Bongo star search 2015

Wapenda muziki wote nadhani mtakubaliana nami kuwa "BSS" mfumo wake unahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa ili dhana ya kuwainua waimbaji chipukizi ifanikiwe.Kwasasa BSS inatafuta sauti tu na kisha kutafuta mwimbaji anayeweza kuiga kuimba wimbo wa mwimbaji yoyote.

Mie nilitegemea BSS ingekuwa ina tafuta vijana wenye uwezo wa kuimba kisha kupitia watalaamu wa muziki wa BSS wakawafundisha mbinu mbali mbali za muziki.Pia Nilitegemea BSS ilipaswa kuwa na majaji wa kutoka maeneo mbalimbali wenye ujuzi wa muziki na pia wanamziki wapimwe kwa kutunga nyimbo zao badala ya nyimbo za watu wengine.Ni imani yangu watalaam wa Muziki watasaidia kuiboresha mada hii ili bingwa wa BSS asipatikani kama alivyopatikana Kayumba na Jumanne Iddi na wababa.
 
BSS ina wenyewe, si mali ya watanzania. Hivyo, wanaweza kufanya watakalo ilimuradi malengo yao ya kuishi hapa mjini yanatimia.

Kama TBC, chombo cha wananchi, kinatumia kodi ya wazalendo inaendeshwa kama tawi la propaganda la CCM, sembuse BSS?
 
Kanyweni chai na huyo Fenabo...
Kayumba oyeeeee,ndio keshashinda,hamtaki andamaneni.
Kila shindano halikosi manung'uniko,hata season ya Walter kulikuwa na manung'uniko wengine walitaka Salma ashinde.
Hata hivyo kutokushinda sio kwamba hajui muziki,afanye yake Watanzania watamsikia.
Kwani Ali Kiba,Diamond,Belle 9 n.k walipitia shindano gani?
 
mnafikiri kuorganise zile mambo ni kama kumvua demu wako kyupi, fanya wewe uone, kayumba deserved it, period!
 
Hata angeshinda FONABO bado watu wengine wangelalamika tu,kama unaamini KAYUMBA alistahili kuingia top 5 basi hakuna haja ya kubisha ushindi wake kwani yeyote kati ya wa5 wale alistahili kuwa mshindi kutegemea na perfomance ya siku hiyo na BAHATI/NYOTA.show za bongo anayeshangiliwa sana ndo kapaform poa.Mshindi wangu alikuwa FRIDA from the first day.
 
Mbona mnalia lia ? FONABO mwanamuziki ukimsikiliza unapata kitu original ila Kayumba ni blaah blah blah tu nampa mwaka mmoja atafuata njia za akina J4.
 
Hivi mnaangalia wapi live jamani wapendwa maana wengine mpaka recorded jumapili sa3 usiku.
 

Lakini unaonaje mdhamini kuweka mtu wake kwenye shindano.....?
 
Lakini unaonaje mdhamini kuweka mtu wake kwenye shindano.....?

Kwani wadhamini ndio waliompa ushindi Kayumba au ni Watanzania?
Kayumba alikuwa na juhudi tangu siku ya kwanza,angekuwa hajitumi hata mimi nisingemkubali.
Yote kwa yote Kayumba ana nyota,watu wengi sana walikuwa wanamkubali mimi mwenyewe nikiwa mmojawapo,haya ya mdhamini hayana mashiko as long as kijana alikuwa na kipaji na bidii.
 
Kwa mtu aliyefwatilia BSS since kipindi cha auditions hawezi kulalamika Kayumba kushinda..Sikatati kuwa Fonabo anajua..Ila mshindi ni mmoja na Kayumba alistahili
 
Mbona mnalia lia ? FONABO mwanamuziki ukimsikiliza unapata kitu original ila Kayumba ni blaah blah blah tu nampa mwaka mmoja atafuata njia za akina J4.

Teh teh..Naona mmeshaanza kujivika umungu mtu..
 
Atafanya vizuri kwa sababu mabosi zake ni mabosi Wa yamoto na hao ndio miongoni mwa wadhamini Wa hiyo BSS.Kwa hiyo ataendelea kubebwabwa na kubebeka lakini hatokuwa na uwezo kama Wa Fonabo Wa kutoka kwa mama.

Wasanii wenye uwezo tz wako kibao sana..Wengine hata hawajulikani..Na wengine wenye blah blah hizo unazozisema wanatoboa hadi kesho..Mziki sio kuwa na uwezo tu mkuu..
 
Teh jamani nifah na daddy Kaboom mnanipa raha mjue. Ukweli utabaki tu kuwa ukweli, kayumba Mungu amempa kibali mbele za watu wengi. Sisi home tangu day one kayumba ameimba msaliti ya king bella tulianza kuwa fans wake na Kayumba ana fans wengi mnoooo. Whether anafahamiana na kina fella or not, mwaka huu ulikuwa wake. Afu kayumba ni alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo. Kwa hiyo watu wajiandae tu kisaikolojia kwamba coz that lil boy is here to stay. Ok Byeeee
 
Last edited by a moderator:
Wasanii wenye uwezo tz wako kibao sana..Wengine hata hawajulikani..Na wengine wenye blah blah hizo unazozisema wanatoboa hadi kesho..Mziki sio kuwa na uwezo tu mkuu..

Unaniumiza roho hapo daddy ukimwacha bella hakuna msanii nayempenda na anayejua kama barnaba boy, sijui nyota ndo tatizo
 

Mi nilichofanya ni kukariri tu majina ya wanaosema kayumba hastahili,amependelewa,ohhhh sijui soon atapotea..Ntawatafuta..Muda utatwambia
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…