Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,446
PARIS,UFARANSA
Ofisa mtendajiu mkuu wa kampuni ya kutengeneza ndege ya Airbus anatarajiwa kuweka mfukoni dola 41 milioni ya kifuta jasho wakati atakapoachia ngazi wiki ijayo, kwa mujibu wa mahesabu yaliyofanywa na kampuni ya ushauri kwa wawekezaji na kutolewa leo.
Kampuni hiyo ilikubaliana na ukubwa wa ukokotoaji huo uliofanywa na Proxinvest, ambao ulitokana na taarifa za kifedha zilizokuwa zinajazwa chini ya utawala wa ofisa huyo mtendaji mkuu Mjerumani, Tom Enders.
Enders, 60, ataachia ngazi wakati wa mkutano wa wanahisa utakaofanyika Amsterdam, ambako ni makao makuu ya kampuni hiyo kubwa.
Malipo hayo hayatapigiw kura katika mkutano huo wa wanahisa, kama ilivyo kwa mwongozo wa viwango vya kampuni kubwa ambao uliimarishwa na chama cha waajiri nchini Ufaransa mwaka jana.
Kwa mujibu wa Proxinvest, Enders atapokea Euro 26.3 milioni kama malipo ya kustaafu kwa kipindi cha miaka 20 ijayo, pamoja na bonasi na malipo mengine yanayofikia Euro 7.3 milioni.
Pia atanufaika na kipengele kilicho kwenye mkataba wake kinachomzuia kufanya kazi na kampuni nyingine kwa mwaka mmoja ambacho kitampatia Euro 3.2 milioni
"Kipengele hicho kinagharimu fedha nyingi, miezi 12 inakwenda haraka sana," mkurugenzi wa Proxinvest, Loic Dessaint aliiambia AFP.
"Kama anataka kuwa mshauri wa kampuni nyingine katika kipinmdi cha mwaka mmoja na nusu, anayo haki," alisema.
Kwa ujumla, Enders atapata malipo ya jumla ya euro 36.8 milioni.
Donge hilo nono litaibua mijadala nchini Ufaransa, kutokana na serikali ya Ufaransa kumiliki asilimia 11 ya hisa kwenye kampuni hiyo ya kutengeneza ndege, huku Ujerumani ikimiliki asilimia 11 na Hispania asilimia 4.2.
Taarifa za vyombo vya habari zinadai kuwa Enders alitangaza kujiuzulu baada ya kutoungwa mkono na bodi mpya.