BOOM Halitoshi Kununua Computer

Nov 13, 2015
19
6
Nimekutana na wanafunzi wengi wa vyuo ambao angalau wanapokea Fedha za kujikimu kutoka Bodi ya mikopo lakini wanalalamika sana kwamba Mkopo haukidhi mahitaji.

Ni kweli Katika soko laptop mpya inagharimu angalau 550,000 ikiwa na sifa za kawaida yaani Intel Celeron, RAM 2GB, HDD 500GB.
Garama hiyo Ni kubwa mno, akinunua itamlazimu kujibana sana (UDSM wanajua misemo yao; utasikia Shatopori, RB nk).

USHAURI
Wanavyuo wanaweza kununua Laptop zilizotumika kwa garama nafuu Na zikafaa kutimiza kusudi lilelile. Katika soko Kuna Brand Na Model ambazo zilitengenezwa kwa viwango vya Juu sana, hivyo basis ukinunua used upo salama. Hp Probook Na Elitebook ziko vizuri. Dell Latitude E6300, E6400, E6500 pia ziko vizuri. Zikiwa na Intel Core 2Duo, RAM 2GB na HDD 160GB Bei huwa kati ya Tzs 320,000 hadi 380,000/-
Wanafunzi wengi hukwazika sana kununua laptop yenye hard disk ndogo kama 80GB au 160GB. Hard Disk sio tatizo, tatizo Ni matumizi mabaya ya raslimali. Wanafunzi wengi hujaza mamuvis, maseries , masizonz, mapo.. na Kila uchafu atakoukuta kwa rafiki au torrent.

Muhimu sana kujua mahitaji ya msingi. Notes za kusoma chuo miaka Minne hazifiki 10GB. Vinginevyo kutakuwa na video na audio .
Kupata ushauri wa Bure namna ya kuchagua wapi pa kununua piga 0715130212 au 0788130212
 
Umejitangaza vizuri, mantiki ni kwamba unauza computer, nipe Coi 7 ya brand yoyite ile isiwe Refurbished, nicheki PM basi
 
kuna hela ya stationery 200,000 kwa mwaka. kama unasoma miaka 3 inakuwa 600,000

sababu computer inaweza kuwa part ya stationery ongeeni na wahusika wawe wanawanunulia hizo pc kwa kuwakata hizo hela pamoja na kuwafanyia subsidy.
 
Ukiamua unanunua tu, mimi serikali ilikuwa inanilipia 40% na najilipia iliobaki, na nyumban walikuwa hawahusiki na iyo 60% iliobaki, niliweza kununua laptop ya tsh 460000/= kwa boom ilo ilo, sifa za mi sub woofer, pasi, majagi ya umeme yote nilikuwa nayo, zaidi sana nilipofika mwaka wa pili nikafungua salon ya kiume nje ya chuo kwa boom iloilo na kufika mwaka wa tatu, nikabadili laptop nikanunua ya lak 7 maana salon kama zao la boom ilikuwa ikifanya vema zaidi.

Nipo kazini mpk leo natumia ileile laptop yangu ya mwisho. Boom na maisha ya chuo nikunyima na kuacha starehe sana, na sifa kwa madem, alafu ukubali kula ekalisti na wakati boom ikichelewa, au ukiwai ingiziwa hakikisha hufamihani na demu yeyote isipokuwa group disc basi.
 
Mkuu umegusa mule mule. Kwanza umenipa ushauri safi. Jana nipo room nilikua najiuliza sana kuhusu hili boom na bei za laptop. Nikaona nikitaka ufahari wa kunnua mzigo mpya ntafeli. Ishu kutafuta used.

Ishu ni kufikia lengo tu. Hizo mbwembwe waachie watoto wa kishua.sie wengine wazazi kusikia boom wanajua ushapata kazi TRA. Wanaanza kukuchukulia tofauti na awali.

Mi sitegemei nikirudi likizo kama ntaendelea kula nyumbani tena. Kama we ni mwanachuo na mtoto wa mkulima, basi ipigie sana hesabu hii miezi. August, September na October baada ya kumaliza mwaka wa kuanza.
Vilevile usisahau kuna ada ya kuingia mwaka wa pili. Kama una 100% is ok. Lakini kama boom lako la kuchovya changa karata zako vizuri.
 
Guys kuna mtu anajua bei ya chromes?(chromebooks) Au sehemu zinapouzwa? Nasikia ni nzuri kwa kusomea na ziko specifically made kwa ajili ya wanafunzi,chuo n.k
 
Zipo mitaani wengi wanaziuza hawazitaki.

Ni nzuri kusomea ila utachapa kazi na kuprint wapi? Sababu printer nyingi na alignment inayotumika ni ya microsoft office ukitumia app nyengine za office kuna uwezekano mkubwa hio kazi isitokee vizuri kwenye microsoft word.

Pia app zake zinahitaji uwe online muda wote, hivyo huwenda ikakupa tabu ukiwa huna net.

Imagine browser ya computer na addons zake ndio chromebook ilivyo.

Mara mia uwe na 2in1 za windows kuliko chromebook.
 
Nimekutana na wanafunzi wengi wa vyuo ambao angalau wanapokea Fedha za kujikimu kutoka Bodi ya mikopo lakini wanalalamika sana kwamba Mkopo haukidhi mahitaji.

Ni kweli Katika soko laptop mpya inagharimu angalau 550,000 ikiwa na sifa za kawaida yaani Intel Celeron, RAM 2GB, HDD 500GB.
Garama hiyo Ni kubwa mno, akinunua itamlazimu kujibana sana (UDSM wanajua misemo yao; utasikia Shatopori, RB nk).

USHAURI
Wanavyuo wanaweza kununua Laptop zilizotumika kwa garama nafuu Na zikafaa kutimiza kusudi lilelile. Katika soko Kuna Brand Na Model ambazo zilitengenezwa kwa viwango vya Juu sana, hivyo basis ukinunua used upo salama. Hp Probook Na Elitebook ziko vizuri. Dell Latitude E6300, E6400, E6500 pia ziko vizuri. Zikiwa na Intel Core 2Duo, RAM 2GB na HDD 160GB Bei huwa kati ya Tzs 320,000 hadi 380,000/-
Wanafunzi wengi hukwazika sana kununua laptop yenye hard disk ndogo kama 80GB au 160GB. Hard Disk sio tatizo, tatizo Ni matumizi mabaya ya raslimali. Wanafunzi wengi hujaza mamuvis, maseries , masizonz, mapo.. na Kila uchafu atakoukuta kwa rafiki au torrent.

Muhimu sana kujua mahitaji ya msingi. Notes za kusoma chuo miaka Minne hazifiki 10GB. Vinginevyo kutakuwa na video na audio .
Kupata ushauri wa Bure namna ya kuchagua wapi pa kununua piga 0715130212 au 0788130212

Huhuuuuhuuuuh eti masizonz ......LOL
 
dah .kama umeniguza ..ha ha ha ha .anyways ngoja nikucheki kwa phone .ili boom kwa watoto wa wakulima mnaojifanya mnajua wakati mmekuja mjini kwa mara ya kwanza ndo mmefikia chuo .msiposkiliza ushauri kama huu mtakuwa omba omba gafla ha ha
 
Mi nashauri nunua laptop yoyote ile ya around 250,000-350,000 mtumba tafuta na printer kwa 120,000 anza ku print kwa wana huko chuoni 100 na 200 za kuprint zitakufaaa kipindi usichotegemea....
 
Asante Savimbi Jr. Nakupa bure Kaspersky Antvirus Key T9HDW-RM3VX5P4Z9-3EQUK . Kwa msaada mwingine piga 0715130212. Wengine mkita ntawauzia misimbazi miwili tu:D:D
 
Ukiamua unanunua tu, mimi serikali ilikuwa inanilipia 40% na najilipia iliobaki, na nyumban walikuwa hawahusiki na iyo 60% iliobaki, niliweza kununua laptop ya tsh 460000/= kwa boom ilo ilo, sifa za mi sub woofer, pasi, majagi ya umeme yote nilikuwa nayo, zaidi sana nilipofika mwaka wa pili nikafungua salon ya kiume nje ya chuo kwa boom iloilo na kufika mwaka wa tatu, nikabadili laptop nikanunua ya lak 7 maana salon kama zao la boom ilikuwa ikifanya vema zaidi.

Hii thread ni ya muda kidogo, ila nimeiona hii post nikaona niandike chochote.

Mkuu nikuombe utupe ufafanuzi zaidi, maswali machache tu:-
  1. 60% ya ada ilikuwa shilingi ngapi?
  2. Boom ulikuwa unapewa shilingi ngapi?
  3. Ulikuwa unakaa hostel au nyumbani?
  4. Bei za vyakula zilikuwa ni wastani wa shilingi ngapi?
Anza na hayo.
 
Labda sana unataka kujua nini? Specifically
 
Kwa wengi boom ni mtaji wa biashara wakiwa wanasoma. Kuna kijana alipanga chumba na kwenda kuchukua mchele mikoani na Kuwapitishia mama ntilie, alileta kijana kutoka kijijini kwa shughuli hiyo.
 
Back
Top Bottom