Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,691
Wakuu,
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Boniface Jacob maarufu kama "Boni Yai" akiwa Kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Chadema Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ameeleza kuwa Chama chake kinatambua mchango mkubwa wa Aliyekuwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, akimuomba asikae mbali na Chama hicho kutokana na kuhitajika kwake.
Jacob amesisitiza wajibu wa kuendelea kumtumia Mbowe na Wastaafu wengine wa Chama hicho katika ushauri, usuluhishi wa migogoro ndani ya Chama, akisema Wanachama na wapenzi wa Chadema wanawajibika kuwalinda na kuwatunza wastaafu hao.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Tuna wajibu mkubwa wa kuwalinda na kuwaheshimu Wazee waliomaliza utumishi wao. Tuna kila sababu ya kujivunia utumishi wa Mbowe ndani ya Chama hiki na tunamwambia asiwe mnyonge sisi vijana tuko nae na tunathamini kazi yake na asikae pembeni kwani bado tunamuhitaji." Amesema Kiongozi huyo.