Bosi wa mashuhushu wanaomlinda Obama alivyojiuzulu ni darasa kwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa

DaveSave

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
440
637
Kama mtu mwenye uelewa kiasi kuhusu utendaji kazi wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, nimekuwa 'nikipiga kelele' mara kwa mara kuhusu haja ya mageuzi ndani ya taasisi hiyo nyeti. Kwa bahati mbaya sio tu kelele hizo ni vigumu kueleweka kwa Watanzania wengi, uwezekano wa kusikilizwa ni mdogo hasa ikizingatiwa kuwa asili ya taasisi hiyo ni kutekeleza majukumu yake kwa siri, na kama hiyo haitoshi, mara nyingi wahusika wa taaluma hiyo inayopaswa kuhusisha matumizi ya hali ya juu ya akili, hawapendi kusikia ushauri wa 'walio nje' kama akina sie.

Mageuzi ninayoyapigia kelele ni ya kimfumo. Kubwa zaidi ni haja ya uwepo wa mazingira ya uwajibikaji pale watu wanapoboronga. Moja ya dhana zinazotawala fani ya ushushushu ni ile isemayo 'kushamiri kwa matishio ya usalama katika nchi husika ni dalili kuwa taasisi ya ushushushu katika nchi husika ina mapungufu.' Sasa huhitaji uelewa wa fani hiyo kutambua kushamiri kwa matishio kadhaa ya usalama katika Tanzania yetu, kubwa zaidi likiwa ufisadi.

Labda waweza kujiuliza, iweje ufisadi uwe tishio la usalama? Jibu jepesi ni kwamba ufisadi unatoa fursa kwa maadui wa ndani na nje wa taifa kutimiza azma zao kwa urahisi. Kwa mfano, laiti kukiwa na ufisadi kwenye mipaka ambapo wahusika wanaruhusu kirahisi tu wageni kuingia nchini pasi kuzingatia taratibu zilizopo, ni rahisi kwa magaidi kutumia mwanya huo.

Ufisadi unaweza kutuletea tapeli la kimataifa kuwekeza kwenye maeneo yanayofahamika kiusalama kama 'vituo muhimu' (vital installations) kama vile viwanja vya ndege na bandarini.

Sasa tukichukulia mfano wa ufisadi, sio tu umeshamiri vya kutosha lakini ndo wazidi kuongezeka. Kuna wanaojiuliza je TISS (Idara yetu ya Usalama wa Taifa) ipo likizo ndefu, wahusika wapo katika usingizi fofofo au kazi imewashinda? Mie sina jibu la moja kwa moja lakini nadhani tatizo la TISS ni la kimfumo zaidi kuliko kiutendaji, japo utendaji wao nao una walakini.

Lakini kabla ya kuingia kwa undani katika mada hii, nirejee kwenye kichwa cha habari. Majuzi, mkuu wa taasisi yenye jukumu la ulinzi wa viongozi wakuu wa Marekani, Secret Service, Bi Julia Pierson alilazimika kujiuzulu wadhifa huo baada ya mtu mmoja kuingia uzio wa Ikulu ya nchi hiyo na kutishia usalama wa Rais Barack Obama. Kwa wenzetu tukio hilo lilikuwa na uzito mkubwa sana, na lilitawala sana katika vyombo vya habari.
Hata hivyo, kwa vile wenzetu wanaendesha mambo kwa uwazi, mwanamama huyo aliitwa mbele ya kamati moja ya bunge la juu la nchi hiyo na kupewa fursa ya kuieleza, ambapo watunga sheria waliafikiana kwamba anapaswa kujiuzulu.
Julia+Pierson+Testifies+House+Committee+yFaGpsh9L0yx.jpg
gty_barack_obama_secret_service_jt_120416_wmain.jpg

Tukirejea huko nyumbani, ukweli usiopingika ni kwamba licha ya vikwazo vya kimfumo vinavyoikabili TISS, ksingizio cha 'taasisi hii yafanya kazi kwa siri na hakuna anayepaswa kuhoji' kinatoa fursa kwa wazembe kupata kinga katika utendaji wao mbovu. Ndio, kazi za TISS ni za siri lakini so far usiri huo haujafanikiwa kuwawezesha kukabiliana ipasavyo na matishio ya kiusalama, la wazi likiwa ni ufisadi.

Miongoni mwa mapendekezo yangu (yapo mengi) kuhusu haja ya mageuzi ni kama ifuatavyo.

Kwanza, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu unapaswa kufanywa kwa uwazi zaidi, ikiwezekana kuidhinishwa na Bunge. Hiyo itazuia uwezekano wa Rais kumpatia wadhifa huo mtu yeyote yule bila kuzingatia uadilifu na uwezo wake kikazi. Kwa kumpa Rais 'blank cheque' ni rahisi kwake kumchagua mtu wake, au mshkaji wake kwa minajili ya kumlinda au kuwa kibaraka wake badala ya kulitumikia taifa kiufanisi.
IMG_0470.JPG
Pili, ni muhimu TISS kama taasisi iwajibike kwa umma, na si kwa Rais pekee (maana huyo Waziri Katika Ofisi ya Rais mwenye jukumu la kuisimamia TISS anakwazwa na mazingira yalivyo, sambamba na 'uoga' wa kawaida). Ifike mahali, watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa Bungeni, kwa mfano, kuhojiwa kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu taasisi hiyo.

Kiutendaji, ni muhimu kwa taasisi hiyo kupewa uhuru wa kioperesheni utakaoiwezesha kuondokana na hali iliyopo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa kama tawi la usalama la chama tawala. Sambamba na hilo ni haja ya kuitengenezea mazingira yatayoiwezesha kuhakikisha mapendekezo yake kwa Rais yanafanyiwa kazi hata pale Rais anapoyapuuza. Ikumbukwe kuwa licha ya Rais kuwa 'mkuu halisi wa TISS,' yeye bado ni mwananchi kama wananchi wengine ambao TISS inawajibika kuhakikisha sio tu usalama wao bali hawawi tishio kwa usalama huo. Rais anapopuuza ushauri unaotishia usalama wa taifa basi TISS ijengewe mazingira ya kuhakikisha kuwa ushauri wake unafanyiwa kazi.

Nimalizie kwa kutumaini kuwa 'kelele' hizi zitasikika kwa wahusika. Tujifunze kwa wenzetu waliotatutangulia na wahusika wasione aibu kusikia ushauri wa wenye uelewa hata kama wapo nje ya 'uwanja wa mapambano.'
Makala hii imeandikwa na ndugu Evarist Chahali.
 
Nadhani kuna umuhimu wa wananchi wote watambue waz waz kazi na mambo muhimu yafanywao na idara hii muhimu. Kuwa wazi kunasaidia ongezeko la maarifa na ushirikiano wenye tija na manufaa kwa taifa, na kwa mfumo huu kila mwananchi atajua umuhimu wake katika kulilinda taifa letu.Tuweke wazi baadhi ya mambo na taratibu ili hali tukizingatia sheria, kanuni na usalama wa taifa
 
Daaah Mkuu umenena vyema kabisa. Nami huwa najiulza hivi huu wizi mkubwa mkubwa unafanyikaje wataki tunaambiwa TISS ipo kila mahali.. Kwer Mkuu kunahitajika mabadiliko. Mapendekezo uliyo pendekeza yange faa kuwa katika katiba mpya.
 
Sijui mfumo wao wa kutoa ajira,ila nilisikia zamani kuwa wanafuatilia watu tangu shule na kuwarecruit ambapo maajenti wakubwa walikuwa ni walimu,
ila miaka hii mtoto wa mjomba ,wa dada na kila ndugu ndiyonhuingizwa huko,
wapo wengine wanaona ujiko kujitambulisha kwa kuonyesha vitambulisho vyekundu vyenye ngao na wengine kukunjua mashati kuonyesha silaha.
sasa najiuliza mtunkama huyo habari atazipataje?maana ameshajulikana!
wafunzwe maadili sana
 
Mkuu umesema vema sana. Kwanza huo mfumo wa ajira za 'kurithishana' ndiyo uliokuja kuiharibu taasisi hii. Mfumo huu huu vile vile umeliharibu jeshi letu la polisi. Ndiyo maana utaona uadilifu hakuna tena kwani kijana anapewa kazi kwa manufaa ya mkubwa wake.
Pili, hakuna uwazi wa kuajiri watu wawe na vigezo gani ambavyo vitamfanya afit katika kazi husika, hivyo kutoa mwanya kwa mjomba kumleta mpwawe katika kazi na matokeo yake kutengeneza cheni ya kumtumikia 'bwana Fisadi' kuanzia baba.....mjomba mpaka mpwawe.
Tatu, weledi nao imekuwa shida. Hatupingi mtu kapata kazi kupitia kwa shangazi, mjomba nk maana waTz hawakawii kusema 'tunawivu na alichopata mwingine' sasa inshu huyo aliyopata kazi hiyo ana weledi mzuri wa hiyo kazi?
 
Kama mtu mwenye uelewa kiasi kuhusu utendaji kazi wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, nimekuwa 'nikipiga kelele' mara kwa mara kuhusu haja ya mageuzi ndani ya taasisi hiyo nyeti. Kwa bahati mbaya sio tu kelele hizo ni vigumu kueleweka kwa Watanzania wengi, uwezekano wa kusikilizwa ni mdogo hasa ikizingatiwa kuwa asili ya taasisi hiyo ni kutekeleza majukumu yake kwa siri, na kama hiyo haitoshi, mara nyingi wahusika wa taaluma hiyo inayopaswa kuhusisha matumizi ya hali ya juu ya akili, hawapendi kusikia ushauri wa 'walio nje' kama akina sie.

Mageuzi ninayoyapigia kelele ni ya kimfumo. Kubwa zaidi ni haja ya uwepo wa mazingira ya uwajibikaji pale watu wanapoboronga. Moja ya dhana zinazotawala fani ya ushushushu ni ile isemayo 'kushamiri kwa matishio ya usalama katika nchi husika ni dalili kuwa taasisi ya ushushushu katika nchi husika ina mapungufu.' Sasa huhitaji uelewa wa fani hiyo kutambua kushamiri kwa matishio kadhaa ya usalama katika Tanzania yetu, kubwa zaidi likiwa ufisadi.

Labda waweza kujiuliza, iweje ufisadi uwe tishio la usalama? Jibu jepesi ni kwamba ufisadi unatoa fursa kwa maadui wa ndani na nje wa taifa kutimiza azma zao kwa urahisi. Kwa mfano, laiti kukiwa na ufisadi kwenye mipaka ambapo wahusika wanaruhusu kirahisi tu wageni kuingia nchini pasi kuzingatia taratibu zilizopo, ni rahisi kwa magaidi kutumia mwanya huo.

Ufisadi unaweza kutuletea tapeli la kimataifa kuwekeza kwenye maeneo yanayofahamika kiusalama kama 'vituo muhimu' (vital installations) kama vile viwanja vya ndege na bandarini.

Sasa tukichukulia mfano wa ufisadi, sio tu umeshamiri vya kutosha lakini ndo wazidi kuongezeka. Kuna wanaojiuliza je TISS (Idara yetu ya Usalama wa Taifa) ipo likizo ndefu, wahusika wapo katika usingizi fofofo au kazi imewashinda? Mie sina jibu la moja kwa moja lakini nadhani tatizo la TISS ni la kimfumo zaidi kuliko kiutendaji, japo utendaji wao nao una walakini.

Lakini kabla ya kuingia kwa undani katika mada hii, nirejee kwenye kichwa cha habari. Majuzi, mkuu wa taasisi yenye jukumu la ulinzi wa viongozi wakuu wa Marekani, Secret Service, Bi Julia Pierson alilazimika kujiuzulu wadhifa huo baada ya mtu mmoja kuingia uzio wa Ikulu ya nchi hiyo na kutishia usalama wa Rais Barack Obama. Kwa wenzetu tukio hilo lilikuwa na uzito mkubwa sana, na lilitawala sana katika vyombo vya habari.
Hata hivyo, kwa vile wenzetu wanaendesha mambo kwa uwazi, mwanamama huyo aliitwa mbele ya kamati moja ya bunge la juu la nchi hiyo na kupewa fursa ya kuieleza, ambapo watunga sheria waliafikiana kwamba anapaswa kujiuzulu.
Julia+Pierson+Testifies+House+Committee+yFaGpsh9L0yx.jpg
gty_barack_obama_secret_service_jt_120416_wmain.jpg

Tukirejea huko nyumbani, ukweli usiopingika ni kwamba licha ya vikwazo vya kimfumo vinavyoikabili TISS, ksingizio cha 'taasisi hii yafanya kazi kwa siri na hakuna anayepaswa kuhoji' kinatoa fursa kwa wazembe kupata kinga katika utendaji wao mbovu. Ndio, kazi za TISS ni za siri lakini so far usiri huo haujafanikiwa kuwawezesha kukabiliana ipasavyo na matishio ya kiusalama, la wazi likiwa ni ufisadi.

Miongoni mwa mapendekezo yangu (yapo mengi) kuhusu haja ya mageuzi ni kama ifuatavyo.

Kwanza, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu unapaswa kufanywa kwa uwazi zaidi, ikiwezekana kuidhinishwa na Bunge. Hiyo itazuia uwezekano wa Rais kumpatia wadhifa huo mtu yeyote yule bila kuzingatia uadilifu na uwezo wake kikazi. Kwa kumpa Rais 'blank cheque' ni rahisi kwake kumchagua mtu wake, au mshkaji wake kwa minajili ya kumlinda au kuwa kibaraka wake badala ya kulitumikia taifa kiufanisi.
IMG_0470.JPG
Pili, ni muhimu TISS kama taasisi iwajibike kwa umma, na si kwa Rais pekee (maana huyo Waziri Katika Ofisi ya Rais mwenye jukumu la kuisimamia TISS anakwazwa na mazingira yalivyo, sambamba na 'uoga' wa kawaida). Ifike mahali, watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa Bungeni, kwa mfano, kuhojiwa kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu taasisi hiyo.

Kiutendaji, ni muhimu kwa taasisi hiyo kupewa uhuru wa kioperesheni utakaoiwezesha kuondokana na hali iliyopo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa kama tawi la usalama la chama tawala. Sambamba na hilo ni haja ya kuitengenezea mazingira yatayoiwezesha kuhakikisha mapendekezo yake kwa Rais yanafanyiwa kazi hata pale Rais anapoyapuuza. Ikumbukwe kuwa licha ya Rais kuwa 'mkuu halisi wa TISS,' yeye bado ni mwananchi kama wananchi wengine ambao TISS inawajibika kuhakikisha sio tu usalama wao bali hawawi tishio kwa usalama huo. Rais anapopuuza ushauri unaotishia usalama wa taifa basi TISS ijengewe mazingira ya kuhakikisha kuwa ushauri wake unafanyiwa kazi.

Nimalizie kwa kutumaini kuwa 'kelele' hizi zitasikika kwa wahusika. Tujifunze kwa wenzetu waliotatutangulia na wahusika wasione aibu kusikia ushauri wa wenye uelewa hata kama wapo nje ya 'uwanja wa mapambano.'
Makala hii imeandikwa na ndugu Evarist Chahali.
Mkuu kwa namna fulani nashindwa kukubaliana na baadhi ya hoja zako,
kwa mfano kwamba watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa bungeni..

hivi bunge unalolizungumzia ni hili hili au kuna lingine.

Kwa uwezo wa bunge letu lilivyo siamini kama lina uwezo huo, bunge letu linaendeshwa mno kisiasa, hawazingatii weledi wala nini, we angalia tu ile ishu ya escrow ilivyomalizwa kisiasa na sasa wale watuhumiwa karibu wote ndio wako bungeni na baadhi ni wenyeviti wa kamati za bunge.

hawa wabunge wa "naunga mkono hoja" sidhani kama wana ubavu wa kuwaita TISS na kuwahoji ki-weledi, bila kuingiza siasa za vyama..

hoja yao ina mashiko kabisa lakini si kwa bunge letu labda kwa miaka ijayo...
hivi bunge letu mnalionaje?
 
...hao TISS si ndio sehemu ya hao wezi(mafisadi),sasa sijui unategemea nini?!
 
Mkuu kwa namna fulani nashindwa kukubaliana na baadhi ya hoja zako,
kwa mfano kwamba watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa bungeni..

hivi bunge unalolizungumzia ni hili hili au kuna lingine.

Kwa uwezo wa bunge letu lilivyo siamini kama lina uwezo huo, bunge letu linaendeshwa mno kisiasa, hawazingatii weledi wala nini, we angalia tu ile ishu ya escrow ilivyomalizwa kisiasa na sasa wale watuhumiwa karibu wote ndio wako bungeni na baadhi ni wenyeviti wa kamati za bunge.

hawa wabunge wa "naunga mkono hoja" sidhani kama wana ubavu wa kuwaita TISS na kuwahoji ki-weledi, bila kuingiza siasa za vyama..

hoja yao ina mashiko kabisa lakini si kwa bunge letu labda kwa miaka ijayo...
hivi bunge letu mnalionaje?
Sidhani kama ni lazima wabunge wote wawahoji ailimradi tu.Wanaweza teuliwa wabunge maalum kuwahoji wenye weledi.
 
Mtu anaerukia na kusema "tatizo ni la kimfumo" bila kuainisha tatizo lenyewe mimi humuona ni punguani anayejaribu kutafuta kosa asilolijuwa au lisilokuwepo.
 
Mkuu kwa namna fulani nashindwa kukubaliana na baadhi ya hoja zako,
kwa mfano kwamba watendaji wakuu wa TISS waweze kuitwa bungeni..

hivi bunge unalolizungumzia ni hili hili au kuna lingine.

Kwa uwezo wa bunge letu lilivyo siamini kama lina uwezo huo, bunge letu linaendeshwa mno kisiasa, hawazingatii weledi wala nini, we angalia tu ile ishu ya escrow ilivyomalizwa kisiasa na sasa wale watuhumiwa karibu wote ndio wako bungeni na baadhi ni wenyeviti wa kamati za bunge.

hawa wabunge wa "naunga mkono hoja" sidhani kama wana ubavu wa kuwaita TISS na kuwahoji ki-weledi, bila kuingiza siasa za vyama..

hoja yao ina mashiko kabisa lakini si kwa bunge letu labda kwa miaka ijayo...
hivi bunge letu mnalionaje?
Khaa... bana mie napenda sana kuangalia tamthilia za vichekesho, sasa mjomba Nape kaondoa live! kwangu shida tupu!
 
Evarist Chahal ana elimu gani au uzoefu gani kwenye maswala ya usalama na vyombo vya usalama?
 
Tatizo la Watanzania huwa tunajifanya tunajua kila kitu hivuo basi kuna vitu vingine havipaswai kuwekwa hadharania maana kila mtu atajifanya kukosoa...TISS inaprotocol zake na inashangaza kama ww unasema "upo nje" alafu unakosoa utendaji kazi wake..Umejuaje!?? Pia hii inamaanisha either upo ndani means u r a traitor au kuna punguani anakuvujishia vitu visivyokuhusu...wat should we do!??:: we shuld leave it and let it go..they know how to handle their own... and USA is "miles" away frm where we are I mean in"all spheres of life"so I suggeat we shouldnt use USA as our reference point...wazi!?
 
Mifumo yetu yote. Inaiga huko ughaibuni. Tiss waige pia usa.kwa sana. Hata wanajeshi wetu wamewahi kujifunza mbinu china,urusi,cuba nk. Tiss nao wawe walinda usalama wa taifa. Uchumi ukiwemo.....nawapa hongera ila wazidishe uzalendo kwa nchi.
 
Evarist Chahali mwenyewe ni TISS maarufu kabisa, sa hivi kakimbili uscoch, ni mtoro anayewindwa sana na ex TISS wengi akiwamo membe
 
Hana lolote..Uwe secret service alafu MAARUFU...it doesn't make sense ni njaa tu ndo zinamsumbua..
 
Hii nchi hii kila mtu mjuaji. Mambo ya ulinzi na usalana yana miiko na taratibu zake kulingana na nchi husika sasa izo habari za kutaka mkurugenzi akajadiliwe na akina Lema na Lisu huu ni uwenda wazimu vipo vigezo vinavyotumika kuchagua viongozi kama hao wa juu hawakurupuki. Itafika mda mtataka kutuchagulia mpaka mkuu wa Majeshi awe nani nchi haiendeshwi kwa kukariri hususani kwenye mambo nyeti kama haya ya Ngoswe tuachie wenyewe akina Ngoswe.
 
Back
Top Bottom