Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

Mabaharia toka Buza tumefika, waweke fence tunarukaga ukuta... kama mafisi hatuachagi hata mifupaaaaa!! MIFUPA

Cha mtu mavi wanashikaga ukuta, bia tatu ila baadae utajuta!!

Gusanisha, nyama kwa nyama.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ndio pointi haswaaa….Likifanyiwa kazi hili kwa kuwatumia BASATA na TCRA …. tutatatua changamoto hiyo na kulinda maadili na Sanaa..Big up ndugu
 

Mmmh
 
Shida ya wafrika hawajui wanachokitafuta.
Katika maisha kuna aina nyingi ya vitu/mambo kwahiyo unatakiwa uchague kile unachokihitaji. Shida ya wafrika hawana chaguzi, wenyewe chochote kinachokuja mbele yao wanataka kuchukua.
Ulimwengu wa sasa, ni wa pesa mbele. Muziki biashara, nani atasikiliza au kuangalia nyimbo yako umevaa dela? Angalia nyimbo ya Nick Minaj Anaconda au The one ya Dj Khalid.
Kuna nyimbo nyingi zipo lakini umeng'ang'ania mpelekee moto. Hiyo nyimbo ya mpelekee moto unajua inashika namba ngapi kwenye vituo vya radio na televishen? Ukipata jibu ujue tupo kwenye karne ya 21. Sasa hivi ukienda kila mkoa utakuta maeneo maarufu ya wadada wanauza miili yao. Hata haushituki? Si shabikii haya mambo ila ujue kuwa ulimwengu umebadilika na tunapaswa kuchague kile kinachokufaa ww.
Mkuu mzee ni nani?, ninavyojua wazee mziki wao ni rhumba za taratibu za akina mbaraka na marijani.
 
"mpelekee moto"

Naona ichi kipande huwa unakitafakari sanaπŸ˜€πŸ˜€πŸ€£πŸ€£

Yaani hawa watu watatu wamekuja na mziki wa peke yao Baddest47, Whozu na Young lunya.
 
"Hizo bia unazomnunulia brother ukipiga kimoko ukalala atatangaza ,sio pesa usipokaza utaitwa kilaza ,we mpelekee moto peleka motooooo"

Haahaaaa

Lunya sasa

"Harafu akiwa ameshoboka na ofaa za bia akasahau kumpelekea moto itafatia ....

Pisi nyingine zinatabia za kitoto nishatuma nauli kufika ndio changamoto ,akifika geto hakuna story Wa maji mpelekeeee motooo pelekaaa motooo"


Aisee hili gomaa linabamba redion....
 
Dah mimi kwa sasa mpk naona aibu,kuna mziki nimeusikia jana eti kiitikio "wazungu hao wazungu hao"
 
Lugha yao ilikuwa na staha sana..

Walitumia sanaa yao vizuri..

Sio hawa wa sasahivi wanachana waziwazi..

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kama utakuwa unafikiri vizuri,utaona tofauti kati ya wimbo wa matusi na wimbo wa mapenzi.

Siwalaumu sana wasanii wa sasa kwa vile wengi IQ yao ni ndogo.Badala ya kuimba nyimbo za mapenzi kama walizoimba wanamuziki wa zamani,mfano Marijani,na wengine wengi,wao wanaimba matusi live.Sijui nataka muhogo,ingiza yote,sijui nasikia utamu nikimumunya..na ujinga kama huo.

Ninachoona kwa wengine kama sisi,inanisaidia sana kuishi kwa utulivu masaa mengi kwa vile sifungui Redio na nikuwasha TV kama ni lazima ninai mute tu na kusibiria taarifa ya habari ama vipindi vya kuelimisha.

Nyie endeleeni tu sie wengine tulishaacha kusikiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…