Bongo nyuyoki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo nyuyoki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yo Yo, Jan 12, 2009.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mambo ya Bongo sasa hivi kiboko; kuna mashopingi moli kama ya mtoni, Maubungo Plaza, Mayfair Plaza na maplaza mengine mengi tuuu! Maapatimenti, mariili esteti broka, mabangaloo, na maskai skrepa! halafu mabarabara ya kimtoni na madaraja kama lile la Kibiti watasha wenyewe wanabloo! Na neshino stediumu mpya ikiisha litakuwa hamna tena Afrika nzima!

  Mademu siku hizi wanang'aaaa! Kuna maMiss kata, miss tarafa, miss wilaya, miss mkoa, miss Tanzania, mpaka miss yunivasi! Mafasheni shoo, madizaina, na mamodozi! Maselebriti wa vipaji vya kitaaluma, kisanii, kimichezo, kisiasa, ua kwa majina ya ukoo. Kuna Matamasha, mabonanza, na makonseti hatari tupu!

  Redio stesheni za kumwaga siyo kama wakati ule idhaa tatu tu; taifa, biashara na eksteno sevisi iliyokuwa inafunguliwa kwa masaa maalumu na kipindi kimoja tu cha salamu siku za Jumapili mchana! Na tivii chaneli kibao siyo kama wakati tivii Zanzibar minara michache mitaa ya Upanga na Ostabei tena usalama wa taifa wasiione, ukionekana mnara utakuwa umeenda kinyume na Azimio la Arusha kwa kuwa bepari au kabaila kwa sababu ya kumiliki tivii! Eee bwana na magari mengine hata ughaibuni hamna sijui mabaluni, maviieksi, Mamuso, mahama, mafoo whili draivu, maleksuzi, yaani wee acha tu!

  Elimu nayo sasa imepanda kuna mainteneshino skuli kuanzia nasari mpaka hai skuli na yunivesti siyo UDSM na SUA tu kuna mayunivesti kibao sijui Nyegezi, Sijui Mikocheni, Makumira, Tumaini, na jingine la nguvu linaangushwa Dodoma unaambiwa hilo yunivesti sijui litakuwa linachukuwa wanafunzi ngapi sijui kwa inteki, yaani hilo yunivesti litakuwa kama Kembriji, Oksfodi, au Havadi! Eee bwana eee!

  Siku hizi simu siyo big dili! Unaambiwa nilikuwa Nanjumbu, Mtwara vijijini ndani ndani huko nikakikuta kibibi kizeeee utafikiri hakikuwahi kuwa kitoto kichanga! Unajua nini? Kilikuwa na kimobiteli cha Nokia hizi ndogo ndogo kinaongea na sijui na nani? Mwenyewe nilizimia! Enzi za TTCL ilikuwa uende kibanda cha simu tena ukikikuta nzima una bahati sivyo sumni yako inaliwa na simu haifanyi kazi. Ua ukitumia simu za nyumbani siyo laini kuingiliana au unaweza kujikuta unasikiliza simu tano kwa wakati mmoja! Siku hizi hela yako tu bazi, seliteli, voda, mobiteli lakini mimi naiona seliteli ndiyo kiboko lakini voda nao moto! Jamaa wa posta kweli walikuwa wanatuzingua barua unaituma Kibaha toka Dar inachukuwa mwezi! Siku hizi teksi meseji au ukiona namna gani vipi unanda intaneti unatuma imeli!

  Usafiri siku hizi siyo sijui ATC, UDA, sijui KAMATA, nyooo! Siku hizi mtu unataka kwenda Mwanza unapaki begi lako unaenda eyapoti unachagua bomba gani udandie Prisisheni, Igo, eyaTanzania au bomba lolote tu! Mabasi siku hizi kuna malakshari yana maeyahostesi kama wa kwenye ndege! Mabasi yana vyoo, tivii, slipingi kochi yaani kama mtoni tu!

  Mimi ughaibuni wala sikuzimii. Jamaa wanaenda ughaibuni nasikia wakifika huko wanabeba maboksi na kukosha vizee. Siulimuona nanihii, alipoondoka kwenda ughaibuni alikuwa na mimba hiyoo mashavu utafikiri anapuliza moto! Karudi mimba imekatika, kakondaa utafikiri Msudani ya Kusini miguu kama mikono ya mawani, yaani utamuonea huruma! Unajua Bongo michoro yako tu! Misheni kibao inategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyopanga kete zako. Kuna majamaa hapa Bongo wanaishi kama mtoni asubuhi wanapata brekifasti ya masoseji, hambagi, juisi na chai ya maziwa matupu au uji uliopikwa na unga wa keki ukatiwa na mapande ya siagi na krimu! Lanchi chikeni chipsi na kuku, dina steki hevi grili pateto au raisi! Yaani wee acha tu, Bongo New York.

  Na manjagu wanakula mavitu hevi siyo kama enzi za Mahita tangu kaja Said Mwema manjagu wanatia vitu vya kimtoni maksi sijui mabelti, yaani we acha tu!
   
 2. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuelewa ujumbe wa mwandishi kama alivyoandika, au kwa kutafakari zaidi ukawa na tafsiri nyingine ya picha iliyowekwa katika ujumbe huo. Kazi kwenu!
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yo yo you are a very interesting character....from what I see from your posts. I totally agree with you on this one, if you have a good job in Tanzania, it's the place to be.... too bad only a few know that and have such priviledges
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Yo Yo can you put this story in English? I get lost somewhere....
   
 5. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  YOYO,majority of tanzanians,are on minimum wage,naomba unipe breakdown at least roughly,BASKET of goods and services,a minimum wage can buy.BY the way better late then never,HAPPY NEW YEAR TO THE JF franternity and all the best.could not wish you earlier cause me was in a keyboard free zone,hopefully me did not miss much.ONCE again happy new year to you all
   
 6. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima wana JF

  Mambo aliyopyasema YoYo ni kweli kwa baadhi ya wakazi wa Dar pengine na Arusha, Mwanza na labda Mbeya. Haya ''maendeleo'' yako mijini kwa wachache wenye pesa za kutosha. Nina uhakika watu walio nje kidogo tu ya Dar. hawana matumizi ya hayo ''maendeleo''. Vijijini kuna shida sana, amini usiamini wanakijiji wana hali mbaya leo kuliko waliyokuwa nayo miaka kumi iliyopita. Hilo suala linahitaji kuangaliwa na sisi wote, siyo wanasiasa peke yao. Baadhi ya hizo investment labda zingewekezwa vijijini ( kwa mfano ukianzisha shamba kubwa kijijini kwako waweza kuajiri watu na kuwapatia kipato kidogo, unaweza kuanzisha kiwanda cha kuprocess whatever crops that are produced there etc, this used to work well wakati wa cooperatives)


  Umezungumzia pia mabarabara, tatizo ya hizo barabara ni kuwa hazikujengwa vizuri ukiangalia upande wa kupunguza msongamano wa magari barabarani. Nyingi ziko karibu na makazi ya watu hivyo ukitoka tu nyumbani kwako tayari upo barabarani na kusababisha traffic friction. Zingetengenezwa ramps kupunguza aina hiyo ya msongamano. Ninafahamu pia ugumu wa hilo maana pengine hizo nyumba na hata maofisi yalikuwepo kabla ya hizo barabara etc. Lakini faida moja ya kuanza shughuli za maendeleo kwa kuchelewa ni kuwa na mwanya wa kuangalia wenzio walifanya nini, tuliipoteza hii opportunity mara baada ya kupata uhuru. ( najua tulikuwa masikini, but this had to be said.)

  Kweli nyumbani ni kutamu, lakini tujitahidi kupunguza bugudha za maisha ambazo tunaweza sisi wenyewe tukachangia, kama hizo road planning etc.
   
 7. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  umepotea wapi?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 12, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Vipi, bongo kuna Nimani Makus? Au Nodistiromu?
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  maeveresingi mazaga zaga bwena yapo ni mshiko wako tu......
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jan 12, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Oh yeah.....kwa hiyo Makwiznos, Papa Joniz, Apobiizi, redi lobusta yote yapo?
   
 12. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Well,Rome was not built in a day.
  Its foundation not on the pride of useless bon vivants
  Nor on the dreams of faineant micawbers.
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kumechoka kivipi?
   
 14. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  YoYo, I can bet kuwa hii story hujaiandika wewe, kuna mahali umeikota, naomba tu utuwekee source pse! Very fun.
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Source kumbe ndio shida yako?
  hii hapa
   
 16. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Mmh? kweli utamu wa kujing'ata hauishi wallah!
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,783
  Likes Received: 83,141
  Trophy Points: 280

  Mbona umewasahau mafisadi wa nchi kuanzia kina Mkapa, Majiyatanga, Mkono, Pesakibao za ufisadi bin Mramba, Mzee wa Vjisenti na Virada na wengi wengineo, au hao hawako Bongo!?
   
 18. Kaka Mkubwa

  Kaka Mkubwa Senior Member

  #18
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkubwa naona uko fiti sana kwenye mambo ya misosi.
  labda niongeze msisitizo kwenye mambo ya vivazi vya kina dada na mapozi ya kufa mtu yaani ya kimtonimtoni.
   
Loading...