BONGO MOVIE waja na kampeni ya uzalendo kwanza baada ya kimya kirefu

likandambwasada

JF-Expert Member
May 27, 2015
5,402
6,072
Umoja wa 'waigizaji' wa bongo maarufu kama bongo movie wameanzisha kampeni ya uzalendo kwanza ikiwa na lengo la kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika uzalendo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa umoja huo steve nyerere, amedai kuwa kampeni hiyo siyo ya kisiasa na inalenga kuhamasisha uzalendo.

Itakumbukwa kuwa bongo movie walikuwa kimya muda mrefu tangu kampeni yao ya mwisho ya MAMA ONGEA NA MWANAO katika kampeni za uchaguzi ambapo waliipigia kampeni CCM.

Source: Tbc1 habari.
 
Wanaunga mkono uzalendo wa mtu ambaye hajawahi kuwa mzalendo? Magufuli lini ameanza kuwa mzalendo? Mzalendo anatoaje rushwa kwa wabunge wa chama chake? Mzalendo anakuwa na mshahara wa zaidi ya milioni 400 kwa mwaka na anakwepa kulipa kodi na wakati huo huo kwenda kuwakamua kodi wale wenye mshahara wa 500K? Mzalendo anachotaje pesa chungu nzima bila idhini ya Bunge?

Mwasisi wa MAMA ONGEA NA MWANAO wema sepetu anashinda Kisutu anapimwa MKOJO siku hizi.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Ukiwa muigizaji siku zote unaishi kwa kuigiza igiza,Hao bongomovie walishindwa kufanya sanaa wakajiingiza kwny siasa za kumpigia kampeni fisiemu sasa hivi wanatuijia na filamu lao la uzalendo!! Anyway ngoja tusubiri tuone BEHIND THE SCENE YA UZALENDO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaunga mkono uzalendo wa mtu ambaye hajawahi kuwa mzalendo? Magufuli lini ameanza kuwa mzalendo? Mzalendo anatoaje rushwa kwa wabunge wa chama chake? Mzalendo anakuwa na mshahara wa zaidi ya milioni 400 kwa mwaka na anakwepa kulipa kodi na wakati huo huo kwenda kuwakamua kodi wale wenye mshahara wa 500K? Mzalendo anachotaje pesa chungu nzima bila idhini ya Bunge?
Bongo movie wanajulikana ni watu wa namna gani, hivyo ni wa kupuuzwa tu, hawajui hata uzalendo ni nini.
 
Bwana yule anatapatapa sasa baada ya kuona umaarufu wake unazidi kuanguka huku akiwa hana chochote cha kuonyesha katika miaka miwili. Nchi haijanyooka, ajira hakuna, nyongeza ya mishahara hakuna, Watanzania wana hofu kubwa kutokana na uhuru wa habari nchini kuminywa. bomoa bomoa, kamata kamata ya wapinzani vyote hivi vinaongeza hofu kubwa nchini. Usiri mkubwa wa Serikali kutaka kuficha hata ndege inapokamatwa etc. Kama alivyojisemea Ulimwengu, tumerudi nyuma miaka 40 tangu awamu hii iingie madarakani.

Bongo movie wanajulikana ni watu wa namna gani, hivyo ni wa kupuuzwa tu, hawajui kwamba uzalendo ni nini.
 
Back
Top Bottom