PostGE2025 Boniface Mwabukusi: Viongozi acheni kudogodesha mauaji mliosababisha!

PostGE2025 Boniface Mwabukusi: Viongozi acheni kudogodesha mauaji mliosababisha!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
11,797
Reaction score
18,037
Viongozi wajiepushe na Kauli za Kudogodesha mauwaji waliyoyasababisha kwa kutokuwajibika kwao. Walipuuza Mazungumzo na kudhihaki kila jitihada ya Mashauriano.

Watu waliwaona na kutambua Maiti za ndugu zao kwenye picha na mitandao ya kijamii wakiwa wameuawa wana kwenda Mochwari miili hamna bado wanamajonzi hawaoni Miili ya ndugu zao huku mara viongozi waseme hakuna aliyekufa ,mara hata Polisi wameuawa....mara walikuwa wakiongea kiingereza ilimradi kuvurugana ...Je ni kwamba tuna viongozi wa Vitu badala ya Viongozi wa Watu?

Kinachonishangaza ni ujasiri wa baadhi ya Viongozi wasio na Utu kuzunguka Mikoani na kutoa kauli za kinyama na kudharau uchungu, Hisia na Machozi ya Wananchi ambao wengi waliuawa majumbani mwao.

Na pale wanapofumbua kinywa kuzungumza wanasikitishwa na uharibifu wa boda boda, vituo vya mafuta nk na siyo Maisha yaliyopotea...huku huyu vituo mia kadhaa huyu tisini na kadhaa yule thelathini na kadhaa...

Nadhani Bodaboda wamejumlisha na zile walizozichoma wao baada ya kuwarubuni wale vijana wa pale Ipinda Wilayani Kyela? Kwamba njooni muwekewe mafuta halafu zikapigwa kiberiti?

Sasa wanapuuza hisia ,Majonzi na Maumivu ya Wafiwa wala hawajishughulishi na shida za Majeruhi lakini katika hali ya kustaajabisha na inayodhihirisha hila katika wito wa maridhiano, wanaita Maridhiano? Unazungumza kuridhiana baina ya nani na nani? Kwa ajili gani? Ili iweje?

Hapa kilichopo ni wananchi kutokuridhika na mfumo wa demokrasia, utawala, uwajibikaji na ulegevu wa vyombo vya maamuzi. Hayo Maridhiano yanakuwaje? Au ndiyo kuzungumza tu ilimradi? Maridhiano ni pale kunapokuwa na pande mbili Kisiasa? Je vipi si vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi viliukubali kuwa ni huru na haki? Kabla ya vingine kubadilisha gia angani?

Je vipi Mdude Mpaluka Nyagali, Humphrey Polepole, Soka na wenzake na Mzee Alli Kibao watawasilishwaje kwenye hayo maridhiano?

Haki, ukweli na Uwajibikaji ndiyo suluhisho. Na huwezi kuzungumza kwa ujanja ujanja.
Waliahirisha Agenda 1992, wakaahirisha 1995 wakiahidi 2000 wakaahirisha 2005 wakaahirisha 2010 na kuiacha Zanzibar ikapitisha Katiba yake iliyofuta kabisa uwezekano wa kilichoitwa serikali mbili kwenda Moja sasa ni wakati wa Serikali ya Tanganyika nayo kurejeshwa kama ilivyopendekezwa na Nyalali, Kisanga na Tume ya Warioba Mwaka 2014 wakaunda mpaka Bunge la Katiba kwa hila wakamuondoa Mzee Warioba na Timu yake wakauteka Mjadala na kuubemenda na kuuwa mchakato wa Katiba .

Hatutakiwi kuburutana lazima kila jambo liwekwe mezani na ratiba ya Utekelezaji iwe bayana halafu tuheshimiane. Kila mmoja aliona uovu uliofanywa na Askari dhidi ya Raia. Ni laana na kufuru (Abomination) kuufumbia macho.

Haki, Ukweli na Uwajibikaji ndiyo hupelekea Suluhisho la kudumu na la Kweli. Ukiona Mtu anazungumzia Maridhiano katika mukhtadha wa changamoto hii jua hajui chochote wala hajui aina ya changamoto iliyopo.

BAK MWABUKUSI.
 
Screenshot_20251119-103538~2.png
 
Back
Top Bottom