Bora kuuza nafsi kwa shetani kupata utajiri kuliko kuwa maskini

Aigle

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
711
6,186
Umaskini ni laana, umaskini ni aibu, umaskini ni kilio, umasikini ni manyanyasiko, hakuna furaha yoyote unayopata kwa kua maskini.

Nimeshashuhudia maskini akikata roho kwenye korido za hospitali sababu hakua na uwezo wa kulipa hela ya kufungua faili tu, yani kufungua faili tu. Nimeshashuhudia maskini akikata roho sababu tu hakua na hela ya kulipia oksijeni kipindi cha korona ikiwa imepamba moto. Nimeshashuhudia maskini akimzika mtoto wake sababu alikosa elfu 20 ya dawa.

Ewe devil, ewe shetani nakuomba msamaha kwa kua mjinga kwa muda mrefu kwa kufikiria na kufundishwa uongo kwamba wewe ndio chanzo cha watu kupata matatizo kumbe sivyo. Wewe ndie unayetoa utajiri, wewe ndie unayetoa mafanikio, elimu kubwa za kidunia ambazo nchi za magharibi wanatumia kupitia wasaidizi wako kuleta mafanikio katika nchi zao.

Nakuomba msamaha tena kwa kukubali kufundishwa uongo na mapadre na wachungaji wa uongo na feki na wanafiki waliokua wanatuaminisha kwamba wewe ni mbaya kumbe sivyo na walikua na bado wanaendelea kudanganya mamia kwa maelfu ya watu ili tu wao wapate au waendelee kupata utajiri mkubwa kupitia hao hao maskini.

Ninasubiri sana kukutana na wewe na kunipatia kile nachohitaji ambacho ni utajiri. Nimeamua kukubali kufunguka akili na kuacha kua MTUMWA wa dini feki na kuwa mtumwa wa umaskini.

Hail Lucifer.
 
Mzee Baba ni hivi...

Pesa ni ngumu hata ukiamua kumfuata shetani. Hivi unadhani ingekuwa kuwa upande wa shetani tu inatosha kupata pesa ni wangapi wangebaki?

Nakuambia hivi hata leo umeandika hayo yote kumuomba shetani, hakuna Suprise ya kiuchumi utaipata, zaidi atakutuma ukaibe, ule moto awahi kupata maokoto yake.

Shetani hatoi Pesa, ukienda hueleweki anagawa matatizo, kwa ufupi nayeye ana vigezo vyake, sio umejichokea huko huna mbele wala nyuma Ajihangaishe na wewe wa nini nakati tayari upo nyavuni.

Plus waliokata tamaa kama wewe hawataki, maana anajua tayari ni mteja wake, anataka wale wagumu.
Kwahio mzee baba wewe ni rafiki wa shetani usijali, sema tuu hana mpango na wewe, tafuta njia nyingne.
 
Ingekuwa shetani yuko sehemu fulani ametulia na mabegi ya hela, ningeshaenda kitambo kumsujudia.

Ila sasa vijiweni zimejaa stori za vitisho ambavyo kimsingi hakuna ukweli.

Umasikini ni kama laana kwakweli.

Ukosefu wa pesa ni hali imayofedhehesha sana.

Yaani mtu unakuta hata hela ya kodi ya nyumba unaiwazia mara mbilimbili utaipata wapi, wakati kodi yenyewe haizidi 50k kwa mwezi.
 
Utajiri ni wakutafutwa sana mkuu sana sana tena utajiri wa kizazi chako chote 'generational wealth' kuna jamaa ndugu zake humtukana sana yuko busy hawakumbuki ana roho mbaya ila akifika kijijini wote meno nje WHY messiah amefika ni fanaka mwendo wa mpunga, pombe na sifa kede kede na machawa kibao hata ukienda kanisani wanakupa heshima inayoendana na mfuko wako. Kama huna hela utabeba magita, vinanda na kusafisha kanisa.
 
Back
Top Bottom