Bongo movie aibu tena

Bongo movies mara ya mwisho niliangalia 2007
 
Kama bongo move wanataka kukamata soko waangalie zaidi mila na desturi za kitanzania,waache kuiga tamaduni za nje ili kujitofautisha,tamaduni zetu zinaweza kukamata soko(create own style)
 
Kama bongo move wanataka kukamata soko waangalie zaidi mila na desturi za kitanzania,waache kuiga tamaduni za nje ili kujitofautisha,tamaduni zetu zinaweza kukamata soko(create own style)
Mkuu hili ni janga,hawa jamaa wanakera sana kwenye maadili.
Na wapumbavu wengine wanakuambia utandawazi,wakati wenzetu ambao utandawazi upo miaka 100 iliyopita na wanaendelea na mila zao kama kawaida na wanateka soko la Dunia kwenye Sanaa.

Leo hii wasanii wakubwa kama kina JB Richie nao wameingia kwenye upuuzi ule,aiseee,aibu saana
Wakenya na kiswahili chao cha tabu wapo vizuri saana.
Hili ni kundi tu la wauza sura,ila ukweli Watanzania ni rahisi saana kuwateka kwenye sanaa ila ni ngum sana kuwarudishwa wakikupotezea.
Sasa hivi filam za nje zilivyo na maadilia mazuri,watu wengi sana wanaangalia filam za mbele huko,Korea,Ufilipino huko nk.Yaani unapata mesej ya maana kwenye mchezo,hata mtoto mdogo asiejua lugha anakuambia mchezo woote na unahisi kabisaa huyu mtoto ana filling za uhalisia wa mchezo na anajifunza kitu.
Na ukifuatilia saana,visa vinakuwa vile vile,ila characters ndio wanakuwa tofauti.
 
Kuna wakti unaweza ukaleta uzi humu jamvini ukaonekana ni kituko au hujui chochote ni vyema kabla hujaaweka andiko ulitathimini kwa kina ili usindike kinafiki au kishabiki, hizo cd za nje zimechangia nn kwenye uchumi wa taifa lako? kwa kiasi gani kazi za wasanii wetu zinachezwa au kuuzwa nje ya nchi kama zao kwetu?fikiria umekesha studio au location umetoa hela kibao kufanikisha kazi yako harafu mjinga mjinga fulani hv yuko sebuleni kwake na machine yake ya kudurufu anatandika copy zako tu kirahisi rahisi tu utazani zake, jifunze kuheshimu kazi za wengine kumb, hapo ndipo wanapopatia mkate wa sku, tufanye kazi vya bure vimeisha.
 
Pole zenu mnaonunua movies K/Koo..
Wenzenu nikiwemo mimi napakua series zangu za kikorea mwenyewe.
Hivyo hilo suala halitoniathiri hata chembe.
Na mimi haliniathiri hata kidogo,waandamane hadi kwa magu
 
B

Kamani kweli basi hawa jamaa wa Bongo movie ni wajinga, filamu kwanza wanaiga maadili ya Kinaigeria. Bilakushindanishwa na wasanii wa nje ya nchi mbona watatuletea vituko hapa.
 
Ndugu yangu mimi si mnafiki na sijasema kiupendeleo ila nawakosoa sababu wanakosea na ndio maana mwisho wa thread yangu nimesema wazi kuwa suala ambalo ndugu zetu wanapaswa kufanya na kulihangaikia ni juu ya kupinga piracy ya kazi zao, maana inajulikana wazi kuwa wanaibiwa mno!

Jambo wanalotakiwa kufanya ni hilo na si kuanza kupinga kazi za wenzao tusizione, tuone zao wakati zao hazina kiwango Ikumbukwe kuwa hii ni Burudani kama Muziki na si kama sukari za ndani ya nchi na nje.
 
Mimi nionavo Serikali kumfungia mtu mwenye duka na bila ya mikakati madhubuti ya kuzuia uingiaji ni uonevu.

Mikakati Ianze kwenye chanzo kwanza, kodi munazitaka zikishuka bandarini na Airpot mnakula hela lakini wengine wasipate. Hebu tuangalie hizi bodaboda zinazopigwa marufuku, kwanini serikali isiseme kwamba sasa Tunazuia uingiaji wa bodaboda hata kwa muda ili mpk zipungue sokoni ndio tutafikiria tena utaratibu huu.

Lakini kodi ya kuingizia mizigo inatakiwa na serikali ILa wewe usiziuze tuzifanyeje?
 
Hii stori haiko sawa mahali. Kuna mtu amehakiki hii habari atupe data zaidi.
 
Kwakweli kwenye mambo ya starehe wangeacha tu. Mfano huwezi kusema ni marufuku kuonyesha ama kushabikia vilabu vya Ulaya kama Chelsea, Man U, Arsenal et ili tushabikie Simba na Yanga. Au useme tusipende kazi za wasanii wa nje ili tupende za hapa ndani wakati hawa wetu hawana idea bali idea wanaazima toka kazi za wengine. Ni kama kusema tutumie tu huduma za ttcl. Kinachofanywa kwenye sukari ni tofauti na hizo filamu kwani lengo ni kulinda viwanda vyetu kutokana na raw materials zipo na uti wa mgongo ni kilimo. Hivyo viwanda vya ndani sharti vilindwe.
 
Movies za bongo uangaliwa zaidi na wasichana wanaofanya kazi za ndani. Karibu zote zinafanana, na vituko vinavyoonyeshwa humo, ukiangalia utajiuliza kuwa sijui wahusika hawako sawasawa?????, yaani uchawi, vichaa, ugomvi na makelele ndio vinatawala. Yaani, wanajaribu kulazimisha kuchekesha audience ya level ya chini.

Wasanii, madereva wa mabasi, bodaboda, tax, wacheza mipira etc wengi wao hawajasomea taaluma zao. Matokeo ni low performance. "Chema cha jiuza kibaya cha jitembeza"
 
Hakika!
 
Wamefungiwa kwakuwa wameshindwa kufata utaratibu hakuna mtu aliye zuiwa kuingiza movie nje bali unachotakiwa ili ufanye biashara ya kuuza lazima uwe na vibali pia na sticker za TRA
Movie zao siyo nzuri hazina hata uhalisia nani azinunue???? Hata wakifunga tutadownload tuuu

Mamlaka ya kufunga maduka wanayo? Au ndio hearsay tu. Nina wasiwasi na hii thread huenda ikawa ni uzushi tu.

Wafunge hata torrent sites kama wanaweza ***** zao%

Mimi movie za kibongo huwa siangaliagi kabisa manake hazina mvuto hata kidogo movie nzur labda ni siri ya mtungi ndo huwa naifatilia kidogo Ile series imenipa ushawishi kwa mbali.

Nikweli Tanzania haina kiwango cha kuingiza na kuimba so waangalie tu kaz zao zisipate kuibiwa

Move za kibongo sizielewi kabisa Na uwaga siziangalii
 
Nina kasema wamefungia filamu za nje kuingizwa nchini? Kinachotakiwa ni wao kufata utaratibu wa kuuza filamu lazima wapitie TRA na Cosota....
 
mmmmmmh!! TRA wafanye kazi yao ila bila utaratibu itakuwa nuksi tu! halafu waigizaji wa bongo movies waache kuigiza chini ya viwango uwezo wanao ila hawana wataalum wanaojua movie ni nn..ndo maana wote wanaiga kujichubu..kuongea sauti ambazo si zao..kingereza kibovu..maudhui ndo hovyo kabisa aibuuuu...bongo movies zote zifungiwe ili wajue wanaharibu waje upya kivingine twaweza elewa!..
 

Mfano ndogo tu nyimbo ya Mpoto zina mafundisho fulani. Lakini za "Diamond" ?????????? sikumbuki hata kaneno ka maana zaidi ya .... nampigia mwanangu.....
 
Ninacho kulaumu kwenye hii thread ni wewe kupotosha na kusababisha kila mtu anaye changia hii thread kudhani serikali inazuia uingizwaji wa movie za nje kitu ambacho sicho kabisa!

Serikali inacho hitaji ni kufuatwa utaratibu wa uuzwaji wa na sio movie za nje maana hata movie za ndani zisizo na vibali au sticker zimekamatwa..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…