che wa Tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2011
- 277
- 71
Wadau nadhani hawa wadau wa sanaa wa Bongo Movie wana cha kujifunza angalau kidogo kutokana na baadhi ya hizi filamu ambazo kwa kiasi kikubwa zimerandana dhahiri na bayana na maisha halisi ya ombwe kubwa la Waafrika.
Hizi filamu nadhani zipo directed na madirector wa hapa hapa afrika ambao hawapo money oriented zaidi kama hawa wa part 2 za kibongo na kuigiza kwingiiiiii maisha ya kibeyonce.
Kwangu ni filamu ambazo zimebeba maudhui zaidi ya maisha ya mwafrika ya kila siku na mandhari yanayowazunguka zaidi waafrika walio wengi. Bongo Movie nadhani wanapaswa wajifunze kutokana na kazi za wenzetu kama hizi na nyingine kama Yellow Card n.k