Bora hata Shukuru Kawambwa, Prof Ndalichako anaharibu elimu yetu

Ukweli usiopingika kuwa prof ndalichako anaharibu elimu yetu kabisa elimu ya msingi sasa kusomwa kwa miaka sita kila kitu tunachokiona ndani ya wizara ya elimu kwa sasa ni kufanya mambo bila utafiti wowote mwisho wa siku kila kitu kinawashinda tu mfano walianza na ada elekezi shule binafsi lakini ikawashinda ,wameshindwa kuajiri walimu kuziba pengo wameshindwa kulipa madai ya walimu .

Bora enzi za kikwete kuliko awamu hii maana elimu ndoo inakufa kabisa wameshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wote ,gharama za vyuo vya ualimu vya serikali mfano butimba TTC zimeongezeka na kuwa vyuo vya kusoma matajiri tu hakuna wa kutetea haya bora shukuru kawambwa karo ya hivyo vyuo ilikuwa elfu sabini sasa hivi laki sita jumla na michango laki Tisa kwa mwaka .
Mkuu, hiyo sera ilianza na kutangazwa tangu Kawambwa akiwa Waziri wa Elimu, hayo ni marekebisho ya sera ambayo inatekelezwa ktk awamu hii.
Hata hivyo, watakaouguswa na mabadiliko hayo ni wale waliopo darasa la tatu. Wale waliopo darasa la nne wataendelea hadi darasa la saba.

Vv
 
Trump bhana ...We do not want Intelligence to interfere politics and politics to interfere the intelligence. ..
...Msiniulize kwanini nimeandika hivyo ila watakao elewa najua tayari mmeelewa
 
Naunga mkono hoja ya shule ya msingi miaka 6

Ni uamuzi sahihi muda mwingi mtu anapoteza kusoma mbona leo watu wanasoma QT miaka 2 na wanafauli

Why miaka saba ya shule ya msingi achen mawazo mgando
Ndio uharibifu wenyewe huo wa elimu, watu hawasomi ili wafaulu mitihani we vipi wewe?!

Mtihani ni kipimo cha kwanza cha uelewa, lkn tunachohitaji ni maarifa. Unaweza hata ukakaririshwa kwa siku 60 tu na ukafaulu mtihani lkn uwezo wako wa kufikiri ukawa haujatanuka.
 
Ukweli usiopingika kuwa prof ndalichako anaharibu elimu yetu kabisa elimu ya msingi sasa kusomwa kwa miaka sita kila kitu tunachokiona ndani ya wizara ya elimu kwa sasa ni kufanya mambo bila utafiti wowote mwisho wa siku kila kitu kinawashinda tu mfano walianza na ada elekezi shule binafsi lakini ikawashinda ,wameshindwa kuajiri walimu kuziba pengo wameshindwa kulipa madai ya walimu .

Bora enzi za kikwete kuliko awamu hii maana elimu ndoo inakufa kabisa wameshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wote ,gharama za vyuo vya ualimu vya serikali mfano butimba TTC zimeongezeka na kuwa vyuo vya kusoma matajiri tu hakuna wa kutetea haya bora shukuru kawambwa karo ya hivyo vyuo ilikuwa elfu sabini sasa hivi laki sita jumla na michango laki Tisa kwa mwaka .
Mama anatekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014 K kama sijakosea. Kufuatana na sera hiyo elimu ya msingi ni miaka sita. ( Swali. Mama ndalichako alikuwa waziri wakati wa maandalizi ya sera?) Kosa lake ni Kutekeleza sera iliyoandaliwa na wataalamu?

Ada yang vyuo vya ualimu ( Teachers colleges fees) ilipandishwa baada ya vyuo kujiunga na mfumo wa NACTE. wakati Huo mama Ndalichako hakuwa na nafasi yeyote wizarani.

No research no right to speak.
 
Hivi sisi kama taifa hatuna sera ya elimu ambayo itaheshimiwa na mawaziri wote watakaopita kwenye wizara hiyo ili kuepuka waziri kufanya anavyoona yeye inafaa?
 
Huko nyuma ilishawah kutokea Waziri mmoja kuvuruga Elimu ya Sekondary, tunaomba mabadiliko yoyote yafanyike baada ya tafit za Kisayansi kuprove na isiwe vinginevyo
Nakumbuka alikuwa marehemu joseph mungai
 
Ukweli usiopingika kuwa prof ndalichako anaharibu elimu yetu kabisa elimu ya msingi sasa kusomwa kwa miaka sita kila kitu tunachokiona ndani ya wizara ya elimu kwa sasa ni kufanya mambo bila utafiti wowote mwisho wa siku kila kitu kinawashinda tu mfano walianza na ada elekezi shule binafsi lakini ikawashinda ,wameshindwa kuajiri walimu kuziba pengo wameshindwa kulipa madai ya walimu .

Bora enzi za kikwete kuliko awamu hii maana elimu ndoo inakufa kabisa wameshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wote ,gharama za vyuo vya ualimu vya serikali mfano butimba TTC zimeongezeka na kuwa vyuo vya kusoma matajiri tu hakuna wa kutetea haya bora shukuru kawambwa karo ya hivyo vyuo ilikuwa elfu sabini sasa hivi laki sita jumla na michango laki Tisa kwa mwaka .
Huu ni uandishi wa kukurupuka kaka. Umeanza vizuri waziri anaua elimu kwa uamuzi wa kuifanya shule ya msingi miaka sita bila tafiti. Mi nilizani wewe ungetuambia hizi mtoto kumaliza shule ya msingi miaka sita kuna madhara gani. Kama kweli umesoma vizuri elimu ya msingi niambie darasa la saba kuna lipi la nyongeza zaidi. Hivi kenya shule ya msingi ni miaka mingapi. Mi nazani ni wazo jema na hakuna tafiti inayoonyesha mtoto akianza sekondari akiwa na miaka kumi na tatu ni shida. Ulaya mtu ana miaka 30 ameshapata PhD umefuatilia mfumo wa elimu wao.
 
Ukweli usiopingika kuwa prof ndalichako anaharibu elimu yetu kabisa elimu ya msingi sasa kusomwa kwa miaka sita kila kitu tunachokiona ndani ya wizara ya elimu kwa sasa ni kufanya mambo bila utafiti wowote mwisho wa siku kila kitu kinawashinda tu mfano walianza na ada elekezi shule binafsi lakini ikawashinda ,wameshindwa kuajiri walimu kuziba pengo wameshindwa kulipa madai ya walimu .

Bora enzi za kikwete kuliko awamu hii maana elimu ndoo inakufa kabisa wameshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wote ,gharama za vyuo vya ualimu vya serikali mfano butimba TTC zimeongezeka na kuwa vyuo vya kusoma matajiri tu hakuna wa kutetea haya bora shukuru kawambwa karo ya hivyo vyuo ilikuwa elfu sabini sasa hivi laki sita jumla na michango laki Tisa kwa mwaka .
Usiongee vitu usivo vifahamu mpango wa muundo mpya wa Elimu ulianza tokea 2014 na ulikua ukiandaliwa kibaha usikurupuke.
No information no rights to speak
 
Naunga mkono elimu ya msingi kuwa miaka sita.
Mtoto anasoma awali mwaka1 ,chekechea mwaka 1, darasa la kwanza na la pili anasoma nini? Utakuta vitu almost ni vile vile tu.
 
Ndalichako ni kati ya mawaziri 10 wabovu kabisa kuwahi kuwepo nchi hii , wanaongozwa na Dk Mpango .

Kuna mambo kibao ya kushughulikia kwenye elimu lakini siyo MAJOHO wala miaka 7 , lipeni madeni ya walimu kwanza .
Kwanza hii ya kufuta darasa moja na kuanzisha mtaala mpya ni kuanzisha gharama mpya na kubwa muno maana utahitaji syllabus mpya,vitabu vipya toka la 1 na mafunzo kwa walimu tena yaani ni shida.Huyu mama ni mbovu muno.
 
Hivi sisi kama taifa hatuna sera ya elimu ambayo itaheshimiwa na mawaziri wote watakaopita kwenye wizara hiyo ili kuepuka waziri kufanya anavyoona yeye inafaa?
Hili ndilo swali bora lililowahi kuulizwa hapa jf tangu mwaka 2017 uanze , Ndalichako akijibu hili sitamsakama tena .
 
Ndiyo maana mimi niliapa kuwa nikiwa hai watoto wangu wote hawatasoma shule za Kata, hebu fikiria miaka saba kulikuwa na wanafunzi wengi walikuwa wanamaliza bila kujua kusoma na kuandika achilia mbali hesabu, sasa ukifanya miaka sita itakuwaje

Na ndipo shida kubwa ilipo, bado haujaweza kuvuka kutoka umimi kwenda kwenye usisi, ambayo ni hatua muhimu kwa Binadamu unajifikiria wewe tu na familia yako, hapa tunaongelea kuhusu Elimu ya Watanzania ya Tanzania na siyo wapi utapeleka mtoto wako kusoma!
 
Ni suala lililofanyiwa utafiti muda mrefu,walioko darasa la tatu sasa,ndio wataishia la sita na kisha kujiunga na kidato cha tatu hadi nne ambayo sasa darasa la awali hadi kidato cha nne itajulikana kama ELIMU MSINGI,na hii ni lazima kwa kila mtoto wa Tanzania,kama vile ilivyo kwa sasa kwa ELIMU YA MSINGI!
Kama waliopo darasa la 3 kwa sasa ndo wanaishia la 6 hivyo unataka kutuambia kwa mwaka huo kutakuwa na wahitimu wa darasa la 6 na hao wa darasa la 7?
 
Back
Top Bottom