani kampuni yake ni ya biashara gani? Ni mzigo halali au haramu? Haya maswali ni muhimu kupata majibu yake kabla ta kufanya maamuzi.

NB: kama ni sembe usiende. Kule wananyonga
Asant kaka
 
Kama ni madawa ya kulevya pleaseeeeeeeeeee usiende!Lazima utakamatwa.Hakuna mtu ambae ameweza kuvusha mzigo salama china.Kuna wanawake walifanyiwa operation na madokta bingwa wakawekewe heroin kwenye matiti yao lakini bado wakakamatwa.Utakamatwa kama kuku dada angu.Achana na huyo boss!Ni rahisi kuchukua bunduki na kuvamia bank hapa Tanzania na ukafanikiwa kuiba hela bila ya kukamatwa kuliko kuvusha madawa ya kulevya china.
 
Back
Top Bottom