Bongo star search ni nini!?

utiyansanga

JF-Expert Member
May 19, 2010
213
7
Huwa nalazimika kufuatili matangazo ya Bongo Star search tangu yaanzishwe si kwa sababu ya ubora wake lakini kutokana nayale ambayo huwa nayashuhudia na pengine mkumbo ...wa familia.!Kama ni kuvuta mashabiki basi waandaji wamekula bingo.Sina uhakika neno bongo hapa linamaanisha nin....Labda Tanzania!?
Kwa wale ambao wanajua mziki na wanaupenda ,shindano hili huwa linawaacha hoi, kuanzia kwa majaji na washiriki wake pamoja na washabiki wao.Hebu fikiria jaji Master T mwaka jana alikuwa anamponda kijana Paschal kuwa hajui kuimba .Kwakweli niliogopa ,kama produza anashindwa kutambua kipaji cha mtu watu wengine itakuwaje ,nashukuru mungu baadaya alitubu makosa yake.Chukua mfano wa mwaka huu je ni kweli Mariam aliwazidi wenzake kwalipi !alichowasidi wenzake ni katika kuimba taarabu na si muziki!
Pengine maamuzi kama hay ndiyo yaliwapoteza vjana mahiri kama Rogers!
Ni lazima waandaji wabadilike ilikuwa kuwavuta watu wanaojua kuimba washiriki la sivyo watu wenye uwezo mkubwa hataingia!
Pengine waandaji wangeweka wazi wanatafuta stars ktk aina gani ya muziki ni huu wa bongomfleva au ni muziki kwa ujumla?
Pengine na vigezo vya kuchagua majaji viwe wazi,JE MAPRODUZA AU WATANGAZAJI wanautaalamu gani!
Kama mojawapo wa majaji wa shindano hili ni wasomaji wa JF wanunue dvd MOJA YA DINI ILIYOIMBWA n TM MUSIC waone vipaji humo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom