Bonge la Marketer

Bonge la Marketer

Amba Samedi

Senior Member
Joined
Apr 5, 2024
Posts
193
Reaction score
326
Habari wanaJF,
NIPO kwenye basi la Laviha inayotoka Dar kuelekea Ifakara. Tupo mkambarani tunakaribia Moro.

Sasa ameingia jamaa mmoja hivi na dawa ya meno ya Vigo Doctor. Akajitambulisha, shughuli ikaanza.

Alivyoishika mfuko wa bidhaa, akaelezea Aina zake na mabadiliko yaliyokuwepo. Akaelezea faida, na product inavyofaa watoto, watu wazima na wenye meno mabovu.

Akaelezea miswaki kwa ina yake, na mwisho akatoa ofa (mswaki na dawa kwa elfu 2)

Bwana ee! Abiria si wakamwagika. Miito ya "leta hapa" si ikawa mingi. Jamaa aliuza aisee.

Soko ni lugha, ni presentation skills, ni emotional connection. Kaka huyu alikuwa nazo zote.

Siku tukijifunza kuuza, fursa zitafunguka.
 
Jamaa kashusha bei, huwa wanauza 5000, na watu wananunua sana tu.

Huwa najiuliza hawa wanunuzi ni kweli kabisa hawazijui hizo dawa au maeneno tu wameingia line.

Kuna wale wauza sabuni pia na dawa za mitishamba za ajabu ajabu nao hivyohivyo, marketing skills tu.
 
Hizo dawa wataziona expire date 2023 wakifika home, na mswaki mkali km brush la kusugulia viatu.!!
Sio kweli. Nimezinunua mwenyewe na watoto wanaenjoy kuzitumia. Mswaki wao mzuri kweli. Works as advertised.
 
Jamaa kashusha bei, huwa wanauza 5000, na watu wananunua sana tu.

Huwa najiuliza hawa wanunuzi ni kweli kabisa hawazijui hizo dawa au maeneno tu wameingia line.

Kuna wale wauza sabuni pia na dawa za mitishamba za ajabu ajabu nao hivyohivyo, marketing skills tu.
Soko huwa haijali so much about your product as about your presentation. Unaweza kuwa na product ya kiuchwara, lakini ukabebwa na chutzpah. Tujifunze kuuza (wauzaji wazuri hawafikii asilimia 10 duniani leo).
 
wanakutisha kwanza kwa kukuambia usipotumia bidhaa yao utapata madhara gani...au bidhaa zao zinapambana kuondoa madhara fulani, wakishakusisimua....wanakuambia dukani inauzwa bei juu na haipatikani kirahisi...
then wanakuambia bei ya bidhaa ni kiasi fulani alafu wanakuambia kwa siku hiyo wana bei ya ofa bab kubwa...
 
Soko huwa haijali so much about your product as about your presentation. Unaweza kuwa na product ya kiuchwara, lakini ukabebwa na chutzpah. Tujifunze kuuza (wauzaji wazuri hawafikii asilimia 10 duniani leo).
Ndio maana huwa nawashangaa wale waongeaji sana kwann sio matajiri 😂😂😂, maana ni kama dunia ya sasa inawapa favour fulani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom