Bongo Life's Vs Ughaibuni (Majuu)

Bongo Life's Vs Ughaibuni (Majuu)

2.wanyumbani hapa wapo juu zaidi
--wa nyumbani wapo juu linapokuja suala la kuwa na kumiliki vitu,wangapi wanaweza kumiliki nyumba ulaya?

Hivyo vijumba navyo unaviita nyumba?

wangapi wanaweza kununua ma-vogue wakiwa ulaya?

Well, ni wangapi Tanzania wanaoweza kumiliki hizo HSEs kwa kutumia riziki halali? Na hata hao wanaozimiliki, iwe kupitia njia halali au haramu, ni asilimia ngapi ya Watanzania? Inafikia hata asilimia 2? Sidhani!

wangapi wanaweza kuwa na biashara,ofisi na makampuni yao wenyewe wakiwa ulaya?

Ni Watanzania wangapi ambao wako Tanzania wanaomiliki biashara, ofisi, na makampuni yao wenyewe? Tuzizungumzie hizo fursa kwa takwimu. Tuanzie na unemployment rate. Kwa Tanzania ni asilimia ngapi?

na hili wabongo wengi wameshaliona ndio maana zile ndoto za majuu siku hizi ni kidogo sana kuliko ilivyokuwa zamani

Lakini...iweje kila mara watu wanatusumbua tuwanunulie vitu huku majuu? Yaani hata manukato watu wanapenda ya huku. Kuna watu wanafanya biashara za kununua manukato na biadhaa zingine za Victoria's Secret, kwa mfano, na kuzituma huko bongo nyoso. Kwa nini unadhani?

ni mtizamo wangu,nakaribisha hoja zenye kujenga

Nami mtazamo wangu ni kwamba Tanzania bado ni nchi ya dhiki sana. Tu wategemezi wa mambo mengi sana. Hata vinywaji baridi vingi bado ni vya kigeni. Hiyo Coca Cola na products zake zingine ni za Kimarekani. Yes, Atlanta, Georgia's very own. Walau Azam wamekuja na cola yao lakini hata wao ni kuiga tu. Hakuna ubunifu hata kidogo.

Bottomline Tanzania opportunities bado sana. Kama mtu hauko well connected na/au kama huna deep pockets kwa kiasikikubwa we ulie tu. Lakini Marekani huhitaji kuwa na jina kubwa. Waweza kuitwa Nyani Ngabu na uka-make it vile vile. Hata usipokuwa milionea, if you work hard enough, if you play by the rules, and if you are disciplined , then you will lead a very decent life.

Halafu, hivi kwa nini huko bongo nyoso watu wanafuatilia sana yatokeayo majuu. Yaani unakuta mtu anajua kinachoendelea Marekani kuliko hata walio Marekani! Watu wanafuatilia TV series utadhani sijui nini. Hivi huko hamna TV series zenu hadi mfuatilie za Marekani na kwingineko?

Na mashauzi ya kujifanya hujui Kiswahili. Mtu akiongea maneno matatu basi ya Kiingereza lazima yawe mawili. Kwa nini iko hivyo?
 
Home kutamu kinachotukimbiza security.nimepona kufa kijingajinga zaidi ya mara tatu.nimekabwa mara nne,nimechomwa chupa tumboni,nimeingiliwa na majambazi mara 3.ajali mara 3 ya mwisho kupona ni mungu tu.nimerogwa hesabu nishasahau,nimeumwamalaria na kuuziwa vidonge fake zaidi ya mara kumi.nimekamatwa na polisi na kubambikiwa kesi zaidi ya mara tano.sasa hapo ntaipenda bongo kwa kipi.mtoa mada anasema wengi tumekimbia kwasababu hatuku-achieve goals(kuwa na kazi,kuoa,kujenga)thats nosense,wengine tuliondoka tukiwa na vyote hivyo lakini bado security hakuna.
Well,i prefer ughaibuni.hamna longolongo,follow the rules and life become smooth and clear.ukizungumzia burden,thats life here. U want to do somethn big go take loan bank.as long as you work.sasa kwa nini usitumie hizo chance km zipo.nyie endeleeni kukaa bongo.maisha ya huko mnayaweza wenyewe.ntakuja km mtalii

Ha ha haaa, kwa haya ndugu lazima uchukie kwenu: uliwezaje kujua kuwa ulirogwa mara kibao?
 
Ah ha, Houston, Texas (This is the way we ball)



Huyo Flip hana akili nzuri halafu hataki kuchagua. Akiona Benz mbili kazipenda anashindwa kuchagua moja anabeba zote mbili.

Hood rich rappers wana vituko sana.

On the topic, the world is my oyster. Tena naangalia uwezekano wa kwenda Andromeda kabisaaa maana wabongo wengine wanazidi kuchonga with their misguided and hopelessly parochial two bit patriotism.

Home is where you make it.

Kulonda kazi ya muziki ugangamaleee.

Eeeh ngangali, dona limeota koti, tatizo noti.
 
Last edited by a moderator:
I hope you are all well wanaJF wa majuu (Nyani Ngabu and the like) of the diaspora. I have noticed how frequently people on the forum discuss the topic of Bongo Vs Ughaibuni and it seems as though people can`t decide which one is best. Of course home is best and we all remember it nostalgically, almost always referring to it fondly; unconsciously editing out the dark bits.

I also found that the recurring subject in this topic is that Tanzanians in the diaspora believe their peers in Tanzania to be doing far better than them because they (Tanzanian peers) have already achieved the life goals of marriage, family, careers et cetera. According to some of them (diaspora), their Tanzanian peers seem to have accomplished all these milestones easily and quickly. Those in ughaibuni often say that they have to work really hard to get from one goal to the next and even after many years of toiling, they feel they can`t match what their peers in Bongo have managed to do in the same amount of time.

What some people in the diaspora forget is that they started out with the double disadvantage of being a foreigner and a person of African descent in a land where such people are a small minority. Although some countries are fair to us than others and our African heritage doesn`t affect how we are perceived, it still takes a long time to be accepted and offered an equal place in their society.

I think that it is highly subjective as to what doing better represents to each one of us and appearances can sometimes be deceiving. Displaying your wealth ostentatiously in a flashy car and living in upmarket LA,NY,LDN, Dar, Mza or Ars might be signs of being financially better off and they might be the only determining factors in deciding this but I have found that showing off all that money is often times a burden.

Life is what you make of it and earthly possessions are transitory, we all pass on to another realm in the end and leave it all behind. We should strive to be wealthy in spirit and good to each other. When we die no one remembers us as being super rich and living in a palace. Our legacy lies in how we treat each other. In Bongo or in Ughaibuni, it shouldn`t matter where we live.

Unfortunately this is a lesson many people on this planet haven't learned yet. They think the meaning of living a good life is having a big house, a fancy car, and lots of expensive toys. The inescapable fact is that when you die, all that shit gets left behind. And those who think they're happy because they have lots of "stuff" are only fooling themselves - they're actually living shallow, empty lives whose sole purpose for existence is the accumulation of more money. Props to you for realizing this, but unfortunately people like us are in the minority
 
samahani mkuu,bongo uliondoka miaka ipi?80's or 90's?

Mwaka jana 2012 mwezi machi na nimezunguka mikoa 20 ya tz, tusidanganyane bongo bado sana msipende kuishi maisha ya maigizo.....hiyo asilimia 1% wanaoishi maisha mazuri haiseidii chochote kama more than 90% ni maskini wa kutupwa wakiugua wanasubiri kudra za mwenyezi Mungu au kukimbila magazeti na redio wachangiwe. Hakuna bima ya afya inayoeleweka au walau hospitali yenye vifaaa. Msijidanganye na vigaru used na nyumba under standard mnazoishi
 
Hivyo vijumba navyo unaviita nyumba?



Well, ni wangapi Tanzania wanaoweza kumiliki hizo HSEs kwa kutumia riziki halali? Na hata hao wanaozimiliki, iwe kupitia njia halali au haramu, ni asilimia ngapi ya Watanzania? Inafikia hata asilimia 2? Sidhani!



Ni Watanzania wangapi ambao wako Tanzania wanaomiliki biashara, ofisi, na makampuni yao wenyewe? Tuzizungumzie hizo fursa kwa takwimu. Tuanzie na unemployment rate. Kwa Tanzania ni asilimia ngapi?



Lakini...iweje kila mara watu wanatusumbua tuwanunulie vitu huku majuu? Yaani hata manukato watu wanapenda ya huku. Kuna watu wanafanya biashara za kununua manukato na biadhaa zingine za Victoria's Secret, kwa mfano, na kuzituma huko bongo nyoso. Kwa nini unadhani?



Nami mtazamo wangu ni kwamba Tanzania bado ni nchi ya dhiki sana. Tu wategemezi wa mambo mengi sana. Hata vinywaji baridi vingi bado ni vya kigeni. Hiyo Coca Cola na products zake zingine ni za Kimarekani. Yes, Atlanta, Georgia's very own. Walau Azam wamekuja na cola yao lakini hata wao ni kuiga tu. Hakuna ubunifu hata kidogo.

Bottomline Tanzania opportunities bado sana. Kama mtu hauko well connected na/au kama huna deep pockets kwa kiasikikubwa we ulie tu. Lakini Marekani huhitaji kuwa na jina kubwa. Waweza kuitwa Nyani Ngabu na uka-make it vile vile. Hata usipokuwa milionea, if you work hard enough, if you play by the rules, and if you are disciplined , then you will lead a very decent life.

Halafu, hivi kwa nini huko bongo nyoso watu wanafuatilia sana yatokeayo majuu. Yaani unakuta mtu anajua kinachoendelea Marekani kuliko hata walio Marekani! Watu wanafuatilia TV series utadhani sijui nini. Hivi huko hamna TV series zenu hadi mfuatilie za Marekani na kwingineko?

Na mashauzi ya kujifanya hujui Kiswahili. Mtu akiongea maneno matatu basi ya Kiingereza lazima yawe mawili. Kwa nini iko hivyo?

kiongozi,asante kwa hoja zako,japo nimejiuliza hukuwa na chochote cha kuzungumza kuhusu nilichokizungumza ktk no 1?

well,sina hakika unakuja tanzania mara ngapi au hata ukija unachukua hata nusu sekunde kutathmini mabadiliko yanayotokea kila siku,cha muhimu ni hali ya kubadilika bila kujali yametokea kwa kiasi gani!najisikia vibaya kukuambia una mawazo na mitizamo isiyoendana na tanzania ya sasa!mambo yamebadilika mno kiongozi

1.siku hizi karibia kila kitu unachokitaka unapata tanzania,iwe kwa kuagiza mwenyewe au kununua dukani,kuna tofauti ndogo tu ya muda toka kitu kinatoka na kupatikana hapa!mfano hapa arusha product yoyote ya apple iliyoko sokoni huko kwenu inapatikana benson!hao wanaowasumbua kutaka muwaletee vitu toka mtoni wangewasumbua kutaka kununuliwa vitu hata kama mngekuwa hapa bongo!

2.kazi za sanaa za mtoni,kaka kama uliondoka tz enzi zile za vibanda vya kanda vimejaa album za kina rkelly na aaliyah na mikanda ya kina chuck norris na kinaijeria mambo yamebadilika mno kiongozi,siku hizi tunasikiliza nyimbo za kina diamond,tunaangalia movie za kibongo,hakuna tena comedy za steve tunaangalia futuhi na ze comedy,na karibuni wabongo wataanza kutoa tamthilia zinazobamba nitakujulisha tu,lakini siku hizi za ulaya na marekani yenu hatuangalii kaka,tunamalizia kuangalia za marekani ya kusini na asia kisha tutajikita kwenye zetu!mark my words!

3.kuhusu kufuatilia yanayojiri marekani ni ktk kutaka kujifunza kaka,wabongo siku hizi tunafyatua vitu vyetu wenyewe baada ya kujifunza sana toka huko,mfano sioni umuhimu tena wa kuangalia oprah show wakati ipo inayonigusa na kunibamba zaidi ya mboni show!hata video za music za bongo ni za ukweli sana lakini hiyo ni baada ya kujifunza toka huko walikoendelea zaidi walikokuendeleza wenzako ambako kwa hakika huna haki ya kujivunia maendeleo yaliyofanywa na wenzako katika nchi zao!

4.bongo ya sasa kufanikiwa huhitaji support au connection kama bongo uliyoiacha zamani,leo hii mtoto wa mkulima ni waziri mkuu,no wonder kesho mtoto wa mfugaji akawa rais!diamond mtoto wa tandale anamiliki assets za mamilioni ya tzs,na tena ninakuambia tena kwa herufi kubwa USISHANGAE NDANI YA MIAKA 20 IJAYO JINA LA TILLY CHIZENGA UKALIKUTA KTK LEVEL ZA ALIKO DANGOTE!tena nikifikia huko nikiwa hapahapa bongo!hapa ni kupambana tu ukiwa na malengo huku ukijua njia ya kuelekea mafanikio utafanikiwa tu kama ilivyo marekani

kwa kumalizia,opportunities zilizopo ulaya na kila kitu ambacho kipo ulaya na marekani hata kama leo hatuna au tunavyo kwa uchache na uhaba na uduni ni jukumu la kila mtanzania kuzitengeneza na kutengeneza yaliyo bora kwa nchin yetu!kuwa kwetu mbali na nchi yetu hakutufanyi tukaacha kufanya vitu kwa ajili ya nchi yetu,nikiwa kama mtanzania niliyeko ndani ya nchi yangu nahitaji kuiendeleza nchi yangu sio peke yangu bali kwa ushirikiano na watanzania wenzangu popote walipo DUNIANI ukiwamo wewe NN,hivyo ninaomba ushirikiano nawe/nanyi ktk kutekeleza adhma hiyo.KARIBU KATIKA UMOJA NA USHIRIKIANO
 
kiongozi,asante kwa hoja zako,japo nimejiuliza hukuwa na chochote cha kuzungumza kuhusu nilichokizungumza ktk no 1?

Ukiona hivyo ujue hicho ulichoandika kwenye hiyo namba 1 ni utumbo.

well,sina hakika unakuja tanzania mara ngapi

Nakuja sana pengine kuliko hata unavyodhania. Hebu kisia tu mara ya mwisho mimi kuja ilikuwa lini.

au hata ukija unachukua hata nusu sekunde kutathmini mabadiliko yanayotokea kila siku,

Kwako muda wa kutosha ili kuweza kupata tathmini nzuri ya mabadiliko yanayotokea kila siku ni upi? Siku tatu? Wiki moja? Wiki mbili? Ama mwezi?

cha muhimu ni hali ya kubadilika bila kujali yametokea kwa kiasi gani!

Hapana, cha muhimu ni mabadiliko ya kweli ambayo yanaonekana at the grass roots level. Mabadiliko ambayo yanaonekana kwa 0.5 % ya wenye nacho hayo si mabadiliko ya kweli. Halafu, mabadiliko ya kweli ni ya watu na hali zao. Mabadiliko ya kweli si ya vitu ambavyo hata wengi wa watu at the grass roots level hawavifurahii kwa urahisi.

najisikia vibaya kukuambia una mawazo na mitizamo isiyoendana na tanzania ya sasa!

Sawa, huo ni mtazamo wako. Lakini mimi bado kabisa niko ndani ya mguso wa kinachoendelea ndani ya Tanzania.

mambo yamebadilika mno kiongozi

Mambo gani? Ya visimu vya mkononi na vi-cable na satellite TVs? Je mambo ya viwango vya maisha ya Mtanzania wa kawaida yamepanda? Je kipato cha Mtanzania wa kawaida kimepanda? Na kama kimepanda, ni kimepanda kwa kiwango gani? Kimepanda kutoka kiasi gani na kwenda kiasi gani? Je huduma muhimu kama afya, elimu bora na si bora elimu, maji, na umeme zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote? Je rushwa ndogondogo nayo imepungua? Kama imepungua, ni imepungua kwa kiwango gani?

1.siku hizi karibia kila kitu unachokitaka unapata tanzania,iwe kwa kuagiza mwenyewe au kununua dukani,kuna tofauti ndogo tu ya muda toka kitu kinatoka na kupatikana hapa!mfano hapa arusha product yoyote ya apple iliyoko sokoni huko kwenu inapatikana benson!hao wanaowasumbua kutaka muwaletee vitu toka mtoni wangewasumbua kutaka kununuliwa vitu hata kama mngekuwa hapa bongo!

Unaona sasa....wewe umepotoka kabisa. Umeonyesha dhahiri kwamba dhana yako ya maendeleo ni ya vitu na siyo watu. Kwa taarifa yako maendeleo ya kweli huwa ni ya watu na siyo vitu. Upatikanaji wa vitu ni ancillary tu kwa maendeleo ya watu.

Na hivyo vitu unavyovizungumzia kwa Mtanzania wa kawaida atumiaye riziki halali viko almost out of reach kwa yeye kuvipata. Get real dude.

2.kazi za sanaa za mtoni,kaka kama uliondoka tz enzi zile za vibanda vya kanda vimejaa album za kina rkelly na aaliyah na mikanda ya kina chuck norris na kinaijeria mambo yamebadilika mno kiongozi,siku hizi tunasikiliza nyimbo za kina diamond,tunaangalia movie za kibongo,hakuna tena comedy za steve tunaangalia futuhi na ze comedy,na karibuni wabongo wataanza kutoa tamthilia zinazobamba nitakujulisha tu,lakini siku hizi za ulaya na marekani yenu hatuangalii kaka,tunamalizia kuangalia za marekani ya kusini na asia kisha tutajikita kwenye zetu!mark my words!

Wewe ni kichekesho kweli. Jana tu nimetoka kuangalia Divorce Court ya Judge Lynn Toler kwenye ITV.

3.kuhusu kufuatilia yanayojiri marekani ni ktk kutaka kujifunza kaka,wabongo siku hizi tunafyatua vitu vyetu wenyewe baada ya kujifunza sana toka huko,mfano sioni umuhimu tena wa kuangalia oprah show wakati ipo inayonigusa na kunibamba zaidi ya mboni show!hata video za music za bongo ni za ukweli sana lakini hiyo ni baada ya kujifunza toka huko walikoendelea zaidi walikokuendeleza wenzako ambako kwa hakika huna haki ya kujivunia maendeleo yaliyofanywa na wenzako katika nchi zao!

Okay.....

4.bongo ya sasa kufanikiwa huhitaji support au connection kama bongo uliyoiacha zamani,

Hivyo eeeh?

leo hii mtoto wa mkulima ni waziri mkuu,no wonder kesho mtoto wa mfugaji akawa rais!

Mfano dhaifu sana huo.

diamond mtoto wa tandale anamiliki assets za mamilioni ya tzs,na tena ninakuambia tena kwa herufi kubwa USISHANGAE NDANI YA MIAKA 20 IJAYO JINA LA TILLY CHIZENGA UKALIKUTA KTK LEVEL ZA ALIKO DANGOTE!

You are a character. I'm finding it hard to take to you seriously with these kind of arguments! But "good lucky", nevertheless.

tena nikifikia huko nikiwa hapahapa bongo!hapa ni kupambana tu ukiwa na malengo huku ukijua njia ya kuelekea mafanikio utafanikiwa tu kama ilivyo marekani

Haya, "good lucky" bwana.

kwa kumalizia,opportunities zilizopo ulaya na kila kitu ambacho kipo ulaya na marekani hata kama leo hatuna au tunavyo kwa uchache na uhaba na uduni ni jukumu la kila mtanzania kuzitengeneza na kutengeneza yaliyo bora kwa nchin yetu!

Hii ni kweli kabisa na hapa ninakubaliana na wewe.

kuwa kwetu mbali na nchi yetu hakutufanyi tukaacha kufanya vitu kwa ajili ya nchi yetu,

Ni kweli kabisa. Na mimi sijai-abandon nchi yangu.

nikiwa kama mtanzania niliyeko ndani ya nchi yangu nahitaji kuiendeleza nchi yangu sio peke yangu bali kwa ushirikiano na watanzania wenzangu popote walipo DUNIANI ukiwamo wewe NN,hivyo ninaomba ushirikiano nawe/nanyi ktk kutekeleza adhma hiyo.KARIBU KATIKA UMOJA NA USHIRIKIANO

Naam, hapa pia tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom