PreGE2025 Boni Yai: Mbowe asikae pembeni kwani bado tunamuhitaji

PreGE2025 Boni Yai: Mbowe asikae pembeni kwani bado tunamuhitaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu,

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Boniface Jacob maarufu kama "Boni Yai" akiwa Kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Chadema Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ameeleza kuwa Chama chake kinatambua mchango mkubwa wa Aliyekuwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, akimuomba asikae mbali na Chama hicho kutokana na kuhitajika kwake.

Jacob amesisitiza wajibu wa kuendelea kumtumia Mbowe na Wastaafu wengine wa Chama hicho katika ushauri, usuluhishi wa migogoro ndani ya Chama, akisema Wanachama na wapenzi wa Chadema wanawajibika kuwalinda na kuwatunza wastaafu hao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Tuna wajibu mkubwa wa kuwalinda na kuwaheshimu Wazee waliomaliza utumishi wao. Tuna kila sababu ya kujivunia utumishi wa Mbowe ndani ya Chama hiki na tunamwambia asiwe mnyonge sisi vijana tuko nae na tunathamini kazi yake na asikae pembeni kwani bado tunamuhitaji."
Amesema Kiongozi huyo.

CHADEMA ina watu wanajua kuongea kwa kweli! Halafu takataka kama Kigaila eti inasema vichwa vimeondoka CHADEMA yamebaki makapi?
 
Mtanyooka awamu hii ,awakaushie hivyo hivyo muozee jela
Humuoni boss wako alivyokosa raha kwa matusi anayotukanwa?
Hana heshima mbele ya wananchi wa kawaida kwa mauaji na utekaji anaofanya ; nyie chawa hela anazotuibia na kuwahonga zimewafanya vilema wa kufikiri!
Mwambieni ajibu hoja za Gwajima kuhusu kuhusika kwake na utekaji na mauaji ya wananchi : msije shangaa siku moja akajikuta yuko Hague!
 
Ametukanwa na nani zaidi ya Wakenya baada ya kuwatia adabu?

Wananchi wa kawaida wa wapi hap ambao hawamuheshimu Rais au wanamtukana? Kina Mdude au? 😂😂
 
Ametukanwa na nani zaidi ya Wakenya baada ya kuwatia adabu?

Wananchi wa kawaida wa wapi hap ambao hawamuheshimu Rais au wanamtukana? Kina Mdude au? 😂😂
Amejibu hoja za Gwajima? Amejibu hoja za vijana wa Kenya kuwa yeye ni mwizi Ndio maana wananchi wanateseka na maisha kutokana na Ufisadi wake?
Angalia clip za mkutano wao uone wangapi wanamshangilia; utaona ni wachache sana na hao wanaomshangilia ni wale Mashangingi wa kutoka Mchambawima huko Zenj!!
Samia hana mvuto kwa wana Tanganyika analazimisha tu!
 
Na Mbowe hawezi kuwa mpumbavu,hao kenge walishindwa kufanya Sasa za ustaarabu ila kumdhalilisha Mbowe.

Sasa ni wakati wao kupigania chama chao kama walivyotaka .

Kwenye Kampeni zote za Mbowe sehemu pekee aliyotoa Lugha mbaya ni kusema alimfadhili Lisu gari,nyumba hivyo ila hajawahi tukana mtu.

Mbowe endelea Kukaa kimya kuwa busy na mambo Yako.

Watu wote wenye Nguvu Huwa ni WA kimya the likes of Samia huwezi msikia anaropoka huko,mtu roporopo kwanza haaminiki hata Mimi binafsi Huwa nawakwepa.
Freeman Aikaeli Mbowe asiendelee kukaa kimya. Arudi kwenye ulingo wa siasa. Wakati ndiyo huu. Ajitokeze kupambania haki. Haki huinua Taifa. Kumbuka. UCHAGUZI wa mwaka huu tunapaswa ufanyike Kwa haki. Sasa FAM ana sababu Gani kujitenga na Chadema? Kama aliwahi kusema amepigania Chadema Kwa jasho na damu. Je jasho na damu yake ipotee Bure?. Popote alipo FAM amka baba.
 
Haki gani?
 
Back
Top Bottom