Bongo is still surviving | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo is still surviving

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Whisper, Jun 8, 2009.

 1. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Omar Bongo wa Gabon "bado mzima"

  Imeandikwa na Mwandishi wa BBC

  [​IMG]
  [​IMG][​IMG]
  Gabon imekuwa katika uhusiano mzuri wa kiuchumi na Ufaransa Serikali ya Gabon imekanusha vikali taarifa zilizoendezwa na vyombo vya habari vya Ufaransa kwamba Rais wa nchi hiyo Omar Bongo amefariki dunia.
  Waziri Mkuu wa Gabon Jean Eyeghe Ndong amesema Bwana Bongo mwenye umri wa miaka 73 ambaye iliarifiwa ana maradhi ya saratani, "yu hai na mwenye afya".
  Serikali ya Hispania ambako kiongozi huyo mwenye muda mrefu madarakani barani Afrika anatibiwa katika kliniki moja, pia imesisitiza kiongozi huyo yu hai.
  Bwana Bongo ameiongoza Gabon tangu mwaka 1967, lakini mwezi wa Mei akasitisha kazi zake. Anakabiliwa na uchunguzi wa Ufaransa kuhusiana na tuhuma za madai ya rushwa.
  Mwandishi wa BBC mjini Libreville Linel Kwatsi amesema mji huo inaonekana upo kimya kama ilivyo kawaida, hata hivyo baadhi ya watu wameanza kukusanya chakula kwa wingi nyumbani, iwapo maduka yatafungwa kama kifo cha rais kitathibitishwa.
  Serikali ya Gabon yenye utajiri wa mafuta imewataka watu kuwa watulivu.
  Shirika la habari la Ufaransa-AFP lilitangaza kifo cha kiongozi huyo wa Gabon baada ya kunukuu rubaa za serikali na pia tovuti ya gazeti moja la Ufaransa la magazine Le Point, zikikariri taarifa kutoka kwa walio katika msafara wa Bwana Bongo.
   
Loading...