Bongo Movie mnashida gani?

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
Hawa jamaa miaka kama 12 sijawahi waangalia siku za Hivi karibuni nilitumiwa picha na wife akisema hili ni jini la bongo movie. Nikajua ni utani wa bibie.

Basi Kwa siku za Hivi karibuni nikasema Wacha Nami nishuhudie vioja Hivi vya bongo movie asee niliishia kulala tu hamna ujuzi wowote uliongezeka zaidi ya kupoteana na kupoteza mvuto kabisa.

Ile tamthiliya sikuijua hata jina japo waingizaji au waandaji wote ni wazoefu mle lkn kinachofanyika hakieleweki.

Zamani kwenye miaka ya 2007.... Ray kigos na Steve kanumba walikuwa wanafanya vizuri kweli.

Tamthiliya kama
More than pain
White maria
Big daddy
Uncle JJ
Magic house
Oprah
Dar to Lagos
Nk. Hizi Hadi waleo Huwa najikumbushia hakika huyu jamaa alikuwa anajua haswaa.

Pamoja na kukaa muda mrefu kwenye game walioachwa haajajifunza kitu.

Hii ndio picha niliyo tumiwa na wife akidai ni jini aliona kwenye tamthiliya kwenye bongo movie.

FB_IMG_1701626170371_1.jpg
 
Ila bwana hayo yote sawa..
Ila kuna watu wanajitahidi sana sasa hivi...

Shout out to LAMATA na JIMMY wana tamthilia Tamu sana .....Jua kali ,Huba ,Kapuni na nyingine nyingi
Mkuu naweza kukubali maana na muda mrefu sana siangalii siku hizi wife akawa anachelewa sana kuja kulala ikabidi nikaangilie Nami hakika sikufanikiwa hata dk 10 nikaona hamna kipya kabisa ukilinganisha na movie za kipnd Cha nyuma
 
Nilichokiandika ni kuwa kwasasa kazi zimejawa na utoto mwingi hna hakuna ubunifu Kama zamani. Nimetolea mfano wa hiyo kazi inaitwa KUBWA KULIKO na kazi nyingine za akina mkojani yaani ni utoto tu ndani yake.
Movie za kina mkojani ni kwa ajiili ya watoto, ukitaka movie check DSTV na AzamTv, kidogo wanajitahidi
 
Bongo Movie. Imekuwa kama ka closed society fulani. Hakuna talents mpya. Wanaangalia majina ya watu wale wale. Wanaingizwa watu kwa matakwa nje ya vipaji halisi. Unamwona MC maarufu naye mwigizaji lakini ni dhahiri hawezi.
Vipaji vipo mitaani kwa Director producer na Director serious.
 
Back
Top Bottom