Bondia Mada Maugo Ajiunga na CHADEMA leo Tarehe 08/06/2013

Bondia Mada Maugo Ajiunga na CHADEMA leo Tarehe 08/06/2013

attachment.php
 
Watu wengi maarufu na wasio maarufu hawaipendi ccm! Sematu hawajataka kutangaza...
 
Wanamichezo na wasanii wanao litatakia mema Taifa lao ni LAZIMA wajiunge na Makamanda. Wanao taka kunyanyaswa waende CCM wakatumike kama ndomu. Muulize Nakaayah atakujuza kitu mbaya alichofanyiwa!
 
Sishangaii huyu bondia si wa mkoa uleeeee

Kwani huo mkoa uleee kuna Chadema tu?Amechagua njia sahihi.Hongera saana Mada Maugo,karibu ktk chama MAKINI kinachojali maslahi yetu watanzania.
 
Na orodha ya walio mbioni kujiunga na chama letu ni ndefu mno! Stay tunned.
Khaa!! ni ndefu, The late Mangwair naye alikuwa na mpango huo, Juma nature, Dudubaya, Wema, Zulfa, ...., ni wengi sana. Siasa ni sanaa inayolipa kuliko sanaa nyingine zote. Hawa jamaa wako smart wanawahi deals za kampeni 2015. wako kikazi. Bajeti ya kampeni 2015 lazima iwe ndefu sana:heh:
 
sasa mpaka leo hamjaweka picha yake huku wengine hatumfahamu
 
Salama WanaJF.

Bondia maarufu nchi Mada Maugo almaarufu King Junior amejiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.
Muda mfupi ujao atakabidhiwa kadi na mjumbe wa kamati kuu kamanda Wakili Mabere Marando.

Nitumie fursa hii kumkaribisha ndani ya Chadema King Junior ili tusaidiane kuendeleza mapambano dhidi ya mkoloni mweusi.

Peoples Power!
ni vyema sana watanzania wenye fani mbalimbali wajue kuwa wakati ule ambao walikuwa wakidanganywa na wanyonyaji weusi kuwa wasishiriki siasa umekwisha maana ilikuwa ni mbinu ya kuwaweka mbali wasijue nini waseme nani waseme naye na hata ikaleta uzito wa watu kufanya maamuzi ya msingi ndio maana hata dhana ya uwakilishi ilikuwepo na watu wa ajabu kama akina MWIGULU ,MAMA ANA ABDALLAH ,MAGEMBE NA MABOGA MAENGINEYO YA CCM sasa ndio angalau watu wa maana kama akina
MNYIKA ,LISSU ,WENJE, LEMA , WANAKUJA kuleta mapinduzi ya neno uwakilishi
karibuni sana wengine kama MADA MAUGO,akina prof J
kuna vijana mtakuja nao kama HECHE, CLLEO,MAWAZO, hawa pia wako nje ya bunge ila ni matumaini mnakuja nao
 
Salama WanaJF.

Bondia maarufu nchi Mada Maugo almaarufu King Junior amejiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.
Muda mfupi ujao atakabidhiwa kadi na mjumbe wa kamati kuu kamanda Wakili Mabere Marando.

Nitumie fursa hii kumkaribisha ndani ya Chadema King Junior ili tusaidiane kuendeleza mapambano dhidi ya mkoloni mweusi.

Peoples Power!

mada.jpg


Bondia Mada Maugo maarufu kama ‘King Junior', juzi amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Bondia huyo ambaye anapigana uzito wa kati, alikabidhiwa kadi jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Wakili Mabere Marando kwenye sherehe za kuchangia kampeni za udiwani Kata ya mianzini. Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa kadi hiyo Maugo alisema ameamua kujiunga na Chadema baada ya kuvutiwa na sera za chama hicho na kwamba siyo mambo mengine.

"Mimi ni kijana mpenda maendeleo, leo nimeamua kujiunga na Chadema kwa ridhaa yangu mwenyewe baada ya kuvutiwa na sera za chama hiki," alisema Maugo.

Alisema, "Kupitia uwepo wangu ndani ya Chadema nitatumia nafasi hii vizuri kwa kushirikina na vijana wengine ili kuhakikisha tunatafuta maendeleo na ukombozi wa nchi yetu."
 
Huu ni Mtizamo mzuri: Hivyo Waalimu, madaktari, wakulima, wafanyakazi, wafugaji, na wafanyabiashara acheni migomo isiyo na tija jiungeni na CHADEMA tujipange pamoja na kulikomboa taifa.

Tatizo wasomi wengi waoga wanaogopa kupoteza vibarua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom