Mbogela
JF-Expert Member
- Jan 28, 2008
- 1,384
- 261
Leo tunasherekea sikukuu nikiwa na furaha kwa ajili ya vijana wetu wanaoimba mziki wa Kitanzania ambao umekuwabranded kama Bongo Flava.
Nakumbuka Katikati ya miaka ya 1990 walijitokeza vijana wachache wakati huo waliamua kuimba mziki fulani wenye radha kama ya kimarekani kiasi fulani, kitanzania na makabila yetu kwa upande mwingine. nakumbuka wakati huo ndio redio binafsi kama redio one ndio zilikuwa zinaanza. Hawa vijana akiwemo Mh. Sugu (Mr. II), Afande sele, Uswahilini Matola, Mr. Paul, Sister P, Zay be na akina Lady Jay de ndio walikuwa wana introduce nyimbo zao za machozi. Watu wazima na vijana wa umri mkubwa kidogo wa wakti huo hawakupenda mziki huo, kwanza uliitwa mziki wa kihuni, baadaye ukaanza kuitwa mziki wa kizazi kipya.
Kadri muda ulivyokuwa unaenda ndivyo hawa washikaji walivyozidi kulazimisha soko kuwakubali. Kila kukicha tukawa tunasikia mwanamziki mpya na muziki mpya ukizaliwa. Ikawa hakuna namna, jamii ikabidi iupokee mziki huu na kuuchukua kama mziki wetu, mziki wa Bongo, mziki unaohitaji kutumia Bongo kwa watu wanaoishi Bongo. Na ndipo ilipofika mahali kila mtu angependa kujiassociate na BongoFlava maana ni mziki wetu. Hongera sana Bongo Flava.
Tumetoka mbali lakini kuna mtu ambaye sitamsahau katika mchango wake kwenye bongo flava, bila ujasiri wake historia ya bongo flava ingekuwa tofauti sana, naye ni si mwingine ni Master J.
Inasemekana Master J alikuwa anaishi Marekani (Hizi ni habari za kusimuliwa sina uhakika na ukweli wake), wakati anarudi alibeba vifaa kadhaa vya muziki, kinanda, amplifier, komputa nk. Inadaiwa kuwa Alivofika home akatengeneza studio kwenye chumba chake cha kulala. Kazi ikaanza, kutoka kwenye chumba hicho kuna album nyingi sana zilitengenezwa na baadaye Master J alikuja kuwa producer mmoja mkubwa sana ambaye alikuja kuwatengenezea nyimbo mpaka kwaya kubwa za nyimbo za injili kama Upendo group na wimbo wao wa Mungu anakupenda.
Baada ya Master Jay wakaja maproducer wengine wengi kama akina P Funky, Allain Mapigo, akina Man walter, nk hawa walisaidia bongo flava ipae kwa kweli, Hawa ningependa niwaite Bngo Flava Producers. Baadaye tukawa sasa kwenye discos tunapigiwa nyimbo kadhaa za bongo flava na baadaye sana disco zimekuwa zikibeba nyimbo nyingi za bongo Flava kuliko hata za wageni.
Lakini mwaka 2014 umeisha na mambo mazuri ya kujivunia kwenye Tasnia ya Bongo Flava. Tumeona wanamuziki wetu wakiwa nominated kuwania Tuzo kwenye vyombo vya kimataifa.
Tumeona Diamoni Platnumz akiwania Tuzo za BET, MTV, lakini mafanikio makubwa zaidi ni pale tulivyoona kijana wetu Diamond akiiwakilisha Tanzania vyema kwa kunyakua tuzo 3 kwa mpigo tuzo za Channel O. Haya kwa kweli ni mafanikio makubwa sana kwa nchi.
Jambo lingine ni mapinduzi katika video, video za bongo flava zimekuwa za quality nzuri sana, ni video ambazo ukiziona zimepangiliwa na zina ubora unaokubalika kwa kweli.
Hata hivyo mwaka wa 2014 nimependa namna ambavyo wana mziki wetu wamefanikiwa kuvuka miaka ya nchi yetu na kuweza kuiga katika nchi za watu wengine. Mwaka unaisha tukiwa na ngoma kama 4 za diamond na waimbaji wa nje hasa wa Nigeria na South Africa, tumemaliza mwaka tukiona wimbo wa AY wa Touche ambao amemshirikisha Kingston, wimbo ni mzuri ambao nadhani utavuta attention sehemu mbali mbali za dunia, Kwa project ya Ay na Kingstone tayari Tanzania tumeshaingia kwenye masoko ya Marekani, jambo ambalo ni lazima tujivunie na kushukuru kwa vijana wetu kutuvusha pacific. Wimbo wa Diamond na Waje wa Coco Baby nadhani ni wimbo ambao Club mbali mbali za muziki na vituo vya redio barani Africa vitaupiga sana. Sasa unakuja wimbo wa Diamond na Bracket, ni wimbo mpya lakini tayari umeshachukua nafasi kubwa kwenye media na clubs mbali mbali
Kwa dhati krismass hii niwapongeze vijana wetu wana Bongo flava kwa kuuvusha muziki wetu kwenye another Level.
HONGERENI BONGO FLAVA NAWATAKIA MWAKA 2015 WENYE MAFANIKIO