Bomu la mafuta ya kula la Magufuli laanza kulipuka

Bomu la mafuta ya kula la Magufuli laanza kulipuka

nzagambadume

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
2,430
Reaction score
5,787
Kama ule mzaha ulivyofanyika kwenye sukari kwa madai kwamba zinafanyika juhudi za kushusha toka 1800 per kilo matokeo yake wavurugaji na wakurupukaji wakafikisha 2800 hadi 3000 per kilo kisha wakaingia mtini na kuuchuna kimya huku wakijisifu kwa kuwajali wanyonge na kuwa wazalendo wanaoinyoosha nchi,

Sasa wamekuja na kituko kingine hapa majuzi wakati wa mkutano na wafanyabiashara kuhusu MAFUTA YA KUPIKIA, waooh korie inapigwa vita kwa maneno ya shombo kwamba tutakamua hata karanga,tutapikia alizeti na mawese yaani yaleyale ya kwamba sukari ya nini tutatumia asali na miwa.Hahahahahaha

Hali iliyopo jijini mwanza ni kwamba wenye viwanda wa mafuta ya kula wana mgomo baridi, maduka ya mtaani wanakataa kununua toka kwa ma agents kwa bei iliyopanda
Kazi kwenu wapiga vigelevigele, mshangilie vizuri sasa, jiwe limewakamata vizuri mlizoea kwenda kwa mangi kununua vimafuta vya sh 200 kwenye chupa ya fanta, mmeambiwa mtumie alizeti

Natamani haya mambo yaendelee tena kwenye hiyo sekata ya chakula hadi wanyonge wapiga vigelevigele waipate fresh ya moto, mambo ni moootooooo.😀😀😀😀😀😀😀😀🙂
 
Muwe mnatafuta ukweli kabla ya kuposti vitu, au wewe ni mnufuaka wa wauza mafuta yaliyojaa sumu? Mnataka kumaliza watanzania na kansa kwa sababu ya kutengeneza pesa?
mizaha inaruhusiwa bwasheeee,hata sukari hiyo mizaha haikukosekana,hata mbaazi juzi watu wanalamika bei kushuka toka 2000 hadi 150 per kilo waziri anajibu kwamba zina protein ni vyema watu wazile kwa bei hiyo,sawa tu ila nafurahi sasa mnaanza kuwagonga watu pale patamu zaidi,nataamni yapande yatoweke kabisa ili muwaokoe na hizo sumu mnazosema
 
Ili mazuzu ya nchi hii yaamke unatakiwa kugusa chakula, maana tumbo ndio kitu pekee cha thamani ka watanzania, kuanzia profesa hadi mpiga debe wote wanaendeshwa na matumbo yao tu.
nimefurahi sana,nimeshuhudia wamama wakaanga vitumbua wakilalamika,nimefurahi jiwe la chato linapiga kwenye tumbo,natamani avuruge kote kwenye misosi ili majinga akili ziwakae sawa
 
Nasikia lita 20 tsh 65000,
lita 10 tsh 38000.

Inabidi kula chukuchuku tu,maana bei ni uneconomical
 
Hivi kwani mkulu hakuikuta sukari sh.5,000 akaishusha hadi sh.2,500? Au masikio yangu hayana ushirikiano? Au mleta mada unataka tu kunigombanisha na mkulu? Maana nilimsikiaga mwenyewe pale Arusha akisema ameshusha bei na tukashangilia kwa nguvu sana.
 
Nasikia lita 20 tsh 65000,
lita 10 tsh 38000.

Inabidi kula chukuchuku tu,maana bei ni uneconomical
wenye maduka ya rejareja mwanza wanakataa kununua kwa bei mpya,give it 0ne to two weeks utasikia balaa halafu atajifanya anaingilia kati ku solve tatizo wakati yeye ndo ka create,sijui huyu jamaa tumemkosea nini yarabi
 
Hivi kwani mkulu hakuikuta sukari sh.5,000 akaishusha hadi sh.2,500? Au masikio yangu hayana ushirikiano? Au mleta mada unataka tu kunigombanisha na mkulu? Maana nilimsikiaga mwenyewe pale Arusha akisema ameshusha bei na tukashangilia kwa nguvu sana.
Jamaa sidhani kama ana nia nzuri na nchii hii,kiuwkeli,wafanyabishara wa mafuta ya kula wanalalamika yeyey ana wa direct kwa pm ambaye mwenyewe hajui cha kufanya kwa mujibu wa wadau nilio nao karibu kwa hiyo kila mtu kasusa sasa hivi mafuta ya kula yatatoweka madukani utasikia anajifanya ni vita ya kiuchumi na mabeberu tukamue karanga
 
nimefurahi sana,nimeshuhudia wamama wakaanga vitumbua wakilalamika,nimefurahi jiwe la chato linapiga kwenye tumbo,natamani avuruge kote kwenye misosi ili majinga akili ziwakae sawa
tutatumia chukuchuku,hamna tabu kabisa,

au tutarudi enzi za mwalimu kutumia samli.

Hii ni oppotunity nzuri sana ya kujiajiri,
kukamua mafuta ya mawese na samli,

mimi niko india hapa anaehitaji mashine ndogo portable ya kutenganisha maziwa na siagi anione
 
Wacha akili za watanzania zianze sasa kuamka, tumbo linaguswa.
Baada ya mafuta ya kula kupanda, huenda kitakachofuata ni Condom kupanda bei.

Kwa jinsi watanzania wanavyopenda ngono, watakuwa wanazifua Condom na kuzianika ili zikikauka warudie kuzitumia tena.
 
Nasikia lita 20 tsh 65000,
lita 10 tsh 38000.

Inabidi kula chukuchuku tu,maana bei ni uneconomical
Leo lita 20 imeuzwa 66,000/= na mzigo wa kimbo umeingia jion hii wamesema bei imepaa so kesho lita 20 yaweza kuuzwa 68000
 
Back
Top Bottom