Boss anataka kufungua biashara kupitia kitambulisho changu. Je, kuna madhara?

Mfano jamaa anataka kitambulisho chako ili afungue kiwanda. Jina likitumika maana yake wewe ndiye mmiliki.

Sasa baadae huko ikajulikana kiwanda kilicho funguliwa kwa id yako kinakwepa kodi atakaye tafutwa ni mwenye jina (wewe)

Mfano mwingine..

Jina lako likatumika kufungulia kiwanda alafu huko badae ikatokea kazi au chance inayo taka mtu asiye jiweza kiuchumi..

Wakaja kicheki kwenye mfumo ukaonekana kuna kiwanda kina jina lako mpaka hapo unakosa nafasi maana wataona tayari una miliki kiwanda.

All in all jiulize kwann anataka kutumia id yako wakati na yeye anayo?

NB: Akili za kuambiwa changanya na zako.
Shukurani kwa maoni mkuu
 
Kama ni kitambulisho cha mpiga kura na unaona ukimkatalia utaharibu mahusiano yenu, mpe then kachukue Loss report police kaa nayo.

Utatunza ajira yako na mahusiano yako na boss na

Utakuwa salama endapo kitambulisho chako kitafanyiwa uhalifu.
Nikichukua hiyo loss report nitaweza tena kukitumia hicho kitambulisho changu au ndio basi tena?
 
Mtoa mada jitazame kwenye kioo changu!

Pengine naweza nikaonekana kwa baadhi ya wadau kuwa mimi sio mshikaji au sisapoti washikaji, ila when it comes kwenye kulinda welfare/status yangu huwa sina urafiki. Natoa mifano minne:-

1. Kuna marafiki zangu na ndugu zangu wa damu kabisa nimewahi kuwanyima funguo zangu za pale ninapoishi. Siwezi na sitarajii kumpa mtu yeyote funguo yangu halafu alete demu au kimada wake ninapoishi..Hii kwangu haiwezekani hata awe nani siwezi kumpa.

2. Kuna jamaa angu alimleta rafiki yake ambae simjui eti nimpe namba yangu ya NIDA ili asajilie line yake..Nilikataa.

3. Siku ya Idd (ijumaa) nilikuwa nimelala home, ghafla kuna brother mmoja tunaheshimiana sana akanipigia simu kuwa yupo airport anataka asafiri na anasubiri ku check-in hivyo anaomba niende kwa mke wake nikamchukulie ID yake then nimuwahishie airport. Yes, nilifanya kama alivyotaka then nlipofika kituoni kwa bodaboda nikamkuta j
Shukurani kwa maoni mkuu,
 
Kuna dogo alikubalo

Bosi wake atumie kitambulisho chake kupata TIN baada ya muda mrefu kupita wakaja zinguana biashara ikafa na kufungwa ilikua Dar, dogo akaenda Arusha kufungua duka alipoenda TRA kuomba TIN akadakwa kwanza akawekwa ndani.

Alikua anadaiwa kodi ya mwaka naaa...dogo alitoa maelezo lakini hawakumwelewa alifilisiwa na kuwa mmachinga na rasmi
Shukuran kwa ushuhuda, barikiwa sana mkuu
 
Mwambie wewe uliwahi kuandikisha biashara huko nyuma na TIN number yako inadaiwa kodi ya kutosha TRA, hivyo akitumia kitambulisho chako, kule TRA itaflag na kuonyesha kuwa huyu mtu ana TIN yenye malimbikizo ya kodi, hivyo watataka deni lilipwe kwanza kabla ya kuandikisha biashara mpya.
Shukuran sana mkuu
 
Atafilisiwa kitu gani dogo hana hata mia? Dogo msikilize bosi wako huyo ndio anakuweka mjini.
Haina madhara yoyote. Mimi kuna kiNGO nilianzisha kwenye katiba na minutes za kikao huwa naandika ndugu zangu na rafiki zangu hadi sahihi zao naweka na wao wanajua na hawana noma wala nini.
Bongo ni lazima ujiongeze pia ishi na watu vizuri, uwe na network.
Binafsi sijitilii shaka kabisa kwa namna ninavyoishi na watu ila wao ndio nawatilia shaka mkuu
 
Weka Mambo wazi kitambulisho gani hasa Cha kupigia kura au kitambulisho chaTaifa ,

Boss huyo ni ndugu yako au ?Kama sio ndugu vip mbona mapema hivyo kujuana !?
Mapema Mno shituka ,kazi yenyewe unafanya usiku ,isitoshe ww mwenyewe hufaamiki na mtu yoyote umeonyesha udhaifu mkubwa mno,; Sijajua ww ni jinsia gani!?
!
Mkuu kitambulisho ni cha mpiga kura, boss sina undugu nae na mimi ni ME!
 
Kama anacho cha kwake na hatako kukitumia lazima akupe sababu, asije akawa anafungua biashara ya kutakatishia fedha.

Ukidakwa hapo haina dhamana, mpaka uchunguzi ukamilike unawezakujikuta upo ndani hata miaka mitano, halafu hukumu ikitoka unatandikwa faini na kifungo cha kujitosheleza.

Lazima upewe sababu zote, usifanye kwa sababu ya nidhamu ya uwoga unaweza kujiharibia maisha yako yote kwa kibarua cha muda mfupi.
Shukuran kwa maoni mkuu
 
yeah italeta maana kwasababu kwenye loss report kitambulisho kitakachoonekana ni hicho ambacho kipo kwa Boss. Hata kama akirenew bado hii loss report itakuwa na nguvu maaana ukirenew unapewa kitambulisho kipya ila Boss anaendelea kutumia kile cha zamani ambacho ndio ulishitaki kuwa kimepotea. So, siku likibuma inakuwa rahisi kumruka Boss.


Ila Idea ya Loss report sio nzuri kwa sababu ukitoa taarifa polisi kuwa hicho kitambulisho kimepotea, maana yake nawewe hutakiwi kukitumia tena kwenye inshu zako maana si umesema kimepotea...Na kwa jinsi ilivyo ngumu kurenew au kupata ID za NIDA basi mtoa mada atakuwa amejifunga kifungo huru...Jibu ni simple, AKATAE.
Kitambulisho kinapotea unakipata mbona kawaida sana assume umepoteza kadi ya benk umeripoti alafu baada ya wiki kuna mtu kaokota kakupa utaacha kukitumia kwa sabb ulikikatia lost report?
 
yeah italeta maana kwasababu kwenye loss report kitambulisho kitakachoonekana ni hicho ambacho kipo kwa Boss. Hata kama akirenew bado hii loss report itakuwa na nguvu maaana ukirenew unapewa kitambulisho kipya ila Boss anaendelea kutumia kile cha zamani ambacho ndio ulishitaki kuwa kimepotea. So, siku likibuma inakuwa rahisi kumruka Boss.


Ila Idea ya Loss report sio nzuri kwa sababu ukitoa taarifa polisi kuwa hicho kitambulisho kimepotea, maana yake nawewe hutakiwi kukitumia tena kwenye inshu zako maana si umesema kimepotea...Na kwa jinsi ilivyo ngumu kurenew au kupata ID za NIDA basi mtoa mada atakuwa amejifunga kifungo huru...Jibu ni simple, AKATAE.
Kisa kitambulisho? Hivi unajua mawakala wanasajilia watu wa ngapi vitambulisho vya watu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom