Bora hata Shukuru Kawambwa, Prof Ndalichako anaharibu elimu yetu

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Ukweli usiopingika kuwa prof ndalichako anaharibu elimu yetu kabisa elimu ya msingi sasa kusomwa kwa miaka sita kila kitu tunachokiona ndani ya wizara ya elimu kwa sasa ni kufanya mambo bila utafiti wowote mwisho wa siku kila kitu kinawashinda tu mfano walianza na ada elekezi shule binafsi lakini ikawashinda ,wameshindwa kuajiri walimu kuziba pengo wameshindwa kulipa madai ya walimu .

Bora enzi za kikwete kuliko awamu hii maana elimu ndoo inakufa kabisa wameshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wote ,gharama za vyuo vya ualimu vya serikali mfano butimba TTC zimeongezeka na kuwa vyuo vya kusoma matajiri tu hakuna wa kutetea haya bora shukuru kawambwa karo ya hivyo vyuo ilikuwa elfu sabini sasa hivi laki sita jumla na michango laki Tisa kwa mwaka .
 
Ndiyo maana mimi niliapa kuwa nikiwa hai watoto wangu wote hawatasoma shule za Kata, hebu fikiria miaka saba kulikuwa na wanafunzi wengi walikuwa wanamaliza bila kujua kusoma na kuandika achilia mbali hesabu, sasa ukifanya miaka sita itakuwaje
 
Ndiyo maana mimi niliapa kuwa nikiwa hai watoto wangu wote hawatasoma shule za Kata, hebu fikiria miaka saba kulikuwa na wanafunzi wengi walikuwa wanamaliza bila kujua kusoma na kuandika achilia mbali hesabu, sasa ukifanya miaka sita itakuwaje
Mzee sio kata tuu si umesikia wamepiga marufuku private ule mtihani wakuwachuja watu kuwatengeneza kuwa vipanga.mm sikuwahi kumkubali na bado haitatokea huyu mama
 
Kwa hili mi nammunga mkono waziri ....

Kwanza elimu yetu ilikuwa ni ya kukua tu darasani yaani masomo unayoyasoma primary school ndio hayo hayo unaenda kusema O level........

Kwa luga mbili tofauti hivyo inaoneka kama vile primary school ni elimu ya mtoto kukua....

Ndalichaka yupo sahihi kabisa sema Mimi nachotaka elimu yetu yote iwe kwa kingereza kuanzai nursery mpaka chuo kikuu.....

Sio kuzalisha watu wasiojua kutafasiri hata mikataba ya nchi....
 
Huyu mama mi simkubali kabisa na nnaomba hizi habari za mawaziri kuchezea elimu zetu zife kabisa kwan kila waziri akingia analeta jambo lake naomba kuwe na chombo maalam kitachoweza badili mfumo wa elimu tz sio kuptia waziri leo kamka na wazo hili afanye hii sio fair jamn huyu mama simpendi kiac nkimkuta simba ana mla mie namkatia kachumbari
 
Huko nyuma ilishawah kutokea Waziri mmoja kuvuruga Elimu ya Sekondary, tunaomba mabadiliko yoyote yafanyike baada ya tafit za Kisayansi kuprove na isiwe vinginevyo
 
Mzee sio kata tuu si umesikia wamepiga marufuku private ule mtihani wakuwachuja watu kuwatengeneza kuwa vipanga.mm sikuwahi kumkubali na bado haitatokea huyu mama
Huyu mama naye ni jipu pia aisee.... Kazi yake ni Kuchora mazombi tu kwenye wizara yake
 
Hii ndalichako ameikuta ni Sera ya elimu ya 2014 hii ni kutokana na lifespan yetu mtu anapoteza miaka mingi shuleni,so 2014 ndio sera ya elimu ilipendekeza hivi na pia miaka ya primary itashushwa,na advance walitaka iwe mwaka mmoja tu.
 
Sita mingi sana wangefanya LA NNE sababu hawana wakijuacho watoto siku hizi zaid ya kuimba mistari tu
 
Back
Top Bottom